Serikali na Jamii ikomeshe ajira kwa watoto

mussaamos

New Member
Jul 15, 2021
4
3
Matatizo mengi hapa nchini huwa endelevu kwa sababu ufuatiliaji wake huwa ni wa msimu, mpaka janga litokee ndo ufuatiliaji unaanza, tukio likiisha ufuatiliaji wa kukomesha tatizo unakoma na kusubiri tatizo jingine tena, huwa hakuna ufuatiliaji endelevu.

Suala la ajira kwa watoto ni jambo mojawapo ambalo halifuatiliwi mara kwa mara ndio maana watoto chini ya miaka 18 wanaendelea kuajiriwa katika uzalishaji wa viwandani, godowns, migodini, ujenzi, majumbani, maofisini migahawani n.k.
Chanzo cha ajira kwa watoto.

*Umasikini katika jamii- wazazi wengi hapa nchini ni masikini hivyo hushawishika kirahisi kwa watoto wao kusafirishwa kwenda mijini kuajiriwa kwa kazi za ndani, viwandani n.k. ili wazazi wawe wanapata vihela kidogo kutoka kwenye ajira bila kujali madhara kwa mtoto. Pia watoto wengine kutokana na umaskini nyumbani huamua kujiingiza wenyewe katika ajira hizi.

*Ukosefu wa elimu kwenye jamii- watu wengi kwenye jamii hawana elimu hasa ya madhara ya ajira kwa watoto ndio maana huwa rahisi kuwasukuma watoto kwenye ajira hizi. Pia hata watoto wenyewe hukutwa hawana uelewa wa kutosha juu ya madhara ya kazi hii kwani unakuta mtoto kamaliza darasa la saba na miaka 13/14 anaingizwa kwenye ajira.

*Ufuatiliaji mbovu wa serikali- kungekuwa na ufuatiliaji wa kina kusingekuwa na ajira kwa watoto, mda mwingine wahusika ni kati ya wazazi na wenye kazi.

*Gharama yao ni ndogo (mshahara)- wengi wanaotoa ajira kwa watoto hukwepa gharama kubwa kwa kuajiri watu wakubwa, huona ni heri aajiri mtoto kwa 40,000 kuliko mtu mzima atakayehitaji kiasi kikubwa bila kujali madhara kwa mtoto.

*Watoto hawajui sheria- watoto huajiriwa kwani hawajui sheria, hata akidhurumiwa hawezi kuidai haki take kama mtu mkubwa. Unakuta mttoto anafanya kazi za ndani, akivunja hata sahani basi anakatwa mshahara.

Madhara ya ajira kwa watoto.

Watoto kukata tamaa za kutimiza ndoto za
o - Kutokana na ugumu wa kazi, udogo wa malipo, kejeli ama manyanyaso kutoka kwa waajiri hukata tamaa ya maisha

Kudumaa- watoto wengi wafanyishwapo kazi zito za viwandani, kubeba mizigo godowns na migodini hudumaa kiafya na kiakili na kutengeneza watu tegezezi.

Kudumaa - watoto wengi wafanyishwapo kazi zito za viwandani, kubeba mizigo godowns na migodini hudumaa kiafya na kiakili na kutengeneza watu tegezezi.


Suluhisho la ajira kwa watoto.

∆ Serikali iweke utaratibu wa kufuatilia Mara kwa Mara sehem mbalimbali zenye miradi na majumbani kwa kutumia uongozi wa mitaa ili kuhakikisha watoto hawawekwi kwenye mpango wa ajira.

∆ Serikali kwa kushirikiana na asasi za kiraia itoe elimu Mara kwa mara juu ya madhara ya ajira kwa watoto.

∆ Adhabu kali iwekwe kwa watakaobainika kuajiri watoto.

∆Serikali iratibu usafirishaji wa watoto ili kuhakikisha wanakoenda ni salama na sehemu sahihi na iwe inafuatilia wanapofika.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom