Serikali (NIDA) imefeli vibaya mno suala la vitambulisho vya taifa; kusubiri zaidi ya mwaka, vitambulisho vinapotea haviwafikii walengwa!

Mkuu kwa hapa nilipofikia nipo tayari kutoa rushwa! Nimekwama trip kama mbili za nje kwa sababu ya kutokuwa na passport mpya! Rushwa nitakayotoa wala haifikii perdiem moja!
Kwa hali hiyo hakuna namna zaidi ya kufanya hivyo mkuu Fanya wepesi tu
 
Mimi nimekamilisha taratibu zote mwezi wa nne mwaka huu nkaambiwa mpaka mwezi wa Saba mwaka huu kitakua tayari mpaka leo nimeishia kuwapigia simu kila wiki kuhakiki.....

jamaa mmoja muhusika ofisini kanambia Kama Nina haraka nacho niende na documents zinazotoa sababu ya uharaka huo ili nitengenezewe kiukweli pia nimekwama Sanaa nakihitaji mnooo tuambieni tutoe hiyo rushwa Kwa Nani ili at least tusipigwe Mana Sasa Imekua kerooo pale ofini washanikariri sasa.
 
Hii taasisi naona ni vijipu uchungu kabisa.
Watu wanahitaji kubadilisha hati za kusafiria ninyi toka 2016 watu wamejiandikisha hamjatoa na hamna mpango wa kutoa vitambulisho.
Huu sio ufanisi ni uzembe ulipitiliza lazima mjirekebishe dunia iko kasi sana mnachelewesha uchumi wa watanzania.
Sio kila mtu anatafutia Tanzania wengine hutafutia nje ya nchi.
 
Aisee nimefatilia pale makao makuu dodoma hadi nimechoka imebid nitulie tu mana hakuna namna
 
Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wamesema wamechoshwa na nenda rudi wanazoambiwa kwa nyakati tofauti na Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa (NIDA) wakati wa mchakato wa kupata vitambulisho....

Chanzo: MWANANCHI
 

Attachments

  • IMG_20181228_084232.jpg
    IMG_20181228_084232.jpg
    172.7 KB · Views: 38
Ukienda ofisi ya serikali ukaambiwa nenda urudi kesho
Jiongeze.........
 
Poleni sana...

Hao jamaa wanapenda sana kunyenyekewa, tena siyo kwa maneno matupu...

Anzieni kwenye serikali zenu za mitaa, inakua rahisi zaidi... mkianzia huko vikiwa tayari wanavipeleka huko...



Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom