Serikali oneni aibu sana kwa hili la wanafunzi wa vyuo!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali oneni aibu sana kwa hili la wanafunzi wa vyuo!!!!!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by BIG X, Nov 11, 2011.

 1. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sidhani hawa viongozi wetu wana watoto kwenye hivi vyuo, Yani wapo tayari kununua maelfu ya mabomu kuliko kuwapatia mahitaji hawa wanafunzi wa vyuo. Labda viongozi wetu hawana watoto, sababu hawajui uchungu wa watoto. Kuna maana gani ya kuwa na viongozi wazee kwenye serikali yetu halafu serikali inakosa busara kama uzee ni busara.

  Ukiangalia hizo picha hapo hao wanafunzi wamekaa wakijadili matatizo yao ambayo yanawaumiza na wayapeleke panapohusika. Mnapowawekea Askari na vifaa vya hatari nyuma manake ni nini, ni kuwatisha!!. Kama ni kuwatisha basi serikali ijue inakosea sana badala yake mnawajenga ujasiri hawa wanafunzi bila nyie kujua. Baada ya miaka mingi 20-30 taifa litakuwa na watu wenye hasira ambao hawataliheshimu Jeshi la polisi hata kidogo, mnajenga nchi ya watu wenye visasi wakati huo nyinyi viongozi hamtakuwepo, mtakua mmetuachia balaa watanzania. Ndio mnataka tuwakumbuke kwa hayo!!!.

  Ni wazazi gani nyie mnaoshindwa kuongea na vijana wenu, mkawasaidia na kuwatatulia shida zao. Mnafikiri mtaiweza nchi kwa kufanya vitisho!!!.

  Kama mnawatisha sana wanafunzi miaka nenda rudi na hakuna anayetishika, mambo yanajirudia vilevile. mmeshindwa kuelewa mnatengeneza nchi ya namna gani.

  Ni watoto wa masikini ndio wanateseka hivi!!!!.

  Mjue tu kila jambo huwa lina mwisho wake.


  DSC06409.JPG images23.jpg images24.jpg images25.jpg
   
 2. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,156
  Trophy Points: 280
  Hao watoto wakasome wanachochewa na wanasiasa uchwara kwa vichipsi kuku. Wanasiasa hao wanajulikana, lakini wahindi wanasema "deka jaega".
   
 4. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Inawezekana hujazaa wewe. Ndio mana hujui uchungu wa mwana. Ungekuwa na mtoto au ndugu kwenye hivyo vyuo usingeongea uo upuuzi. Nenda kashinde kule Cheat-Chat ndio kunakufaa.
   
 5. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kweli waone aibu!! wazee wazima kujali matumbo yao tu!! Loh!
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Serikali ina mkakati wa dhati wa kufanya hili taifa kuwa taifa la mambumbumbu, kwa nini watoto wanaodai elimu wanapigwa mabomu?

  Serikali inafikiria nini ???????

  Kweli serikali imeshindwa kuwasikia hawa watoto na kuwapa mikopo, hawaombi hela za bia, hawaombi hela za club wanataka elimu.

  Serikali yetu hii hivyo ina watu wenye akili kweli?????
   
 7. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,088
  Likes Received: 883
  Trophy Points: 280
  punguza kuvuta bange............. ndo madhara yake hayo!
   
 8. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,830
  Trophy Points: 280
  Kenge huwa hasikii mpaka umtandike hadi damu imtoke maskioni ndo ataskia.
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Nov 11, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ma.vi wewe
   
 10. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Juzi tu wanafunzi wa karatu sec. mliwafanyia hivihivi, hamna aibu nyie, leo UDSM hivyohivyo, na kesho mtaendelea hivyo hivyo. Hamuwezi soma alama za nyakati. Huyo JK ana raha gani kutalii kila siku huku wanafunzi nchini wanapata shida!!!.
   
 11. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Polen sana wana udsm,inahuzunisha sana vijana tunavyoteseka,huku tukiona mabilion yanaibiwa mchana kweupe
   
Loading...