frankshops
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 212
- 180
Nilitembelea ofisi za Elimu mkoa,nilikuta utitiri wa wazazi na watoto wengi wamejazana kilio chao kikiwa ni watoto wao kupangiwa chuo wakati vijana hawa walitamani kwenda kusoma kidato cha tano lengo ambalo pia nilikuwa nalo.
Cha ajabu ni kwamba jibu walilopewa kila mmoja ni nafasi hazitoshi,ushindani ni makubwa.Ukifuatilia wengi wa watoto hawa wanna division 2 na wengine division 1.na kutakiwa kuwapeleka private ambazo ada tu ni Kati ya 1500,000. hadi 4,500,000.wengi watabakia mtaani kwa Sababu jambo hili limekuwa la ghafla kwao,lakini pia uwezo mdogo.
Pia Mtoto wa miaka 17 anatoka kijijini,Kasulu unampangia Dar Chuo cha biashara jiji la maisha ya ghali, ambako hajawahi kufika,akaishi maisha ya kujitegemea ni kama kumsusia na kumnyima haki yake kielimu na kumpa mzigo mzito mzazi ambaye maisha yake ni ya chini.
Ongezeko la ufaulu ,Ongezeko la usajili kidato cha kwanza,na Ongezeko la shule za Kata, linatakiwa liendane na upanuzi wa shule za A-level.Mkakati uliofanywa na Rais kuhakikisha kuwa watoto waliofaulu darasa la saba wanaenda kidato cha 1,utumike pia kwa Kidato cha tano.Fungueni A- level kila kata watoto wetu w apate elimu wanayotaka kwani wanazo sifa wamefaulu.Shule zipo majengo yapo walimu wabobezi wapo,wataalamu wa Wizara zetu mnashindwa nini?Msaidieni Rais,msisubiri mpaka atoe tamko.
Unapomuacha mtaani kijana Ana div 2 point 20,Math C,Physics D,Biology B,Chemistry C,Geography C,History C,Civics C,Kiswahili C na English C ,eti kisa shule aliyochagua ilikuwa na ushindani kwenye combinatoon au hakubadili tahasusi baada ya matokeo ,ni uonevu mkubwa.msifikiri wazazi wote wana smartphone.
Na. kama mtoto huyu hataki kwenda chuo ,anataka kusoma kidato cha tano,na amefaulu kwa nini umlazimishe.Haki ya huyu mtoto kupata elimu anayoitaka iko wapi?.
KAMA vipi basi,toeni ruzuku shule binafsi ada ipungue hadi walau laki 4,watoto wetu wasome.Inaumiza kwa sababu sisi wengine tulipata elimu bure enzi zetu,
Naamini awamu hii ni sikivu sana,mtatusikiliza wazazi.Hiki ndo kilio likubwa mtaani kwa sasa.