Serikali ndio ya kulalamikiwa, Mitandao ya simu inafidia gharama zinazoongezwa na Serikali kwa kupandisha bei vifurushi

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Nimekuwa nikiona sehemu nyingi watu wanalalamikia mitandao ya simu kuongeza bei za vifurushi, hii sio sawa, tunalalamikia 2 badala ya kulalamimikia chanzo cha 1+1.

Ni kama vile gharama za mafuta zikipanda basi nauli nazo zinapanda, si haki kuwalaumu wafanya biashara wenye mabasi.

Ndivyo ilivyo kwenye mitandao ya simu kuna gharama za vibali, kodi, leseni, tozo, n.k. hizo gharama kwao ni kama mafuta ya kuendeshea biashara zao, gharama zikipanda zinafidiwa kwenye vifurushi,

Nakumbuka hapo miezi michache tu iliyopita Zungu alitoa pendekezo kwa Nnape afanye utaratibu wa kuongeza bei kwenye vifurushi vya data kwasababu kuna watu wengi tunatumia internet, agizo limetekelezwa na sasa wananchi ndio tunabeba mzigo wa kilichoongezwa.

Ni kosa kuwalaumu mitandao, wao wanafidia gharama zinazoongezwa.
 
Back
Top Bottom