Serikali na TAKUKURU muimulike Hospitali ya Mkapa Dodoma

Fulema Nangwa

Member
Jul 27, 2017
79
46
Hospitali ya Mkapa Dodoma Rushwa imekuwa kawaida kabisa mgonjwa hawezi kupata huduma yaaina yoyote bila ya kutoa chochote. Tumempeleka mgonjwa sasa ana wiki matokeo ya vipimo hayajatoka na bado mgonjwa hajapewa huduma yoyote zaidi ya kupewa dawa za kuondoa maumivu.

Daktari anapita analeta maneno ukiuliza unaambiwa subiri utatibiwa , hivi kweli na mgonjwa umelipia huduma na kitanda ,wegonjwa ambao wapo hapo hospitali wanasema kuwa bila chochote hupati huduma hata kama umelipia maabara ili upewe majibu lazima utoe chochote. Nadhani wanafanya hivi kwa kuwa hospitali ipo nje ya mji .
 
Nimeiona taarifa. Naomba uwasiliane nami kwa maelezo zaidi tuweze kuchukua hatua. Asante
 
Ni kwa wangonjwa wote au wale wenye mlengo wa CDM? Kuwa specific ili hatua zichukuliwe mara moja
 
Nimeiona taarifa. Naomba uwasiliane nami kwa maelezo zai
Nimeiona taarifa. Naomba uwasiliane nami kwa maelezo zaidi tuweze kuchukua hatua. Asante

Hiyo ni "clue" inatosha kuanzisha investigation process. Taarifa gani zaidi unahitaji. General hospital Dodoma wanajitahidi sana kutoa huduma nzuri. Hao jamaa wa mkapa hospital ni jina tu. Serikali isogeze macho yake pale. Itaona ukweli wa malalamiko ya mama huyo na mengine. Watu bado wanafanya kazi kwa mazoea.
 
Nimependa thw prompt response from Dr. Ndugulile naibu waziri wa afya. plz mtupe feedback/mrejesho!
 
Hakuna hospitali ya serikali ngazi ya wilaya hadi rufaa isiyo na tuhuma za rushwa kwa watumishi wake.
 
Hospitali ya Mkapa Dodoma Rushwa imekuwa kawaida kabisa mgonjwa hawezi kupata huduma yaaina yoyote bila ya kutoa chochote. Tumempeleka mgonjwa sasa ana wiki matokeo ya vipimo hayajatoka na bado mgonjwa hajapewa huduma yoyote zaidi ya kupewa dawa za kuondoa maumivu.

Daktari anapita analeta maneno ukiuliza unaambiwa subiri utatibiwa , hivi kweli na mgonjwa umelipia huduma na kitanda ,wegonjwa ambao wapo hapo hospitali wanasema kuwa bila chochote hupati huduma hata kama umelipia maabara ili upewe majibu lazima utoe chochote. Nadhani wanafanya hivi kwa kuwa hospitali ipo nje ya mji .
Dawa ni kuwaripoti TAKUKURU tena taja na jina la muhusika lakini kulalamika haisaidii kitu......
 
Kashitaki pengine tu ndugu yangu wala sio TAKUKURU maana watakachokifanya ni kuwapandisha vyeo hao watuhumiwa wote ili kukukomesha.
 
takukuru ipi ya afande mlowo?

ndungu kama mwanaume akete mrejesho jukwaani.

toeni tu hata 10,000 kama ya kufulia koti
 
Ulipowataja tu TAKUKURU nikaahirisha kuusoma Uzi wako. Unamaanisha ile taasisi yenye double standards katika kushughulikia watuhumiwa wa rushwa au ni nyingine nisije kuwa nime mix madesa.
Hebu nikumbushe nimesahau walimwambiaje Nassari kuwa wanachunguza kama mtuhumiwa anakesi ya rushwa au just wrongdoing!!!
 
Nimeiona taarifa. Naomba uwasiliane nami kwa maelezo zaidi tuweze kuchukua hatua. Asante
Ubarikiwe Sana Mh. kwa mwitiko wako wa haraka.
Lakini nikuombe tu Mh. kwa taarifa ya ndugu yetu huyu iwe mwanzo tu wa kulitafutia ufumbuzi wa kudumu tatizo hili katika Hospitali za serikali kwa sababu lipo kwa kiwango kikubwa sana.
Unapokuwa na mgonjwa hasa wa operesheni katika hospitali za serikali unaambiwa gharama, na ukisharipa gharama zote unaambiwa nafas yako ya kufanyiwa itakuwa miezi mitatu mbele au fanya hivi (utoe pesa binafsi kwa daktar atakayekufanyia operesheni) ili upate nafasi.

Kuna baadhi ya madaktari ukishalipia gharama za opereshini katika hospitali za serikali wanakuambia hapa nafas zimejaa, kama unatakakufanyiwa huduma haraka unatakiwa umlipe daktari uliyepangiwe pesa ya ziada na baada ya hapo anakuhamishia katika hospitari binafisi na huko unapata huduma.
Mh. naomba katika ziara zako katika hospitari za serikali hepu lifanyie uchunguzi suala hili ili kuwapunguzia usumbufu wananchi.
 
HII IPO HOSPITALI KARIBU ZOTE, HASA UKIWA NA TATZO KUBWA LA KIAFYA MFN. KAMA UNATAKA KUFANYIWA UPASUAJ, LAZIMA UMPOOZE SURGEON AKUFANYIE
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom