Serikali pigeni marufuku ujinga huu wa wachungaji feki

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,238
2,866
Naandika kufuatia tukio lililotokea mjini Moshi. Tunayo mifano ya haya yaliyotokea Moshi. Miaka ya 90 Alijitokeza Joseph Kibwetere aliyeteketeza roho za watu Uganda kwa makusudi. Ombi langu kwa serikali ni kupiga marufuku mikutano ya aina hii ambayo lengo lake ni kupotosha watu wenye udhaifu. Kwa nini tunaendelea kuruhusu watu hawa kupata umaarufu kupitia dini? Je kweli dini imejaa upuuzi na umaarufu wa kijinga kiasi hiki?

Tukubali kwamba mikutano na mahubiri nje ya nyumba za ibada lengo lake ni kupotosha watu. Iwe ni waislamu au wakristu, yote yamejaa upuuzi tu. Sehemu kubwa ya hawa wanaojiita mitume na manabii au masheikh wa mihadhara, wengi wakiwa hawakupitia mafunzo yoyote ni matapeli wa imani. Wengine sasa wanajidai eti ni semina zilizojaa mafunzo ya ngono na upuuzi wa kila aina. Mara Mgogo, mara mpuuzi fulani anafundisha kukata viuno.

Tunawachekea lakini tuendako sio pazuri kabisa! Ni watu wanaotafuta pesa kwa watu wenye matatizo. Tusiingie kwenye mtego wa kuwa ni watu tunaoamini kila tapeli awe na uwanja wake. Shughuli za kidini zibaki ndani ya nyumba za ibada, na huko wakifanya upuuzi kama huu watiwe kibano.
 
WACHUNGAJI NA HATA MASHEKH FEKI NAO WAANGALIWE, KUNA WENGINE WANAFANYA DUA HUKU KITAANI WANAWEKA KITUO KAMA KAMBI,
HAPO DADA ZETU WANAUMIA MNO.
 
Serikali=CCM ..
kura za Mazuzu ndiyo mtaji wao...
Gwajima
Kakobe
Rwakatare
Mzee wa upako
Mwamposa..nk
Hivi unaweza kumpata Mtu mwenye akili kutoka kwa hao wanaojiita Manabii !!!

Na wengi ndiyo wapiga kura wa CCM..
 
DC wa Ilala aliyakemea mkamtukana matusi ya nguoni Leo mnataka yadhibitiwe hakuna zuieni wenyewe huko Moshi sikujua Kama chagga washamba hivi
 
DC wa Ilala aliyakemea mkamtukana matusi ya nguoni Leo mnataka yadhibitiwe hakuna zuieni wenyewe huko Moshi sikujua Kama chagga washamba hivi
Huna sababu ya kutaja kabila. Hata kabila lako ni rahisi kuwapata wazembe laki moja watakaokwenda kumsikiliza mpuuzi huyu.
 
Back
Top Bottom