Serikali na marufuku ya biashara ya Viroba

Wazabanga kuku

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
264
378
a8175d4bfb70a0f2d671395937059b4e.jpg

Serikali inatakiwa itazame upya marufuku yake dhiki ya biashara ya Pombe inayofungashwa kwenye mifuko ya nylon almaarufu Viroba, naamini viroba sio hatari kama serikali inavyopiga propaganda zake ,biashara ya Pombe ndio inaingizia nchi pesa nyingi Leo hii kuipiga marufuku eti kisa wanafunzi wanabeba class si haki inapaswa walimu na wazazi ndo waadhibiwe juu ya watoto/wanafunzi wao kutumia hii Pombe wakiwa shule pia hii Pombe ilikuwepo katika tawala za awamu zote 4 iweje awamu hii ipige marufuku kama uchumi umeharibiwa na uongozi wasisingizie vijana ndo wanaharibu kisa tu wanakunywa konyagi ya jero ,serikali ijitathimini imeteleza wapi ila hizi marufuku zingine ni ngumu kutekeleza kwa nchi hii yenye watu zaidi ya M50 wa vijijini na mjini ,Viroba ni biashara nzuri sana kuikataza ni kupoteza mapato na kuhusu vijana kuathirika kiafya sikubaliani kabisa kwa viroba vinavyozalishwa Tz ni salama kabisa havina scandal chafu kama vya kutoka burundi,Uganda Zambia au Malawi ,hivi vya nje ya nchi ndo vipigwe marufuku ila vya ndani viachwe
 
Serikali hii ya mwendokasi .....ila in the mean time tuhamieni kwenye balimi!

Ova
 
a8175d4bfb70a0f2d671395937059b4e.jpg

Serikali inatakiwa itazame upya marufuku yake dhiki ya biashara ya Pombe inayofungashwa kwenye mifuko ya nylon almaarufu Viroba, naamini viroba sio hatari kama serikali inavyopiga propaganda zake ,biashara ya Pombe ndio inaingizia nchi pesa nyingi Leo hii kuipiga marufuku eti kisa wanafunzi wanabeba class si haki inapaswa walimu na wazazi ndo waadhibiwe juu ya watoto/wanafunzi wao kutumia hii Pombe wakiwa shule.
Kwani mwalimu ama mzazi anashinda na mwanafunzi muda wote?, unauhakika kama mwanafunzi hawakaguliwi labda kuwa wepesi wa kuificha anaweza kuhadaa mwalimu na mzazi.
 
Ngoja siku ukute mwanao wa shule ya msingi anagonga kiroba ndio utatia akili. Pombe sh mia tano hata mtoto wangu wa miaka mitano anauwezo wa kununua. Viroba viende tu hatuvitaki. Awamu hii full adabu...no viroba, no unga, no ushoga, no kata K...nasubiri vimini vipigwe marufuku.
 
Maamuzi mengi ya nchi hi yanafanywa na viongozi wa kisiasa bila kuwahusisha wataalamu, wadau wala utafiti. Serikali ingewahusisha wadau wachini ingepata mwanga jinsi watoto wanavyopata viroba. Ni uzembe wa usimamiaji uuzaji. Vinauzwa kwenye maduka na viosk, watendaji wa serikali wanaangalia. Bar watoto wanafukuzwa, kwani wamiliki wanaelezwa sheria ya vileo wakipewa leseni.
 
Back
Top Bottom