Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,471
- 23,744
Kwa miezi mitatu mpaka mitatu na nusu wanafunzi wamekuwa nyumbani kutokana na janga la Corona.
Na sasa masomo yamekuwa resumed tunaamini yataendelea na mwishoni mwa mwezi wa 11 au katikati ya mwezi Dec kutakuwa na likizo mpaka Januari.
Shule ni Huduma. Tunalipia huduma ambayo ktk miezi hiyo mitatu mpaka mitatu na nusu hakukuwa na huduma hiyo. Je ada bado zitabaki zile zile za Milion 2 ,Mil 3 na Mil 4 kwa primary na baadhi ya sekondari?
Nadhani kuna haja ya Serikali kufanya mgawanyo ambao hautaumiza wazazi ktk suala hili.sababu kama wazazi watalipa ada ile ile ya mwaka mzima ni wazi watakuwa wanaumizwa na kuzifaidisha shule ambazo muda huo wote hazikuwa zikiingia gharama yoyote ila zimekuja kupata faida.
Ni kama gari ambayo ilikuwa imepark miezi yote hiyo then unapokuja kukodi tena unaambiwa ulipie na miezi ile ambayo gari lilipark ukiacha kuwa kuna siku mwenye gari alikuwa analiwasha kulipasha moto halafu anazima tena.
Wenye shule binafsi wamekuja kwa kasi na kuanza kuwasumbua wazazi wakitaka ada na kusahau kuwa hata wazazi wengi wameathirika kwa janga hili la Corona.
Maoni yangu ni kuwa ada igawanywe kwa miezi then ipigwe hesabu ya miezi ambayo wanafunzi hawakuwa shuleni itolewe then ilipwe kwa miezi iliyobaki.
Wazazi wengi wamekuwa wakilalamikia jambo hili la kudaiwa ada ya mwaka mzima wakati watoto hawajasoma mwaka mzima.na athari ya Corona imewapata wengi.
Najua jambo hili wamiliki wa shule na wanafunzi litawatoa povu sana. Tujadiliane kwa busara na akili.