Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Serikali imewatoa hofu wananchi wake kuwa nchi iko Salama na itaendelea kuwa salama.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Hamad Yusuf Masauni, akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu Tauhida Nyimbo (CCM) aliyetaka kauli ya Serikali kutokana na kuwapo kwa taarifa za vitisho zinazotolewa kwenye Mitandao wakati huu wa maandalizi ya sikukuu ya eid el-fitr.
Waziri Masauni alisema pamoja na kuwapo kwa vitendo vya kiuharifu vinavyotokea, nchi bado iko Salama na itaendelea kuwa salama kutokana na serikali kuhakikisha inadhibiti uharifu huo.
Pia Serikali imesema mikutano ya kisiasa itaendelea kuzuiwa hadi pale polisi watakapoona inafaa kufanyika.