Serikali na kiini macho cha bank loans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali na kiini macho cha bank loans

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by NasDaz, Jul 3, 2009.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Binafsi sina details kuhusu lini na kwanini suala la collateral liliingizwa kama condition mojawapo ili mtu akopeshwe!! Lakini nikiulizwa maoni yangu, i can say tangu pale binadamu alipopoteza sifa ya uaminifu hivyo ilibidi itumike mbinu ya kumfanya alipe deni alilokopa!!! Wakati fulani serikali ilizungumzia kutoa Hati Miliki za Mashamba ili wakulima waweze kukopeshwa!! Kwa serikali, wakulima wanashindwa kukopeshwa na mabenki kwa vile hawana HATI MILIKI YA MASHAMBA YAO!!! Ni kweli hii? Ni nyumba ngapi zina hati miliki (hususani zilizo nje ya big towns) ambazo zina hati miliki? Mbona hawa wanakopeshwa? Hivi kweli kutoa hati miliki kunaweza kuongeza thamani ya mashamba/ardhi ya kulima hata mabenki washawishike kutoa mikopo na kufanya ardhi hizo kama dhamana?! Binafsi, nahisi dhamana bora ambayo benki ingeitaka ni ile ambayo inahuzika kirahisi sokoni!! Nazani thamani ya kitu inakuwa determined na market force. Ni benki gani ambayo itakuwa tayari kutoa mkopo kwa mtu ambae nae yupo tayari ku-forgone dhamana yake kwa ajili ya mkopo aliochukua? Hivi ni wakulima wangapi leo hii ambao wanaweza kutokuwa tayari kuziachia hekari 50 zao kwa ajili ya mkopo wa 5m? Hii ni kuwahadaa wananchi, nalizungumza hili kwavile najuwa litarudi tena vichwani mwetu kipindi hiki cha bunge? Hivi serikali haifahamu kwamba benki inafanya financial business na wangependa kuwa na most liquid assets than otherwise? Mimi naamini endapo benki zingekuwa na uhakika kwa at least 95% kwamba watu watalipa mikopo yao bas nazani wasingeangalia sana mambo ya collateral. Wanataka collateral ili kum-induce aliyechukuwa mkopo aweze kulipa mkopo wake. Na ndio maana Loan officer anayeijua kazi yake kitu muhimu kwake ni uwezo wa biashara iliyokopewa kuweza kulipa mkopo huo na suala la collateral ndo linafuata? Na kwavile Collateral sio muhimu kuliko kulipwa mkopo basi always bank zitataka collateral ambazo mdaiwa hatakuwa tayari kuzipoteza kirahisi. Hivyo, endapo serikali inataka kweli kuwasaidia wakulima katika suala zima la mikopo basi haina budi kukifanya kilimo kuwa ni profitable business. Hili likifanikiwa basi automatically thamani ya ardhi itakuwa juu na hamna ambae atapenda kuipoteza. Kwavile watu hawatakuwa tayari kuipoteza then inaweza kuwa best collateral kuliko hata kama ukitoa hati miliki katika mazingira yaliyoo. Najenga hoja.
   
Loading...