Serikali: Pato la kila Mtanzania laongezeka kwa Tsh. 100,000. Dar na Mwanza vinara msongamano wa watu

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Serikali ya Tanzania imesema pato la wastani la kila Mtanzania lilifikia Tsh. Milioni 2.4 mwishoni mwa mwaka jana kutoka Tsh. Milioni 2.3 mwaka 2017.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Juni 13, 2019 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati akiwasilisha Bungeni jijini Dodoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa katika mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/2020.

Dkt. Mpango amesema ongezeko hilo ni sawa na wastani wa asilimia 5.6. Kutokana na takwimu hizo, ongezeko hilo ni sawa na Tsh. 100,000 kwa kila Mtanzania

Dkt. Mpango amesema kiasi cha pato la wastani kwa kila mtu mwaka 2018 ni sawa na Dola 1,090 za Marekani ikilinganishwa na Dola 1,044 za Marekani mwaka 2017, sawa na ongezeko la asilimia 4.4.

=======

Dar es Salaam na Mwanza ni kati ya mikoa minne iliyotajwa kuwa na msongamano mkubwa zaidi wa watu kwa mwaka 2018 huku mikoa mingine inayofuatia kwa idadi kubwa ya watu ni Kagera na Kilimanjaro

Dar es Salaam ilikuwa na msongamano wa watu 3,695 kwa kila kilomita moja ya mraba ukifuatiwa na Mwanza iliyokuwa na watu 373.1, Kagera watu 119.6 na Kilimanjaro watu 104

Mkoa wa Lindi ametajwa kuwa na idadi ndogo zaidi ya watu kwa kilomita moja ya mraba ikiwa na wastani wa watu 14.9, ukifuatiwa na Katavi watu 16.1 na Ruvuma watu 24.8 kwa kila kilomita moja ya mraba
 
... depreciation ya sarafu imezingatiwa? Thamani ya TZS leo ni mbaya by far than 3 years ago. Uwezo wa mwananchi kununua ni mbaya kuliko siku zilizopita which means hali ya maisha imekuwa ngumu zaidi. Nadhani kuna factors nyingi za kuangalia in different dimensions badala ya kusema tu pato limeongezeka kwa TZS 100,000!
 
Serikali ya Tanzania imesema pato la wastani la kila Mtanzania lilifikia Tsh. Milioni 2.4 mwishoni mwa mwaka jana kutoka Tsh. Milioni 2.3 mwaka 2017.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Juni 13, 2019 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati akiwasilisha Bungeni jijini Dodoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa katika mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/2020.

Dkt. Mpango amesema ongezeko hilo ni sawa na wastani wa asilimia 5.6. Kutokana na takwimu hizo, ongezeko hilo ni sawa na Tsh. 100,000 kwa kila Mtanzania

Dkt. Mpango amesema kiasi cha pato la wastani kwa kila mtu mwaka 2018 ni sawa na Dola 1,090 za Marekani ikilinganishwa na Dola 1,044 za Marekani mwaka 2017, sawa na ongezeko la asilimia 4.4.

View attachment 1126338
Kumbe kwenye cabinet kuna vichaa wengi!
 
Haturuhusiwi kuhoji takwimu za serekali au hata kufanya utafiti kulinganisha ongezeko hilo la pato la taifa na hali halisi ya mwananchi. Kwa hiyo, tunapaswa kukubali, yaishe.
 
Back
Top Bottom