Serikali ni Nini? Serikali inamilikiwa na nani? Uwepo wake ni kwa Faida ya nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ni Nini? Serikali inamilikiwa na nani? Uwepo wake ni kwa Faida ya nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Oct 14, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa wale waliopitia Mjadala wa leo uliondaliwa na Kigoda cha Mwalimu pale Nkrumah Hall kuna kitu ambacho kimejitokeza ambacho Prof. Shivji alitaka kujua na hatimae kilizaa jambo ambalo limesababisha kuuliza swali naomba kujua:

  Serikali Ni Nini? Serikali ni Nini? Serikali Inamilikiwa na Nani? Uwepo wake Ni Kwa Faida ya Nani?

  Waliopo madarakani uenda wakawa wako humo kwa tafsiri tofauti tofauti ni ndio sababu hatufiki na kila siku ni afadhali ya jana.

  Tafadhali wana JF naona nahitaji kujuzwa.
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mimi nafahamu serikali ni kwa faida ya wananchi na inamilikiwa na wananchi. Kuhusu serikali ni nini sifahamu!! Naona tu ni mkusanyiko wa watu wanaowatawala wenzao!! Political Sciencitist watujuze
   
 3. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  hakika tukipata mmdau atusaidie manake inavyoonekana siasa za kiafrika au dunia serikali zinatafsiri nyingi manake leo Mwanaporoganda Mkubwa wa CCM kasema Serikali ni kundi la watu wachache na si Umma na kuwa serikali inayomilikiwa na Umma haipo duniani.ndio maan tukipata watu wa political Science watusaidie.
   
 4. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Mkuu swali hili pia aliuliza marehem Othman ni kitabu chake ambacho na title yake hiko hivi A STATE OF TANZANIA, WHO CONTROLS IT AND WHOSE INTEREST DOES IT SERVE? Of coz I have a copy.

  Ukisoma hiki kitabu ambacho kina collections za Rodney na Shivji utapata mwanga mzuri kuhusu majibu ya swali lako.

  Ebu nijikite kwenye mada kwa kutumia uelewa wangu.Serikali ni watu wenye nguvu za kisheria na mamlaka yakuongoza jamii ambayo imewakubari watumie madaraka na nguvu walizopewa na wanajamii na sheria.

  Nani anayemiliki serikali? Serikali haimilikiwi na mtu yeyote kama mtu ila inaongoza na kuongozwa na watu kwa ujumla ni kwamba serikali hiko chini ya sheria na wanajamii.

  Serikali hipo kwa mjibu au interest ya nani?Serikali hipo kwa kutumikia na kuwaudumia wanajamii au watu walioipa mamlaka na nguvu za kuongoza in short government has to serve the interest of the people.

  Kumbuka mchango huu ni uelewa wangu kama mtanganyika and member wa JF.
   
 5. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mkuu mbona umesema unafahamu, halafu baadaye tena ukasema hufahamu?
   
 6. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Serikali na watuSheria ya 1984Na.15 ib.6​
  8​
  .-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuatamisingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikaliitapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwawananchi kwa mujibu wa Katiba hii;(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yaokwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.(2) Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar, au wa chochote kati ya vyombovyake na uendeshaji wa shughuli zake, utatekelezwa kwakuzingatia umoja wa Jamhuri ya Muungano na haja ya kukuza
  umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa.
   
 7. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hivyo ndio kusema Kingunge ambae ndie the last CCM Propaganda engineer and the constructor of our Political destiny via CMM is right?Kwa hiyo alivyosema Serikai ni Kikundi cha watu ni sahihi mbona wanazuoni wanasema Government is for the people hii imakaaje Mkuu?
   
 8. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo kinatharia [Theory] ni kweli Serikali ni Mamlaka ya watu lakini kwenye uhalisia [Reality] NI KWELI KUWA HAKUNA SERIKALI YA WATU BALI KUNA SERIKALI AMBAYO NI KIKUNDI CHA WATU WACHACHE TU. Ebu tathimini kupitia kwenye red,inaonyesha kuwa madaraka yanakuwa VESTED kwa Baadhi ya watu wachache [kikundi] ambao wanakuwa na mamlaka ambao ndio wanaogeuka kuwa SERIKALI YENYEWE.
   
 9. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  mkuu mbona jibu umepata tayari ila kuna maneno ya kiingereza ambayo yanachanya kama haya for,of and by kwahiyo kama wanazuoni wasema government is for the people inamaana ni kwa ajiri ya watu.Sasa kuna kitu muhim cha kujiuliza who are the people?
   
 10. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye nyekundu yaweza kuwa ndio maana halisi inapolala "who are the people" its that mean a small group of people whith their interest and not the majorities [Mass people] based on their interest.?
   
 11. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  faida yetu kwa maana halisi but uendeshaji wake ndio mh!
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu kulikuwa na maswali matatu.
  1. Serikali ni nini?
  2. Nani anaimiliki serikali
  3. Serikali ipo kwa maslahi ya nani?
  Nimejibu mawili. Moja la serikali ni nini nikasema sifahamu.
   
