Serikali na Madaktari: Nani anawajibika kwa watanzania?

MOUREEN

Member
Apr 30, 2011
37
25
Nimekuwa nikiona mawazo mbalimbali hasa katika sakata la mgomo wa madaktari. Wengine hulaumu Serikali na wengine Madaktari. Ila kwa maoni yangu: Serikali inawajibu kwa wananchi kwa sababu ndio walioiweka madarakani. Serikali then ina namna yake ya kuhakikisha vyombo vyake kama Madaktari, Polisi, Jeshi, walimu na watumishi wake wote kwa ujumla wanawajibika kulingana na mikataba kati yake na nao ikiwa ni pamoja na kusuluhisha migogoro yao. Ni katika umahiri wa serikali kuwajibika kwa wananchi ndipo wananchi wanaamua kuirudisha madarakani. Kama haiwezi, wananchi huchagua nyingine itakayoweza. Fikiri:Kila mtu akiibuka kuwajibisha vyombo hivyo vya serikali ndo nchi inaanza kuwa as if haina serikali na ndipo wananchi wanalaumiwa kuchukua sheria mkononi. Kama serikali ikitaka tuisaidie kulaumu madaktari basi pia wakubali wananchi wawasaidie kupiga wahalifu, wezi wa mali ya umma, wanasiasa mafisadi, polisi wanaouwa raia na yote yale ambayo wananchi wataona ni kero.

Hitimisho: wale wanaolaumu madaktari ni lazima wawe ni sehemu ya serikali. Sisi wananchi tuitake serikali ambayo ndo tuna mkataba nayo (katiba na ahadi za kwenye kampeni) iwajibike kulingana na mkataba alafu nayo iwajibike kwa madaktari na vyombo vyake vingine ambao ndo wanamkataba nao. Madaktari hawawajibiki kwetu na hatujui terms and conditions za mkataba wao kama tusivyojua ya makampuni mbalimbali ya madini na uwindaji, n.k. Hii ni kisheria zaidi. Pia ifahamike kuwa kodi yetu inazolipa madaktari sisi huitoa kwa Serikali na Serikali ndo inawajibika. SERIKALI ISITAFUTE HURUMA TOKA KWETU. Tunawalipa kodi ili mtutumikie. Hatukuwalazimisha. Mlituomba kura tukakubali! Please note that you are not our friends! Kikazi zaidi!
 
i katika kujipendekeza kwenu kwa ccm tunaomba mjichunge kila mtembeapo jihadharini na mabinti na mjichunge mnakula na kunywa wapi lazima tuondoke na mmoja wenu halafu mapata lessons maana watanzania wanteseka sababu ya serikali ya kufisadi na nyie mnashabikia hali hii especialy kitendo cha gerald hando lazima tujibu mapigo wenzenu watakuwa bungeni na sisi nanyie god bless you guys watch your backs:embarassed2:
 
Back
Top Bottom