Queen Esther
JF-Expert Member
- Apr 5, 2012
- 2,205
- 1,461
GT's naamini kwa rehema za Mwenyezi Mungu mu wazima. Na wale wenye changamoto za maisha basi Mungu awape wepesi.
Tumeshuhudia Serikali ya awamu ya tano ikitekeleza mambo mazuri yaliyoanzwa na awamu zilizopita ikiwemo awamu ya nne. Moja wapo ni hii ya BOMOA BOMOA. Kwanza nawashukuru wote walioandaa hizo ripoti.
Hoja yangu inaanzia kwa kuiomba Serikali BOMOA BOMOA iendelee maeneo husika hasa yale hatarishi. Haya ni maeneo ambayo sio salama kwa ndg zetu na yenye kuathiri mazingira na viwanja vya wazi ni muhimu zoezi likaendelea maana likiachwa sasa halitafanyika MILELE!!! Pia sehemu kubwa ya watu walikuwa wamepanga huko Mabondeni kwani vyumba ni bei rahisi. Wafanyakazi wengi wa Serikali na wafanyabiashara ndio WAMILIKI wa hizo nyumba. Serikali ichunguze hili inawezekana inajifitini yenyewe kupitia hao wafanyakazi wenye hizo nyumba. Wanajidai WAMILIKI wanalalamika kumbe ni wao na wanawahonga hela kwenda hata mahakamani.
Kuna maeneo yanaweza kuangaliwa kwa jicho la tatu, haya ni Yale maeneo ambayo hayana direct impact kwa wanaoishi, jamii na mazingira pia. Mfano eneo la viwanda Mbezi nk
NATAMANI Leo Ma Great Thinkers tungeisaidia Serikali kwa kuishauri ni maeneo yepi tunaona yangeachwa yaendelee maana hayana madhara kwa JAMII, MAZINGIRA NA WAHUSIKA. Na sio kupinga tuu na kutaka zoezi lisimame!!!
Hali ya ukimya huu na zoezi kusimama sio mzuri hata kidogo. Halafu kuna watu wanaporomosha maneno mabaya kuwa Mhe Lukuvi na Serikali wameufyataa!!!!???? Hayo sio maneno mazuri hata kidogo.
Pia Mhe. Lukuvi alisema atatoa ramani za maeneo yetu tujue wapi ni open space nk ili tuanze kudhibitiana wenyewe kwenye Serikali za mitaa. Huku mitaa kuna watu wamejenga maeneo ya wazi wameziba mpaka barabara, watoto hawana pa kucheza nk.
Leteni hizo ramani tupate pa kuanzia. Mbona mnachelewa, muda muafaka ni sasa!!!
Mwisho narejea kwenye kichwa cha habari.
TUNAOMBA WAZIRI ANAYEHUSIKA NA MAZINGIRA AHAKIKISHE SABABU ILIYOSABABISHA NYUMBA KUBOMOLEWA INAKUWA WAZI. TUNAENDELEA KUONA VIFUSI VYA KUBOMOLEWA VIPO PALEPALE NA HUO NI UCHAFU NA VIJUMBA VIPYA VIKIANZA KUJENGWA, MAFURIKO YAKIJA HAO WATU WATAKUWA SALAMA??? HIVYO VIFUSI VITAONDOLEWA LINI NA KUSUDI LA HIYO ARDHI KUDHIHIRIKA MACHONI PETU ITAFANYIKA LINI??? "
A change is not a change unless the result changes".
KAMA NI MITI BASI TUONE MITI INAPANDWA, KAMA NI MTO UNAWEKEWA KINGO ZAKE VIZURI NA TUONE HILO LIKIFANYIKA, KAMA NI ENEO LA WAZI TUONE VIWANJA VYA WATOTO WETU VYA MICHEZO, KAMA NI ENEO LA WAZI KWA AJILI YA KUPUMZIKA TUONE MAUA YAKIPANDWA NK
NATAMANI KUONA UHAMASISHAJI WA KUPANDA MITI NA MAUA KTK JIJI LETU PENDWA LA DSM NA NCHI NZIMA. Sio tunakaa kumsubiri Mhe. Rais atoe maelekezo namna ya kutunza mazingira!!
Naliangalia hili nikikumbuka spirit ya usafi ilivyowekwa na Mhe Rais. Naona jiji limeanza tena kuwa chafu. Je tu nasubiri Rais aje tena????
Waziri wa Mazingira ni kijana na ni muelewe ukizingatia amekaa sana ughaibuni. Pia mama yetu Makamu wa Rais aliahidi wakati wa kampeni kushughulikia mazingira. Tunatamani tuone utekelezaji na TUNAOMBA uliweke vizuri jiji letu na TZ kwa ujumla.
Naomba kuwasilisha.