Serikali, Pambaneni na wezi wa Wizara ya maji kama ilivyofanyika ktk ujenzi

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
1,519
2,000
Serikali iliwahi agiza kazi za ushauri elekezi zifanywe na taasisi za serikali, lakini Wizara ya maji haifanyi hivyo. Ziara ya Mh. Rais ktk mikoa ya kusini imepambwa na malalmiko ya wananchi juu ya maji. Wizara ya maji ni imejaa wezi. Nasema tena Wezi. Kuna network kubwa tangu maafisa wa mabonde, maafisa wa mamlaka za maji na wakurugenzi, wizarani. Sijui huyo Katibu mkuu maana naye baada ya kuhama chama kiurahisi, msimamo wake hauaminiki.

Katika sekta ya ujenzi na hasa ujenzi wa nyumba, tatizo hili limepungua baada ya serikali kuipa nguvu taasisi ya serikali, TBA. Kwa upande wa barabara, bado hatuna nguvu maana MECCO ilikufa siku nyingi. Kwa upande wa maji tuige mfano wa TBA. Miradi ya upembuzi na ushauri mbali mbali ipelekwe kwenye taasisi za serikali ambazo zina uwezo mkubwa kuliko hao wanaopewa. Bahati mbaya pamoja na agizo la serikali, kazi hizo zinafanywa na taasisi za binafsi kwa lengo la ni kujinufaisha kwa 10%.

Pitieni miradi yote, Wizara iulizwe kwa nini iliwatumia watu binafsi na matokeo ni sifuri?
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
13,794

Ukina hivyo Katibu Mkuu ameshikwa kwenye kengele
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,155
2,000
Hii wizara kwa kweli! Dah! Huyo Mkumbo anafanya nini?
Hatuna uhaba na wataalamu wa maji. Hakuna anayejivuna eti ana utaalaaamu saaana! Wote ni usanii tu.

Pendekezo: Fukuza maafisa bonde wote ndani ya wizara hii. Bonde linaloongoza kwa wingi wa pesa ni Wami-Ruvu. hili hawataki mtu mwaminifu maana anawazibia masela wa Dar ulaji wao.

Fukuza wakurugenzi wa miji isipokuwa Tanga. Baadaye pambana na wasimamizi wa miradi pale wizarani. Wanapeleka pesa mikoani, halafu zinawarudia. Filisi wooote!
 
munkango

JF-Expert Member
Sep 12, 2016
336
500
Kazi za ushauri elekezi si tatizo katika miradi, tatizo ni kuwa Serikali hailipi madai ya Wakandarasi kwa wakati, kitu kinachokwamisha miradi mingi. Wanasiasa badala ya kukiri na kujirekebisha kwa kulipa kwa wakati wanawashushia lawama Washauri na Wakandarasi.

Hata kwenye majengo si kuwa TBA wanafanya kazi nzuri. Kazi nyingi wamezifanya kwa sifa za kisiasa na nyingi zimewashinda na mpaka nyingine wamenyanganywa.

Kinachotakiwa kufanyika Ni Serikali kuheshimu mikataba na kulipa kwa wakati
 
Mkuu, Maji ni tatizo la kudumu. Kuna wakati niliuliza hapa ni kwa nini kuchimba kisima cha serikali inagharimu milioni zaidi ya 100 wakati nyumbani unakichimba kwa milioni 10? Jibu ni wapigaji wa Wizara. Wakandarasi nao wamejipanga kuwaridhisha wapigaji hao. Ukiangalia mikataba ni ya ajabu tu! Mikataba mingi inayofanywa na wakandarasi wetu imejaa ujanja kwa imani kwamba wataelewana na wasimamizi wa miradi. Ndo hayo ya kufukia mabomba yanayobomoka kila kona au kisima kinachimbwa popote na kufunga kila kitu wakati hakina maji!

Upuuzi unatofautiana lakini Wizara ya maji upuuzi umezidi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom