Serikali: Polisi wameshindwa kuendelea na kazi ya upelelezi wa kesi ya shambulio la Tundu Lissu

CCTV hamjazing"oa? Kwa nini CCTV MMEZIFICHA?
Cctv anaweza akaziondoa mtu yoyote mwenye nia mbaya au mwenye huo mchongo wa lissu, lakini lissu mguu wake wakulia umepigwa risasi pia, hile gari y lissu ilipigwa risasi upande wa kushoto, mdio maana tunamuomba nadereva aje atupe dondoo mbili tatu tupate pakuanzia.
 
Tumesha kua donor country. Hii product, Tundu, iliyo tokea singida inamaket saana huko ulaya na marekani. Hata bunge letu kila siku hufuatilia mafanikio ya hii kitu kutokea singida; Otherwise, mambo hayaendi.
Mpaka 2020 ifike, possibility ya TZ kuwa donors wa demokrasia ni nzuri saana. 🙏🙏
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amelieleza Bunge kuwa Jeshi la Polisi limeshindwa kuendelea na kazi ya upelelezi wa kesi ya kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu lililotokea September 7, 2017 nyumbani kwake Dodoma wakati akitokea Bungeni.

Waziri Lugola akiwa Bungeni amesema kuwa wapelelezi wameshindwa kutokana na kwamba kwenye gari kulikuwa na watu wawili tu ambao ndio key witnesses.

Akaendelea kwamba anashangaa kwanini mpaka sasa dereva wa Lissu ameamua kuitelekeza kesi hiyo kwa kushindwa kuonesha ushirikiano.

----
Waziri wa mambo ya ndani ya nchini, Kangi Lugola amesema kesi ya kushambuliwa kwa risasi mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu imeshindwa kuendelea kutokana na mbunge huyo pamoja na dereva wake kushindwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwani wao ndiyo mashuhuda muhimu wa tukio hilo.

Lugola amesema hayo bungeni jana alipokuwa akijibu hoja za wabunge waliokuwa wakichangia taarifa ya kamati ya bunge ya mambo ya nje, ulinzi na usalama.

Lugola amesema siku hiyo ndani ya gari Lissu alikuwa na dereva wake ambao ni mashuhuda muhimu katika kesi hiyo (key witness).

“Kesi ya Tundu Lissu imetelekelezwa. Gari lilikuwa na watu wawili baada ya tukio hilo ‘key witness’ wamepotea katika mazingira ya kutatanisha.

“Ingawa ameshapona na kutoka hospitalini, kwa nini harudi kuja kutusaidia. Sisi hatuwezi kujua ni wembamba, wanene, aje ili atusaidie,” ameongeza.

Ametaka watu kutotumia mbinu zao kusema kuwa kesi zinacheleweshwa wakati hawataki kutoa ushirikiano.

Hata hivyo, wakati wote Lugola anaeleza hayo wabunge wa upinzani waliomba kutoa taarifa bila mafanikio baada ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kusema ameshakataa kutoa nafasi za taarifa wala mwongozo tangu awali.

Lissu alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 mchana wa Septemba 7, 2017 katika makazi yake Area D jijini Dodoma akitoka kuhudhuria vikao bungeni ambapo kwa sasa ametoka hospitali na anaendelea na ziara barani Ulaya na Marekani.
was inside job ndio maana dereva hakuchafuliwa hata shati....
 
Rubbish, waziri Lugola Lissu anashangaa pia katika hao eye witness alikuwepo house girl wake na house girl wa naibu speaker. Ambao hwajawahi kuhojiwa na polisi.

Mlishindwa kwenda kumhoji Nairobi alipopata fahamu?
Hata huko aliko panafikika kwa nin wasiende!!?
 
Hajafa sasa si aletwe ili uchunguzi ufanyike?
Mnamchunguza yeye au tukio? Hata kujua silaha iliyotumika na risasi za aina gani tu mmeshindwa?

Hata CCTV picture kama ya Surf kutoka Mozambique nayo mmeshindwa kupata?

Yule afisa mstaafu wa jeshi yeye aliwataja waliompiga risasi? Kwamba ni wanene, warefu, wembamba, wazungu, wanaongea kizulu...n.k?

MO aliyekwa mbona mlimtafuata kwa mbwembwe....alikuwepo kuwaambia waliomteka na kwamba yupo wapi? (Ofcourse kutekanatekana ndiyo michezo yenu mkishaishiwa punzi).

Hamna hoja, zilizopo hazina mantiki. Ni ujinga ujinga tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo hili tu, Serikali imeshindwa mengi. Hata polisi aliyempiga risasi Akwilina (RIP) alitambulika ila walishindwa kumtambua. Ikaishia kuwafungulia mashtaka viongozi wote wa CHADEMA.
Sasa TAL akiielezea dunia yaliyompata na kwamba serikali haioneshi nia ya dhati kutimiza wajibu wake, wao wanaendekeza propoganda za kiCCM zilizopitwa na wakati eti Lissu ametukana taifa, anapaka matope taifa! Amewaeleza vizuri kwamba serikali zinaweza kuja aina mbalimbali lakini taifa ni lile lile. Kinachoshindwa kutimiza wajibu si taifa la Tanzania (wananchi), bali serikali ya Tanzania (kikundi cha watu waliochaguliwa na wananchi kusimamia utekelezaji wa Katiba).
 
Kama Kweli kuna maaskari waliokuwa wakikaa getini, kama hii habari ni ya kweli, na hao maaskari hawajaguswa, hawajaulizwa kama siku hiyo waliona nini, maaskari hao wapo uraiani kama vile hakikutokea kitu, hapo kuna utata Mkubwa sana, hatuna sababu YA kuendelea na kesi hata kidogo.
 
hivi maraisi wastaafu wakisikia haya maneno wanajiona vipi?na wanaona hii nchi inaongozwa na watu wa aina gani?mbona wako kimya tu,na viongozi wa dini haya hawayasikii?kwa hali hii misikiti na makanisa watakuwa wanakwenda kusali wanafiki tu,
 
Kama polisi wameshindwa waruhusu upelelezi kutoka mashirika ua nje waone wasiojulikana wanajulikana mchana kweupe. Akiwemo suipuka, laama zinawaandama

Back
Top Bottom