Serikali ndio inamtesa na kumuumiza spika bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ndio inamtesa na kumuumiza spika bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jul 19, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,967
  Likes Received: 37,520
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni na mtazamo wangu mwenendo wa serikali bungeni ndio kiini kikubwa cha kumfanya spika aumbuke kila mara.Udhaifu anaounyesha spika ambao nashindwa kuelewa kama kweli ni udhaifu wa kibinadamu au ni kwa malengo maalum ndio unatumiwa vibaya na serikali kama kinga yake kwa mambo ambayo serikali haitaki yajadiliwe au yasemwe bungeni
  Msingi wa maoni yangu ni kuwa hivi kuna siku hata moja spika amewahi kukataa kupokea muuongozo au hata taarifa pale waziri anapoomba kufanya hivyo hata ktk mazingira yasiyoridhisha kwa mfano hapa majuzi alipokatisha maoni ya kambi rasmi ya upinzani juu ya bajeti ya wizara ya mambo ya ndani.Hivi ingekuwa ni waziri anasoma bajeti alafu mbunge wa upinzani akasimama kuomba muuongozo au hata taarifa kweli spika huyu angemruhusu mbunge huyo?Kuna siku spika amewahi kumkatalia waziri pale anapotaka kuomba muongozo au kutoa taarifa?Je ni kweli serikali siku zote huwa sahihi ktk taarifa na muongozo?
  Tukio la jana trh 18/07/2012 ndio ambalo kwa kweli kwa maoni yangu limemuweka spika ktk hali ngumu kuendelea kuaminika kama kiongozi ndani ya bunge.Hivi ni kigezo gani alitumia kukataa muongozo wa mh.Hamad Rashidi na wakati huohuo kukubali muongozo kutoka serikalini kwa jambo lille lile ambalo awali alilipinga?
  Ushauri wangu kwa mh. Spika awe makini sana na hoja za upande wa serikali na ajue siku zote bunge lina kazi ya kuisimamia na kuishauri serikali.
  Madam speaker, ukiendelea kufanya kinyume cha haya ni doa kwa wanawake wenzako kupata nafasi kama hizo siku zijazo na wewe binafsi utaingia ktk historia ambayo si nzuri hata kwa vizazi vijavyo.
  Mwisho mama yangu kumbuka kiapo chako na hata dua kabla ya kuanza shughuli za bunge.
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jamani tusisahau kuwa kile kiti alipewa kama zawadi, sio kwamba alikuwa na uwezo:
  hivi vyote hivi vinavyojitokeza ni mlolongo tu wa uwezo wake mdogo, na harakati za kuendelea kulinda hako ka zawadi kasimponyoke. Uwezo wa kuongoza Bunge la Tanzania kwa ujumla hana, basi tu...
  sanasana bunge analoweza kuliongoza ni Bunge la ccm, ambayo ni rahisi kuliongoza kwa mtu yoyote...kwani ni usingizi kwa saaaaana... wakizinduka ndiyoooooooooooooo... kuunga hoja asilimia 100, hata kama hawajui mjadala unahusu nini....
   
Loading...