Serikali na madaktari wachukue hatua za haraka kuokoa maisha ya Wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali na madaktari wachukue hatua za haraka kuokoa maisha ya Wananchi

Discussion in 'JF Doctor' started by EU-ME, Jan 26, 2012.

 1. E

  EU-ME New Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii inatakiwa kuchukua hatua za haraka kumaliza mgogoro baina yao na madaktari ili kuepusha madhara makubwa katika upatikanaji wa huduma za afya nchini. Ijulikane kuwa, jukumu la awali la wizara kwa kushirikiana na madaktari ni kuboresha afya za wananchi na kuokoa maisha yao, hivyo ni wajibu wao kufanya kazi kwa pamoja ili kufanikisha hili.
  Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuwepo kwa mgomo wa madaktari katika vituo vya huduma za afya vya umma kufuatia kushindwa kwa Wizara ya Afya kukutana na Chama cha Madaktari ili kujadili madai mbalimbali yanayokwamisha kutoa huduma bora za afya kama inavyostahili.

  Mgomo huu baridi wa madaktari unasababisha athari kubwa kwa wananchi katika upatikanaji wa huduma za afya. Sikika inaamini kuwa Wizara ya Afya ilikuwa muda wa kutosha na uwezo wa kutatua tatizo hili mapema ili kukwepa adha wanayoipata wananchi sasa.
  Waziri Mkuu naye alikuwa na muda wa kutosha kulishughulikia tatizo hili lakini hakulipa umuhimu unaostahili. Tumefurahishwa na kauli ya Waziri Mkuu leo kwamba anawaonea huruma wagonjwa na kwamba jambo hili linazungumzika. Lakini tunajiuliza alikokuwa hadi hali ikafika hatua hii. Tunaamini kwamba Waziri Mkuu alikuwa na mamlaka ya kuzuia vifo vinavyotokana na mgomo huu wa madaktari.

  Madaktari wanadai nyongeza ya mishahara vifaa na mazingira bora ya kutolea huduma za afya. Mwezi huu wa Januari madaktari wanafunzi 229 waliopo katika hospitali ya rufaa ya muhimbili pia waligoma wakidai kulipwa posho zao kiasi cha shillingi 176 milioni.

  Wakati Sikika inafahamu kuwa kwa mwaka huu wa fedha serikali kupitia wizara afya imetenga kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 4.5 kwa ajili ya posho za madaktari wanafunzi, haijulikani sababu wanafunzi hao wacheleweshwe kulipwa posho hizo.
  Kwa sasa Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za kijamii na kiuchumi kutokana na mipango mibovu na uwajibikaji dhaifu. Madhara ya changamoto hizi pia yanaipata sekta ya afya. Ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi tunahitaji jamii yenye afya bora. Mchango wa sekta ya afya katika kuendeleza uchumi wetu ni kuhakikisha kila mwananchi ana afya bora na hapotezi maisha.

  Wizara ya afya na ustawi wa jamii inatakiwa kujenga ushirikiano na nguvu ya pamoja na watendaji pamoja na wadau wake. Wizara hiyo inatakiwa kufanya kazi bega kwa bega na watumishi wa afya ili kutatua changamoto zilizopo katika huduma za afya pamoja na kuboresha huduma za afya ili ziwafikie wananchi wote na kwa gharama nafuu. Ili Wizara na madaktari wafanikishe haya unahitajika uwazi, ukweli, ushirikiano, na kuaminiana.

  Sikika inatoa rai kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutumia busara na kuweka maadili mbele. Kutafuta suluhisho la dharura ili kutatua tofauti baina yao na madaktari pamoja na kuweka mazingira mazuri ya wao kufaya kazi pamoja. Wananchi wanahitaji afya na uhai.

  Wizara ina wajibika wa kuboresha uhai na afya za wananchi ili waweze kushiriki katika kukuza maendeleo yao binafsi na ya nchi kwa ujumla. ​
  [​IMG]
  Bw. Irenei Kiria
  Mkurugenzi Mtendaji, Sikika, S. L. P 12183 Dar es Salaam,
  Simu: +255 222 666355/57, Nukushi: 2668015, Barua pepe: info@sikika.or.tz, Tovuti: www.sikika.or.tz
   
 2. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hapa wakuu kama tulivyo Waafrika wengi tutaanza kuzunguka mbuyu lakini cha msingi ni kimoja tu:

  Ni kwa nini Blandina Nyoni/Hadji Mponda wasijiuzulu kwanza ili kama madai ya Madaktari hayatekelezeki tujue baada ya ujio wa wengine!??

  Hili laweza kuonekana gumu leo lakini halina budi kama kweli tunataka kujenga misingi imara ya uwajibikaji katika nchi hii changa na bara kwa ujumla
   
Loading...