Serikali: Rada ya Chenge imechoka; Usalama wa anga sasa upo shakani!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,477
2,000
*Waziri ashangaa, ashauri inunuliwe nyingine
*TCAA yasema moja haitoshi, zinahitajika tano

HATIMAYE Serikali imekiri kuwa rada inayotumika kwa ajili ya kulinda usalama wa anga nchini, imechoka. Kutokana na hali hiyo, usalama wa anga la Tanzania upo shakani, kutokana na ubovu wa rada hiyo ambayo ni muhimu kwa ajili ya usalama wa anga.


Taarifa hizo za majonzi kwa Serikali, zilielezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba alipotembelea Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), jijini Dar es Salaam jana.

Dk. Tizeba, alisisitiza umuhimu wa Serikali kununua rada nyingine haraka iwezekanavyo, ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea kutokana na ubovu huo.

Dk. Tizeba alikiri kuwa amepata maelezo juu ya utendaji kazi wa rada hiyo, yanayotia wasiwasi kuhusu usalama wa anga hasa kwa usafiri wa ndege.

Kutokana na hali hiyo, ameitaka mamlaka husika kuwasilisha maombi mapema ofisini kwake, ili jambo hilo liweze kuingizwa katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014.

“Ni kweli rada yetu imechoka….kwa hili tusiweke mzaha kuna umuhimu wa kununua rada nyingine haraka iwezekanavyo, tukiendelea na mtindo wa kulilea tatizo hili siku moja litatuaibisha jamani,” alisema Tizeba.

Mapema Agosti, mwaka huu rada hiyo ilishindwa kufanya kazi baada ya kuharibika kifaa (Power Supply Unit) ambacho kiliigharimu Serikali Sh milioni 40.

Rada hiyo, ilinunuliwa kutoka Kampuni ya BAE System ya Uingereza kwa Sh bilioni 40 na hivyo kuibua mjadala mkubwa, baada ya kubainika bei hiyo, ni kubwa kinyume na bei halisi.

Rada hiyo, ilinunuliwa kwa ushauri wa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati huo, Andrew Chenge ambaye sasa ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM).

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TCAA, Fadhili Manongi alisema mamlaka yake inafanyakazi katika wakati mgumu, kutokana na rada hiyo kusuasua.

Hata hivyo, Manongi alisema kulingana na ukubwa wa anga la Tanzania rada moja haitoshi na kusema Tanzania inapaswa kuwa na rada zisizopungua tano, ili kuongeza ufanisi wa usalama wa anga.

“Anga la Tanzania ni kubwa ikilinganishwa na maanga ya nchi nyingine za Afrika Mashariki, wenzetu Kenya wanatumia rada tano.

“Wanatumia rada tano kwa hivi sasa, licha ya anga yao kuwa ndogo kuliko ya kwetu, iweje sisi tuendelee kutumia rada moja tena iliyochoka na ukiangalia bei ya rada kwa sasa imeshuka kwa kiasi kikubwa,” alisema Manongi.

Alisema mamlaka yake inalazimika pia kufanya kazi katika anga ya Rwanda na Burundi na inatarajia kutumia Sh milioni 102, kwa ajili ya kutengeneza kituo kipya eneo la Kasulu, ili kuongeza ufanisi.

Taarifa hiyo ilimshitua naibu waziri, ambaye alihoji kama huduma za TCAA nchini Rwanda na Burundi zinalipiwa.

“Inakuwaje mnahudumia mataifa hayo, mnafaidika nini…kama hawawalipi inabidi wachangie gharama za kituo cha Kasulu…sababu mambo ya kubeba majukumu ya taifa lingine ni ya kizamani na tukiendelea hivi wanatudharau,” alisema Dk. Tizeba.

Mkurugenzi wa TCAA alikiri mamlaka yake hailipwi chochote na nchi hizo na wanafanya hivyo kwa kufuata agizo la Mamlaka ya Kimataifa ya Usalama wa Anga, (ICAO).

“Kwa kuwa nchi hizi zina eneo dogo la anga, kwa kuanzia umbali wa mita 24,500, inabidi tuwahudumie na hii inatokana na agizo la Mamlaka ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (ICAO),” alisema Manongi.

Chanzo: Mtanzania | Nov 30, 2012
 

MR. ABLE

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,471
2,000
Tanzania tunautajiri wakutosha sema tu baadhi ya viongozi hutumia madaraka yao kwa manufaa yao binafsi.
 

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,850
2,000
Tanzania tunautajiri wakutosha sema tu baadhi ya viongozi hutumia madaraka yao kwa manufaa yao binafsi.

mkuu umeongea kidhaifu sana,hatuna tena muda wa kusema,,sema tu,,, hiyo sentensi ndiyo imetufikisha hapa tulipo
 

Kifulambute

JF-Expert Member
May 8, 2011
2,476
2,000
kila kukicha nachukia kuwa Tanzania na kero zake ndizo zinanifanya niishiwe nguvu...iweje uhudumie nchi nyingine wakati wewe huna uwezo na nchi yako?
 

tusichoke

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
1,313
1,250
na bado wahusika wa hiyo rada wanapigiana debe la kwenda ikulu ili madili ya kuimaliza tz kiuchumi yakamilike ;kweli tunaelekea kubaya mungu atuepushe
 

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,728
2,000
mkuu umeongea kidhaifu sana,hatuna tena muda wa kusema,,sema tu,,, hiyo sentensi ndiyo imetufikisha hapa tulipo

Ndugu yangu nawe umeonyesha udhaifu pia cha muhimu unapomkosoa mtu basi mpe na mbinu ya kufanya kuondokana na hicho alichokosea.
 

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,743
0
'wenzetu kenya wana rada 5'
nimenukuu tu hapo,
'sisi tuna anga kubwa kuliko nchi nyingine za afrika mashariki'Nukuu nyingine hii.
 

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,563
2,000
'wenzetu kenya wana rada 5'
nimenukuu tu hapo,
'sisi tuna anga kubwa kuliko nchi nyingine za afrika mashariki'Nukuu nyingine hii.

Tena tunatumia rada moja tu,inayosuasua.

Tanzania kichwa cha mwendawazimu.
 

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,589
2,000
Watanzania tulishaambiwa hata Nyasi tutakula bali Rada ije! Sasa tujiandae kula majani ya ***** Rada ingine iagizwe! I Salute Kikwete na serikali yako.
 

Mwanaweja

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
3,576
1,195
ccm inatafuta hela ya uchanguzi 2015 tuweni makini jamani yaani hawa watu hawana haya/soni wameshakuwa mafisadi, wezi na pengine wahujumu jchumi wetu. sioni haja ya kununua rada kama ndani ya nchi tu kuna vingugumkuti vingi tu vinafanyaika bila hata usalama wa taifa kujua je, kweli rada inaweza kutusaidia?
 

Mimibaba

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
4,558
1,195
ccm inatafuta hela ya uchanguzi 2015 tuweni makini jamani yaani hawa watu hawana haya/soni wameshakuwa mafisadi, wezi na pengine wahujumu jchumi wetu. sioni haja ya kununua rada kama ndani ya nchi tu kuna vingugumkuti vingi tu vinafanyaika bila hata usalama wa taifa kujua je, kweli rada inaweza kutusaidia?

Hivi kwa nini serikali asituambie mafanikio ya usalama wa anga ambao umeletwa na hiyo RADA? Mimi binafsi nakubaliana na wewe kuwa hili ni dili la CCM; na kama siyo dili la CCM ni dili la mataifa yanayofaidika na hiyo RADA. Nitashukuru kama kuna mtu atajitokeza na kunieleza manufaa ya hiyo RADA kwa mimi mtu wa kawaida toka inunuliwe.
 

Mvuni

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
343
195
usalama gani huo? mbona haupo kabisa !! nchi ipo ipo tu... inaendeshwa kwa mungu nisaidie...
 

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Nov 7, 2012
1,970
2,000
Kama sikosei ilikuwa mwaka 2001/2002 nikiwa form two au one kulipoobuka mjadala mkali juu ya ununuzi wa ndege ya raisi na rada nakumbuka wakati huo waziri wa fedha alikuwa Mlamba na ndo ikatoka kauli moja kwamba ni heri watanzania wale nyasi lakini vitu hivyo vinunuliwe, nakumbuka pia watanzania kwa ujumla wao walipingana sana na matumizi hayo hasa ununuzi wa rada.

Kiukweli mjadala huo haukuwahi na wala haujawahi kuisha hasa ukizingatia bei ya vitu hivyo viwili, japo nilikuwa mdogo lakini kwa uelewa wangu watanzania hawakupinga umuhimu wa vitu hivyo lakini kikubwa ilikuwa ni gharama zake ukilinganisha na uchumi wa nchi yenyewe, mjadala ukaibui mengi mwisho wa siku ikaonekana watanzania tuliingizwa mkenge hadi leo kuna kitu kinaitwa change ya rada ambayo hadi sasa wtanzania hawaelewi mchanganuo wake na hatua za kuwachukulia wale walio husika.

Karibu miezi mitatu sasa mwaka huu kumekuwa na tetesi nyingi na taarifa vilevile kuhusu rada hiyo wengine wakisema mbovu, kesho imepona nk. ni leo tu naibu waziri wa usafirishi ameripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kama magazeti vimemnukuu akisema kuwa rada hiyo imekufa kabisa hivyo inahitajika mpya haraka kwa usarama wa nchi.

Serikari hapa moja

Imeumbuka sana kwani ni serikali ile ile ya CCM ndiyo iliyopigia debe sana kwa njia zote ili rada hiyo inunuliwe bila kujali malalamiko na umaskini wa raia hasa ukizingatia ilikuwa ni kwa bei ya kuruka.

Pili, serikari imeadhibiwa kutokana na laana ya watanzania kwa kutokuwa sikivu, ikiwapuuza na kufanya maamuzi bila kuzingatia matakwa yao, hivyo basi hii ni laana tosha kwa Mkapa, chenge, mlamba na serikali ya ccm.

Mungu ibariki tanzania, mwenge kama ule wa wazamani uwachome mafisadi (sio huu wa sasa unaosambaza ukimwi tu)
 

Tabby

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
10,661
2,000
Maumivu yako kwa Mtanzania wa kweli. Mafisadi wanahasara gani? Kwanza wanafisadia raslimali zetu, pili kodi hawalipi na wala hiyo rada hawana mchango nayo na wao kusema wananunua nyingine kwa kama hiyo kwa wizi ule ule siyo tatiz. Wewe na mim ndio tunaochangishwa kwa lazima fedha za hayo manunuzi na gharama zake zote. Hi jambo la huzuri sana. Maskini tunazidi kuumizwa na hii serikali dharimu ya ccm.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom