Alwatan kamba
Member
- Nov 16, 2020
- 70
- 236
Ingawa ni jambo jema kwa serikali kutoa elimu bure ili kusaidia watoto watokao kaya maskini kupata elimu ya msingi lakini huu mpango unafaa kuangaliwa upya kwa sababu utekelezaji wake una hasara nyingi kuliko faida.
Hasara ya kwanza: Tangu kuanzishwa kwa sera ya elimu bure, serikali imeshindwa kuajiri walimu wa kutosha na hivyo kusababisha uhaba mkubwa wa walimu hususani wa masomo ya sayansi mashuleni na hivyo kupelekea wanafunzi wengi kufeli masomo hayo katika mitihani yao ya kidato cha nne.
Kadhalika, ukosefu wa walimu pia unachangia wanafunzi kukata tamaa ya kusoma baadhi ya masomo hasa ya sayansi na wengine huamua kuacha shule kabisa na kujichanganya mtaani. Hii yote ni kwasababu serikali inatumia gharama kubwa zaidi ya billions 20 kwa mwezi kuhudumia elimu bure na hivyo kupunguza kiwango cha bajeti cha kuajiri walimu wapya kwa mwaka.
Hasara ya pili: Kufuatia mpango wa elimu bure, upatikanaji wa vifaa muhimu vya kufundishia na kujifunzia kama vile vitabu, vifaa vya maabara na kemikali za kufanyia majaribio upatikanaji wake umekuwa sio wa kuridhisha na hivyo kufanya walimu pamoja na wanafunzi kujifunza katika mazingira magumu. Hii inaweza kuwa inachangiwa na ucheleweshaji wa kupeleka pesa za kuhudumia elimu bure katika baadhi ya halmashauri au bajeti kubwa kupelekwa kwenye ujenzi wa miundo mbinu ya shule na kusahau eneo muhimu la ununuzi wa vifaa vya kielimu.
Hasara ya tatu: Serikali inatumia gharama kubwa kulipia wanafunzi ada ambao saa nyingine huamua kuacha ama kufukuzwa shule na hivyo kufanya serikali kuingia katika gharama zisizokuwa na msingi.
Hasara ya nne: pamoja na serikali kutoa elimu bure bado kuna changamoto ya madawati na hivyo kupelekea wanafunzi kusoma katika mazingira duni ya kukaa chini hasa katika vipindi vya darasani.
Hasara ya tano: Tangu serikali ianze kutoa elimu bila malipo kumekuwepo na ufuatiliaji mdogo wa wazazi kuhusu maendeleo ya watoto wao(wanafunzi). Hali hii inachangia kushusha kiwango cha taaluma mashuleni kwakuwa ufuatilaji wa maendeleo ya wanafunzi kwa asilimia kubwa umekuwa ukifanywa na walimu pekee. Katika hili, wazazi wamejiweka kando kutokana na kwamba hakuna hasara yoyote wanayopata kwakuwa gharama zote zinalipwa na serikali.
Hasara ya sita: Elimu bure imechangia kudumaza ushiriki wa wazazi katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo. Mfano, ushiriki katika ujenzi wa shule, ushiriki katika upanuzi na ujenzi wa madarasa. Linapotokea suala la kuchangia shughuli kama hizo wazazi wamekuwa wagumu wa kuchangia huku wakidai ni elimu bure hivyo hatutakiwi kuchanga chochote.
Kufuatia hasara hizo na zingine ambazo hazijatajwa, napendekeza elimu bure ifutwe badala yake wazazi waendelee kulipa ada na serikali ifanye yafuatato:
1. Serikali itumie bajeti ya kutoa elimu bure kununua na kuhakikisha kuna vifaa vya kutosha vya kielimu mashuleni.
2. Serikali itumie bajeti ya kutoa elimu bure kuhakikisha kuwa kuna upatikanaji wa madawati ya kutosha mashuleni ili watoto wasiendelee kukaa chini.
3. Serikali itumie bajeti ya elimu bure kuajiri walimu wa kutosha mashuleni ili kuinua kiwango cha taaluma katika sekta ya elimu.
4. Utekelezaji wa elimu bila malipo uanze baada ya changamoto zote kwenye sekta ya elimu hususani mashuleni kufanyiwa kazi.
5. Hakuna haja ya elimu bure kwakuwa wazazi wanao uwezo wa kusomesha watoto wao lakini hawana uwezo wa kuwaajiri katika ujira wa kudumu. Hivyo ipo haja ya bajeti ya elimu bure kutumika kuangazia kutoa fursa za ajira kwa vijana.
6. Kama kuna umuhimu wa Sera ya elimu bure kuendelea kuwepo basi ihamishiwe katika ngazi ya elimu ya juu(vyuo vikuu) kwakuwa ndiko kwenye gharama kubwa kuliko huku chini ambako mzazi anaweza kupambana kwa biashara ya kuuza ubuyu, karanga au kilimo cha bustani na kumsomesha mwanae.