Serikali na taasisi zake zimekuwa zikiweka kikomo cha umri wa miaka 45 kama moja ya vigezo vya mtu kuajiriwa ktk utumishi wa uma.Kisingizio ikiwa ni takwa la mifuko ya kijamii juu ya pension. Kigezo hiki ni cha kibaguzi, hakina msingi wowote ule,kimepitwa na wakati.Na kimekuwa kikiweka nguvukazi kubwa nje ya mfumo wa utumishi wa uma.It is a very unreasonable requirement. Kigezo chenye mantiki juu ya umri ni chini ya miaka 55.Hii itasaidia nchi kuitumia nguvu kazi kubwa ya watalaam wetu mbalimbali. Leo mtu hata akiwa na miaka 50 bado ana nguvu na apate haki ya kuajiriwa katka utumishi wa uma. Kigezo cha ukomo wa umri wa miaka 45 hakimo kwenye sheria za utumishi wa umma(Public Service Laws).