Serikali na hisa zake kwenye kampuni binafsi inakuwaje?

KITA

Member
Jan 3, 2015
20
5
Kuna nyakati najiuliza sana. Pale ambapo Serikali Yetu Ya Tanzania, moja kwa moja, ama kupitia taasisi zake, inapokuwa na hisa kwenye makampuni, je ni mamlaka gani inasimamia maslahi na haki za Watanzania?

Tunaweza kuzungumzia mamlaka kibao, ila hapa kwenye maeneo yenye maslahi ya umma, pia tuangalie. Tusisahau pia, pale ambapo wananchi wana hisa pia.

Transfer Pricing inasemaje mahala ambapo Serikali ina hisa zake? Mishahara ya wakurugenzi (hasa wageni) maamuzi, bodi, miradi n.k.

Tumekuwa tukiona jinsi makampuni haya yamekuwa na mamlaka ya kuteua (sawa coz ni majority), lakini hatuoni ni wapi Serikali yetu inaweka zuio, kama vile kuhakikisha bwana fedha ni Mtanzania, maana hapa ndipo tunapolizwa.

Mradi unaweza kugharimu mapesa kibao, kumbe makampuni yameweka "gharama zao" za experts, au hata kama ni wa ukweli, gharama zao zaweza kuwa "inflated".

Achilia mbali hilo, je, wageni hawa wana sifa? Kama vile wale jamaa waliowanyanyasa Watanzania, kiasi cha kumfukuza kazi kama kibaka Meneja Rasilimali Watu (Sam) na aliyemfuatia (Ste) kule Saruji Kusini. Yote ni kwa kuwa walisimamia maslahi ya Taifa, na haki za Watanzania, na watanzania Seniors walioacha kazi kati ya 2012 na 2015 ni zaidi ya 12.

Tuangalie hili... NAWASILISHA.
 
Back
Top Bottom