Serikali ondoeni huu uchafu wa noti za sh 500

kerubi afunikaye

JF-Expert Member
May 20, 2013
1,183
1,057
Hizi noti sijui zimetengenezwa wapi!nimekaa nchi hii miaka mingi sijawahi kuona noti mbovu zinazowahi kuharibika kama hizi!zinaleta usumbufu sana kwenye transactions hasa huku kwetu tunaolipa nauli za daladala,chips yai,unga kilo moja,supu ya pweza,sadaka n.k kila siku kukunjana mashati tu!Niwataarifu tu enyi mliokalia viti vya kuzunguuka huko wizara ya fedha na BOT kuwa hizi noti zenu za sh 500 zimegeuka kero kubwa.Kwa kweli hii ni kashfa kwa vyombo vikubwa kama Benki kuu kutokuwa makini na kutengeneza vitu vya ajabu ajabu namna hii.hebu tafuteni mbadala wa noti hizi jamani,kulikoni?mbona enzi za Nyerere na Mwinyi tulikuwa na noti nzuri,walizitengenezea wapi zile noti zilizokuwa na signature za akina Msuya?Maji,umeme,barabara mtunyime,hata noti nazo?ina shida gani serikali hii jamani,jamani,jamaaanii..ah,ee Mungu,this country..!!
 
Utafiti usio na shaka umeonyesha bila ya wasiwasi wowote kwamba TANZANIA NDIYO NCHI PEKEE YENYE HELA MBOVU NA CHAFU kuliko nchi yoyote dunia !
 
Walisema zimetengenezwa kisasa kwa ubora wa hali ya juu!Hiyo ndio serikali ya ccm na hayo ndio maisha bora kwa kila mdanganyika!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Bila shaka MUSTAFA MKULO atakuwa anafahamu kisa cha kututengenezea hizo hela na manufaa aliyoyapata , siku ikifika tutamuuliza .
 
Walisema zimetengenezwa kisasa kwa ubora wa hali ya juu!Hiyo ndio serikali ya ccm na hayo ndio maisha bora kwa kila mdanganyika!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

uzuri ni kwamba wahusika wote wanafahamika ! Ni suala muda tu , watatajana tu .
 
Wakuu,inaonekana kuna kitu mnafahamu kuhusu huu uchafu.Dawa ni kufunguka ili watu wajue iko siku maneno yenu yatafanya kazi.Mie sijui kwa undani lakini nahisi tu,lazima kuna kitu hapa.Hizi noti ni very low quality,si bure!kwa jinsi nijuavyo mwenendo wa mambo ulivyo Tanzania,hapa nasikia harufu ya ufisadi kwa kweli!naungana nanyi!there is something!
 
Hizi noti sijui zimetengenezwa wapi!nimekaa nchi hii miaka mingi sijawahi kuona noti mbovu zinazowahi kuharibika kama hizi!zinaleta usumbufu sana kwenye transactions hasa huku kwetu tunaolipa nauli za daladala,chips yai,unga kilo moja,supu ya pweza,sadaka n.k kila siku kukunjana mashati tu!Niwataarifu tu enyi mliokalia viti vya kuzunguuka huko wizara ya fedha na BOT kuwa hizi noti zenu za sh 500 zimegeuka kero kubwa.Kwa kweli hii ni kashfa kwa vyombo vikubwa kama Benki kuu kutokuwa makini na kutengeneza vitu vya ajabu ajabu namna hii.hebu tafuteni mbadala wa noti hizi jamani,kulikoni?mbona enzi za Nyerere na Mwinyi tulikuwa na noti nzuri,walizitengenezea wapi zile noti zilizokuwa na signature za akina Msuya?Maji,umeme,barabara mtunyime,hata noti nazo?ina shida gani serikali hii jamani,jamani,jamaaanii..ah,ee Mungu,this country..!!

Kweli this country, this country, mkuu hata mi najiulizaga hivi haka kabiashara ka kushinda tunabadilisha fedha ni ka nani? Mbona za zamani ni bora kuliko za sasa,kwa nini zisibaki zile zile hivi why i say why? Nyie mlio juu hivi why? Naona mnataka tujilipue au sio haya subirini.
 
Back
Top Bottom