Serikali na Zitto lao uenda likawa moja linapokuja sakata la KIWIRA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali na Zitto lao uenda likawa moja linapokuja sakata la KIWIRA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Byendangwero, Mar 12, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kama kuna wizara imeifilisi nchi hii wizara hiyo ni ya Nishati na Madini. Kila kitu katika wizara hiyo kinaonekana kufanyika shagala bagala; chukua huu mgodi wa KIWIRA, baada ya uamuzi wa kuurejesha serikalini kufikiwa, ilitegemewa kwamba hatua za haraka zingelichukuliwa kuhakiki rasilimali na madeni ya mgodi huo ili zoezi la makabidhiano rasmi liweze kufanyika. Mpaka sasa yapata zaidi ya miaka miwili hakuna kilichofanyika. Wakati huo huo, kuna habari kwamba Tanpower Supplies kwa kupitia mgongo wa mgodi huo ilichota mabilioni ya fedha kutoka serikalini na katika vyombo vya fedha na kuziweka kusikojulikana. Habari hizo zinazidi kutonya kwamba hivi sasa, kunafanyika njama ya kuhamishia madeni hayo serikalini, na kwamba Zitto ni mshiri katika njama hizo, ndiyo maana hadiriki kuzizungumzia.
   
Loading...