Bangusilo
Senior Member
- Feb 7, 2008
- 137
- 10
Na Ramadhan Semtawa, Dodoma
UFISADI umezidi kuitikisa nchi baada ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kubaini mtandao mkubwa ambao umesababisha malipo hewa ya Sh3.4 bilioni kwa walimu wa shule za sekondari nchini.
Kubainika kwa ufisadi huo kumekuja miezi michache baada ya gazeti hili kuandika sakata la Mhasibu Paul C Mhumba, ambaye alifukuzwa kazi mwaka 2006 kwa idhini ya Rais Jakaya Kikwete, baada ya kushirikiana na Idara ya Usalama wa Taifa kuibua tuhuma za malipo hewa ya zaidi ya Sh3bilioni kwa walimu wasiokuwemo kwenye ajira.
Hata hivyo, Rais Kikwete alipotoshwa na vigogo wa Wizara ya Elimu siku chache baada ya kuingilia madarakani ili aidhinishe kufukuzwa mhasibu huyo aliyekuwa Ifunda, bila sababu za msingi.
Lakini jana, Waziri Hawa Ghasia alitoa taarifa mjini hapa inyaoonyesha kuwa fedha hizo zililipwa katika kipindi cha kati ya mwaka 2001 hadi Desemba 2007, ambacho pia Mhumba aliwahi kukieleza.
Waziri Ghasia alifafanua kwamba uchunguzi uliofanywa na Ofisi yake katika kipindi cha Machi 2007 hadi Desemba, umebaini upo mtandao mkubwa kuanzia Makao Makuu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Ofisi hiyo ya Utumishi.
Akizungumzia jinsi ufisadi huo ulivyofanyika, Ghasia alisema katika uchunguzi huo imebainika fedha hizo zililipwa kwa watumishi hewa 1,413, huku baadhi yao wakiwa na namba za hundi zaidi hivyo mtu moja kuwa na mishahara miwili.
Serikali kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, imefanya uhakiki wa rasilimali watu katika shule za Sekondari nchini chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kugundua kuwepo kwa watumishi hewa 1,413, alisema waziri Ghasia na kuongeza:
Taarifa ya uhakiki huo zinaonyesha kuwa jumla ya Sh3.4 bilioni, zililipwa kama malipo hewa kwa watumishi hao, zoezi hili lilifanyika Machi hadi Desemba 2007.
Alifafahamisha kwamba ukaguzi huo pia ulibaini kuwa baadhi ya watumishi wanaolipwa mishahara hawako kazini, wamekufa na wengine wanafanyakazi katika taasisi nyingine.
Waziri Ghasia akionyesha ni jinsi gain ufisadi bado unaitikisa nchi, alitoa mfano katika shule moja mjini Moshi ambako kuna mwalimu mwenye hundi ya malipo ambaye alikuwa na cheo cha Afisa Elimu Msaidizi daraja la Kwanza, lakini hajawahi kuhudhuria mafunzo ya ualimu.
Kwa mshangao, Ghasia alisema mtu asiye na sifa alikuwa akipandishwa vyeo muda wote kana kwamba amepewa mafunzo ya ualimu, na kuhoji vipi alipelekwa kufundisha shule hiyo ambayo hata hivyo, alikata kuitaja, bila kuwa na sifa.
Alifafanua kwamba, katika zoezi hilo shule za sekondari 2,861 ambazo wakati wa uchunguzi huo zilikuwa na walimu 26,953 zilikuja kubainika walimu 1,413 walikuwa hewa ambao walilipwa mishahara benki iliyofikia kiasi hicho cha Sh3.4 bilioni.
Ghasia aliongeza kwamba, fedha hizo hazijumuishi walimu wanaodaiwa kwenda mafunzoni bila kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazohusu mafunzo kwa watumishi wa umma.
Alifafanua kwamba, katika ukaguzi huo uliofanywa kutekeleza Sheria Namba 8 ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002, ambayo kipaumbele kilikuwa ni mahudhurio kazini, uzingatiaji kanuni za Sheria ya Ajira, Mahitaji ya Watumishi na Ukaguzi wa Malipo ya Mishahara, ilibainika baadhi ya walimu wanafundisha chini ya kiwango kwa asilimia 50.
Mikoa vinara kuwa na watumishi hewa na idadi yao katika mabano, ni Dar es Salaam (21), Morogoro (149), Mwanza (132), Iringa (119), Mbeya (101), Rukwa ( 95), Arusha (72), Dodoma (57), Shinyanga (52) na Singida (50).
Mingine ni Lindi (4), Tanga (4), Mtwara (41), Pwani (40), Kagera (35), Manyara (35), Tabora (33), Kilimanjaro (27), Ruvuma (27) Mara (19) na Kigoma wa mwisho (15).
Hatua zilizochukuliwa, waziri Ghasia alifafanua kwamba uamuzi wa kwanza ni kuwaondoa walimu hao hewa katika mfumo wa malipo ( Payroll), ambao Ofisi hiyo ilichukua hatua hiyo kwa walimu hao 1,413 katika malipo ya utumishi wa umma hadi ilipofika Desemba mwaka 2007.
Alisema hatua ya pili, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imechukua hatua ya kuwaondoa kwenye orodha ya malipo ya mishahara ya watumishi 1,853 waliobanika kutokuwapo kazini bila ridhaa ya mwajiri.
Hivyo kufanya idadi ya watumishi waliondolewa kwenye orodha ya malipo kufikia 3,266 hadi ilipofika Machi, mwaka huu, huku hatua inayoendelea sasa ikiwa ni kuchunguza mtandao huo kwa undani ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani, alisisitiza.
Alisema mchakato unaofanyika sasa ni kubaini fedha hizo zimeingia katika mikono ya nani.
Ufisadi katika Wizara ya Elimu ni moja ya kasfha kubwa, ambazo zimeubuliwa na serikali ya awamu ya nne ikiwa imeanzi miaka ya nyuma.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi