Jaslaws
JF-Expert Member
- May 31, 2011
- 6,016
- 5,284
Heshima kwenu,
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada. Kama mwananchi kuna jambo limekuwa likiniumiza sana. Serikali walitenga baadhi ya hoteli kwa ajili ya watu wanaotoka nje kukaa huku wakichunguzwa ugonjwa wa Corona, moja wapo wa hoteli zilizotengwa ni FQ village iko Ukonga Stakishari.
Sasa kilichonifanya kuandika hapa ni kutokuwa na uaminifu kwa askari wanaolinda hizo hotel, wamekuwa wakiwaruhusu hawa watu kutoka na kuingia mtaani, kwa mfano juzi walikuwa bar jirani na hiyo hotel inaitwa Kiliman bar wanakula pombe tena katikati ya watu bila kujitenga. Jana pia nimepita maeneo hayo wanasema hata supu wanakunywa kila asubuhi.
Nawaza kwa bahati mbaya kuna mtu anao huo ugonjwa na ile sharing ya bar tutakufa kama kuku
Naomba Serikali wafuatilie kisha wachukue hatua kabla ya dhahama.