Serikali na Wizara ya Afya ninaomba "FUKIZA KILA KAYA", kampeni maalumu ya kutokomeza magonjwa ya milipuko

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,402
2,000
Tunaona nchi mbalimbali zikizalisha chanjo za magonjwa ya Corona na kuwagawia wananchi wake na kuuza kwa mataifa mengine.

Sisi nasi tumezalisha Tiba za magonjwa kama hayo na tunaona kwenye mitandao ya kijamii waliozitumia wakizisifu. Ni kwa bahati mbaya sana dawa hizi zinapatikana kwa shida sana maeneo mengi. Kwenye maduka ya madawa hazipatikani.

Tunaweza kuwa tumezalisha dawa inayotibu na ambayo tungeipeleka mpaka kimataifa lakini shida hatufanyi promosheni ya kutosha.

Promosheni ya kwanza ni kugawa kwa watu wetu watumie na jumuiya ya kimataifa tuwaonyeshe matokeo.

Lakini pia kwa kugawa kwa watu wetu tunakuwa tunajali watu wetu.

Tuzindue kampeni ya kaya "FUKIZA KILA KAYA" kwa kugawa dama moja kila kaya na kuwaelekeza matumizi sahihi hasa pale kunapotokea uhitaji.

Na pili ni kufanya dawa hizi zipatikane kila kona ya nchi hii ili mwenye kuhitaji baada ya kutumia moja ya bure akanunue.
 

Earthmover

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
16,870
2,000
Kwa hisani ya Watu Wajinga kaombeni VENTILETA hospitali zimezidiwa..hayo matogwa kunyweni wenyewe...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom