Serikali na JWTZ waige Eritrea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali na JWTZ waige Eritrea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Netanyahu, Oct 3, 2009.

 1. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #1
  Oct 3, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nilibahatika kuwemo katika msafara wa wapiganaji wa misituni wasiokuwa na kombati wala vyeo wala pasipoti kutembelea nchi zinazoongozwa na maraisi waliokuwa wapiganaji wa misituni za Rwanda,Sudan Kusini na Eritria ili kujifunza kama viongozi hao wapiganaji wa zamani kama wana uwezo wa kukisimamia kile walichokuwa wakipigania au walikuwa wakipigania tu wapate utawala ili wafisadi nchi na kujaza matumbo yao tu.

  Katika nchi hizo kwa ujumla kila nchi ilituvutia kivyake.Niseme wazi maraisi wa nchi hizo tatu wanakijua wanachosimamia.

  Katika nchi ya Eriteria nililojifunza ni jinsi nchi ile kwanza inavyojua kutumia jeshi lake.Tenda za ujenzi kama wa barabara muhimu za nchi hiyo hufanywa na jeshi.Serikali hutoa tenda hizo kwa jeshi na ukiziona barabara zilizojengwa na jeshi hazina tofauti na za kampuni ya kijapani ya Konoike au Kajima zilizojengwa Tanzania.Labour costs huwa ziko chini kwani wanajeshi wale hujenga bila malipo ya ziada zaidi ya mishahara yao ya mwezi walipwayo.Serikali ya Eritria imejiwekea utaratibu wa kuhakikisha wanajeshi wanatumika productively wakati hakuna vita kufanya miradi mikubwa ya kusaidia nchi badala ya kulala kwenye makambi na kufyeka majani na makwanja kuzunguka kambi wakisubiri tarehe za mshahara zifike wachukue wakalewe pombe za bei nafuu zisizolipiwa kodi.

  Kitu kingine nimejifunza kule ni jinsi serikali ya Eriteria isivyopenda mikopo iwe toka benki ya Dunia IMF au kutoka ndani.Raisi wao ana msemo usemao USE YOUR SWEAT NOT DEBTS akihamasisha kila mahali watu wapende kutumia nguvu zao zaidi kujikwamua kibinafsi na kiinchi kuliko kutegemea mikopo.Ni muumini mkubwa wa ule msemo usemao MTAJI WA MASKINI NI NGUVU ZAKE.Kila mahali apitapo raisi yule huhamasisha watu kutumia nguvu zao zaidi kujikwamua kuliko kutegemea mikopo.Anaita mikopo kuwa ni utumwa wa hiari mambo leo ambao mtu au nchi huishia kuwa kibarua wa mkopeshaji milele asipokuwa makini.


  Japo Tanzania haina uhusiano mzuri sana na Eritria kwa sababu ambazo Tanzania inajua yenyewe lakini kuna mambo ya kujifunza kule.

  I salute you president of Eritria.keep it up.

   
 2. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  You are joking!The president is a dictator ,with massive human rights violation.Tangu mgogoro na ethiopia uishe,Bw Isaya afeweki,hataki kutoka madarakani.Bado kuna njaa huko,sijui unapiga debe la nini na nchi ya Eritrea!
  Bw Netanyahu get the fact right
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Oct 3, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwnamasala,
  Mkuu unazungumza vitu gani!..unamjua rais wa Eretria au umesimuliwa na watu!.
   
 4. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Bw Mkandara,siwezi kuandika kama sina facts.Nchi haina press freedom,at least Tz tunaweza kusoma newspapers yeyote ,sio yale ya serikali tu kama uhuru,dailynews etc.Umechemsha hapa,vita vya msituni vimepitwa na wakati,unabidi nawewe usonge mbele,kama uilijiembedd na waeritria miaka ile,usije ukahalalisha.Ni meonana na waeritria wengi,wanakimbia nchi yao kila siku
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Oct 3, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Embassy of Eritrea in Washington!!!


  Afewerki ranked No. 8 on Parade Magazine's 2009 World's Worst Dictators list, behind Ayatollah Khamenei (Iran) and ahead of Gurbanguly Berdymuhammedov (Turkmenistan).  Isaias quotes
  • "What is a free press? There is no free press anywhere. It's not in England; it's not in the United States. We'd like to know what free press is in the first place."[9]
  • "There is no victory without its people, no development without its people, who triumphed decisively through their national unity.
  • "Democracy is very important. Democracy meaning allowing majority or population to participate in the politics of every country. That is part of the software that we need to develop. But it should not polarize society.
  • "Sometimes when you have large population it becomes a liability. People speak about big populations. But they underestimate the fact that it is not numbers. It is not only the productivity of the population in one country that matters; it is also the quality of the productivity."
  • "Even when we are disappointed, we have to fight this war for peace and we have no other choice of brokers. The brokers are there, whether we like them or not. Whether we are happy or disappointed with what they are doing, we have to live with that to finally give peace a chance.
  Huyu jamaa ana sura mbili, pia ni rafiki wa marekani, we know America they once loved Saddam, Osama bin Laden, they trained Ghadafi......they have killed many innocent African leaders, never mention sources of civil wars.

  Population kubwa iliyojaa akina Mwanakijiji,Jeneral Ulimwengu, Zito Kabwe haiwezi huyu!
   
 6. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaani tuige mfano wa afwereki? this is a joke right? if its not a joke, all i can say is...miafrika....
   
 7. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #7
  Oct 3, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hata dicteta Idd amin ana vitu vizuri vya kujifunza kutoka kwake mfano alipofukuza wahindi Uganda waliokuwa wakimiliki njia kuu za uchumi njia hizo kuu za uchumi zikiwemo maduka alikabidhi waganda wazishike mali hizo na hadi sasa zipo nenda kaone Uganda tofauti na Tanzania ambayo ilipotaifisha njia kuu za uchumi ilizikabidhi kwa wanasiasa na wapenzi wao wakazila barabara na kuua mashirika karibu yote ya umma halafu wakawauzia wageni tena kwa kwa bei za chini ili na wao waanze kuzila part two.

  Yes kwa kipengele cha Matumizi ya Jeshi kujenga miundombinu Tanzania yaweza kuiga .Siombi msamaha kwa hilo tuna cha kuiga Kwa dikteta Raisi wa Eritria.

  Tofautisheni pia DEMO-Krasia na DOMO-Krasia.Hivyo Tanzania ina DOMO-krasia watu wana uhuru wa kupiga Domo na vidomo domo magazetini,redioni,n.k lakini nchi haiendi.Nchi nyingi za Afrika bado ziko kwenye kiwango cha DOMO-krasia nadhani tunahitaji madikteta watakaosaidia Kuondoa hii DOMO-krasia washinikize watu wafanye maendeleo kidikteta kama Kagame na Huyo raisi wa Eritria wafanyavyo.DEMO-krasia waweza demonstrate ukaonyesha ulicho-achieve wakati DOMO-krasia utaishia kuonyesha ushahidi wa vineno vya uhuru wa mdomoni na uhuru wa vineno vya midomoni vilivyoandikwa magazetini lakini nchi iko ziro kimaendeleo.Afrika kumejaa DOMO-krasia na Sio DEMO-krasia.
   
 8. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Idi Amin hakuisaidia Uganda hata kidogo kwa kufukuza wahindi...na miundo mbinu hawakupewa wananchi wakawaida, aliwapa mawaziri wake na marafiki zake kwanza na ndugu wanajeshi wake wakaharibu nchi pia na hakuna zuri (soma news clips za uganda economy 1972-1979) alilofanya zaidi ya kuua waganda zaidi ya 300,000...... nchi yetu pamoja na mambo mengi, kuwa na uhuru ambao uliopo ndio unasaidia kuyaanika mengi na kuwaaibisha wengi..kwa mwendo huu watu wengi watazidi kufahamu ni nani anakula pesa zao, nani mwizi...mwisho Democracy "may" prevail..democrasia ni watu wenyewe, kama wanapenda ufisadi wataendelea ufisadi, wananchi inabidi wakumbushwe kwamba hao viongozi ni waajiriwa na wananchi labda hapo watu hawata fanya mchezo...Kagame anafanya mambo makubwa kwasababu nchi na wananchi wengi wanamuunga mkono na wana moto wa kuendelea...angekuwa dictator ange-revenge na kuwashughulikia wengi sana waliyofanya maasi lakini Rwanda wakafanya mambo tofauti kabisa kisheria na siyo kulipizana visa bali kuanika nini kilitokea na kusameheana (gacaca courts) na hana upuuzi kama huyu wa eritrea ambaye bado anahusika na kuvuruga amani kwa wenzake na kufunga wananchi wake..viongozi tofauti kabisa. Nchi kuendelea kamwe isitegemee kiongozi tu, wananchi wenyewe ndio wenye nguvu za maendeleo na kumchagua huyo kiongozi...mkimchagua kiongozi Domo, mna nguvu wa kumuondoa huyo domo kwa kura baada ya miaka 5.
   
 9. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Netanyahu,umechemsha!Kagame na Museveni ni wa Watusi ,ambao nia yao ni kuzitawala Uganda,Rwanda na Burundi indefinitely!Wote ni madictator,ni tu kwa sababu ni puppet wa Marekani !Mauaji ya Rwanda,ukumbuke ni baadhi ya kutunguliwa ndege ya Marais wawili ,waliokuwa wanatoka Tanzania kwenye mkutano.Kama Rwanda kuna kura moja,mtu mmoja,Kagame hawezi kushinda,
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Netanyahu hujui unacho kiongea, assistant lecturer kule eritrea analipwa dola 140 za marekani. Wa eritrea kibao wanakimbia nchi, halafu kibaya zaidi wafadhili wakubwa wa eritrea ni Saudi arabia, al qaeda, iran, libya, sudan n.k. kwa mifano hii nadhani unaelewa nini kinaendelea.

  Huyu rais wa eritrea wakati wa vita kati yao na ethiopia aliamuru ndege za kivita kushambulia shule tatu, mbili za primary na moja ya sekondari tena kwa white phosphorous na akaangamiza wananfunzi wote.

  Hapo ndo serikali ya ethiopia ikaamua kusitisha vita, sasa unasema huyo ni mutu wa kuiga? umekosa kazi wewe, na kwa kuwani weekend nenda kanywe chibuku.

  Rais wa eritrea, mseven, kagame wote hawa wamesaidiana ktk vita na ugomvi wa eritrea na marekani ni kwa sababu walishirikiana na al qaeda wakati wanapigana na ethiopia.
   
 11. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Netanyahu tayari amekunywa Chibuku!Uzuri wa JF kuna watu wanaoelewa mambo.Sio mtu anajiandikia tu bila kuwa na facts.Thanks Magezi kwa kuchangia mada hii
   
 12. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  tatizo letu jingine, Marekani ikisema leo Kikwete ni dictator tutakubali tu kisa kagomea maslahi yao...tuache unyonge,tuna uwezo wa kujiamulia wenyewe, tuanakosa moyo wa kuthubutu...
   
Loading...