 13. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wananchi si serikali hila wao ndio watoa dhamana ya kuongozwa na watu kadhaa ( through political parties) kwa kuwapigia kura kutokana na sera zao (particularly za maendeleo ya jamii kwa ujumla) hili wapewe hiyo dhamana kuongoza taifa.

  Nchi zenye chaguzi za uraisi mshindi wa uraisi ndio mwendesha serikali, na serikali yenyewe haswa ni raisi na baraza la mawaziri ambao wao ndio watekelezaji wakuu wa sera za chama kilicho shinda. Bunge na Judiciary (including police) wao wapo kuhakikisha serikali inatekeleza au inafanya kazi zake kulingana na katiba na hawavuki mipaka yao.

  Hivyo maana halisi ya serikali ni raisi na baraza la mawaziri as they are supposed to be the orchestrators of anything under them to make sure their policies are implemented to the people.
   
 14. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Hii mada naona inazua maswali mengi sasa nataka tujurishane hapa hivi ingawa naweza kuwa tofauti GOVERNMENT is a entity of governing and it exist by social contract and mutual trust between the governed and the rulers.

  Sasa mkuu unaposema kuwa serikali ni raisi na mawaziri unakuwa unaleta majibu ya jumla kwani serikali hipo sehemu kubwa mfano organisations,civil societies etc then the rationale of government is governing.

  Kuna nchi ambazo the dnt have political parties and president but they have government mfano Lesetho and Swaziland then government siyo lazima iwe na political parties, president etc

  Katika karne ya leo uwezi sema kuwa serikali inatengezwa na organ tatu bali ni nne excutive,judiciary,legislature and civil society.Pili inabidi kujua kuwa siyo wanaochaguliwa tu ambao tunawaita matchtime ruler kuwa ndo serikali bali na hawa Bureacrats ndo permanent rulers of a Nation-State.
   
 15. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Unachanganya mambo kwa sababu the government has the responsibility of appointing most of the civil servant, adding on to that senior civil servant are just overseers of government policies and they have to abide by the regulators and policy makers, who have the authority to fire anyone going against their wishes if he/she is working for them.

  Huko Lethoso and Swaziland i dont know what the constitution says therefore i cant comment, as i dont know exactly the limitations of the royal rights. But if you want to argue on the basis of 'liberal democratic' societies; election are what forms the basis of the government which are supposed to works for the people, therefore those elected are responsible especially those on the executive branch.
   
 16. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ukijibu hilo swali bila kupingwa unapewe PhD... Kila mtu ana jibu lake, na hata jibu la Mwalimu lina tafsiri kadhaa...
   
 17. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Jana usiku saa 2 katika tarifa ya habari ITV, kulikuwa na matukio yafuatayo yameniacha mdomo wazi:-

  (1) Mbunge wa Same Mashariki Mh. Anne Kilango amekwenda katika msitu unaodaiwa kuwa umemalizwa na ukataji miti. Alikuwa anaongea na Wananchi wa eneo husika:

  KINACHONISHANGAZA:
  Mh. Kilango ameilaumu Serikali kwa kuachia watu kumaliza msitu na hivyo hatari ya kusababisha ukame. Ametishia kukwamisha bajeti ya Wizara ya Maliasili!!!!

  Pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Same naye pia ameilaumu Serikali kwa tukio lile.

  (2) Mkoa Mara Mbunge Nimrodi Mkono aliwatembelea wananchi walioathirika na mafuriko:

  KINACHONISHANGAZA:
  Mbunge nimrodi ameilaumu Serikali kwa nini inachelewa kupeleka msaada wa kuokoa maisha na mali za wananchi, ameahidi kwenda DSM kufuatilia kwa Viongozi wa Serikali kuhusu suala hili.

  HOJA YANGU:

  Mimi kwa upeo wangu mdogo najua kuwa Serikali ni chombo kilichopewa dhamana ya kuongoza wananchi. Viongozi wa Serikali ni wale waliiopewa dhamana ya kuongoza wananchi mf. Mabalozi nyumba kumi, Wabunge, madiwani, viongozi wa Halmashauri, wenyeviti vitongoji nk.

  Je, wadau labda mimi nakosea katika kufikiria kwangu maana ya Serikali na viongozi wa Serikali.

  Naomba ufafanuzi.


  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 18. Bob

  Bob JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2012
  Joined: Sep 10, 2007
  Messages: 277
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kilango - Anahofu ya operation "VUA GAMBA VAA GWANDA" iliyohamia Same ikitokea Arusha.
   
 19. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Anaamua kujisafisha ili aonekane yupo karibu na wananchi wake. Alikuwa wapi msitu ulipokatwa miti hadi leo umeisha ndio analaumu Serikali. na akiwa Mbunge alipaswa kuliona hili kabla na sio leo kukiwa hakuna msitu tena imebaki matawi ya miti tu.

  Sasa analaumu KIKWETE au yeye na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Same ndio wa kulaumiwa kwa usimamizi mbovu na kufumbia macho uharibifu huo?  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
Loading...