Serikali na TRA, mnaweza kuwezesha utoaji wa risiti za VAT kwa njia ya mobile SMS. I stand to be corrected

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari za wakati huu ndugu zangu wa hapa JF.

Juzi nilienda kununua bidhaa ya gharama kidogo kama shillings laki tatu na nusu kwenye duka moja pale kariakoo. Nilipewa bidhaa yangu, nikaikagua vizuri na kuhakikisa ipo sawa na hakuna dosari yoyote kisha nikafanya malipo ya pesa stahiki hiyo 350,000/=

Baada ya malipo hayo nikadai receipts ya mashine (EFD) wakadai kuwa kwa sasa hawawezi kutoa kwa maana mashine ni mbovu. Kwa kweli nilisikitika sana kwa maana ofisi ninayofanyia kazi haikubali receipts ya kuandikwa kwa mkono kwa maana wanaogopa auditors wa TRA.

Proposed Solution: Serikali kupitia TRA wanaweza kuwezesha utoaji wa risiti kupitia mobile sms, pale ambapo mfanyabiashara anadai kuwa machine haifanyi kazi, aka mbovu, ama network inasumbua.

Mfano baadha ya mimi kulipia laki tatu na nusu, muuzaji anaweza kupiga number *150*kiasi alichopokea*number ya mnunuzi*PIN# kisha anapiga.

Kama kwa TANESCO imeweza kwenye LUKU kwa nini TRA washindwe katika VAT, pale ambapo wafanya biashara wanasingizia eti mashine ni mbovu ama network inasumbua.

Najua kuna some technical procedures and protocols to be followed, ila hili linawezekana saaana tena saaanaa.

Naomba tujadili hili kwa kina na sio kutukanana wala kukejeliana.

Ninawasilisha hoja.

Thanks.
 
Nafikiri itawezekana, lakini wafanya biashara watakuwa tayari kununua machine nyingine laki tisa yenye hiyo option?
 
Kwa E-mail ndio bora zaidi na kumbukumbu inakaa poa kizaidiiiiii.
Hili la hivi ilibidi walifikirie hata kabla ya hizo mashine zao hazijaagizwa.. labda lipo.. kama halipo basi hao watakuwa watu wa karne zilizopita ndio walisukuma hizo oda.
 
maelezo yapo too technical yamekaa kiufundi sana wewe huwezi kuelewa mdogo wangu

hahahahahaha kama kifaa cha TRA kimekosa Net au ni kibovu likewise its possible kwa simu ya mkononi pia kuwa mbovu au kukosa Net. Maana zote zinatumia line hizo hizo za simu! Technically possible but doing the same solution for the same problem seen as different solution. Think outside the BOX!
 
I wish ningekuwa mkuu wa mkoa, mapato mengi sana yanapotea kihirera ningewanyoosha zaidi ya mzee mwenyewe. Sheli wamuzua kamtindo kuwa mashine iliyofungwa EFD mashine ni moja hivyo hawaitumii wanatumia ya pembeni ambyo bado haijafungwa, ukiuliza unaambiwa ni mbovu, Pumbavu sana. maduka hali kadhalika, mtu anaenda kariakoo dar ananunua mzigo, anasfirisha kwenda mkoani kwa fuso, anachukua risisti anaenda mkoani anashusha mzigo, kisha anarudi dar kufunga mzigo anatumia risiti ileile ya mara ya kwanza kwa kigezo cha kuwa gari iliharibika hivyo hakufikisha mzigo sehumu husika alikwama njiani.
I WISH NINGEKUWA MKUU WA MKOA AMA WA WILAYA TU NIWANYOOSHE
TRA wamelala usingizi kabisa wapo maofisini tu, kuweni kama maafisa mikopo mzurure mitaani. kwa leo naishia hapa NYAMBAFU SANA
 
Inawezekana,mimi nimenunua kitu kwenye maduka ya "Best buy"nchini marekani na receipt sikuprintiwa nilitumiwa kwenye simu yangu.So inawezekana ni maamuzi tu .Kwani wenzetu wanakuuliza ukitaka printed ou utumiwe via email or mobile.Na inasaidia kupunguza utumiaji wa karatasi
 
Afu hizo return unaandaaje?
Return in rahisi kwani ikishapanch ile receipt tayari TRA has all infomation so whether una print au la tayari iko recorded kwa system.Emarging tunanunuaga vitu online i.e Amazon na unaletewa kila kitu chako pamoja na receipt yako kwanza hiyo ndio njia rahisi ya ku control mapato kwani you can verify transaction as someone has received receipt through mobile number.Kwani Receipt ya MPESA and mobile money unapataje !
 
Back
Top Bottom