Serikali na Hatima ya ATCL

nDUGU WANANCHI,KUMEKUWA NA MAWAZO YA WATU MBALIMBALI AMBAO KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE WANAPEWA MADARAKA YA KUONGOZA NCHI MAKAMPUNI AMA MASHIRIA MBALIMBALI KWA KUPEANA AMA KUJUANA KINDUGU,,SASA BASI IMEFIKA SASA WANANCHI WAMEONA BASI INATOSHA NA YOYOTE ALIETUMIA MADARAKA YAKE VIBAYA LAZIMA AFIKISHWE KWENYE MKONDO WA SHERIA,,JF KAMA SEHEMU YA KUFUNDISHANA NA KUMSHAURI RAISI NINI AFANYE NANAI AMTEUE...TUMEONA MAWAZIRI MBALI MBALI MRH MRAMBA NA MH YONA WAKIKWAA GARI LA KIJANI KUELEKEA KEKO KUJIBU TUHUMA ZA UBADHIRFU WA MALI YA UMMA KWA KUTOA MISAADA YA AJABU AJABU..SASA BASI HIVI SASA TUSIKIMBILIE TU SIMBA WAKUBWA WAKUBWA TWENDE KUWAONYESHA ADABU WALE WANAOPEWA HAKI YA KUONGOZA MASHIRIKA YA UMMA KAMA ,,BOT.TANESCO.TRLA,TTCL.ATCL NA MENGINEYO....MAJUZI NIMESOMA KIJARIDA KIMOJA KUTOKA HAPA JF KINAONYESHA JINSI BAADHI YA VIONGOZI WA ATCL WALIVYOLITAFUNA SHIRIKA LA AIRTANZANIA BILA AIBU...NA KILICHONIUMA ZAIDI NILIPOONA KUNA BAADHI YA WANABODI WAMEGAWANA DOLLER 11,000 NDANI YA WIKI MBILI HUKU KUKIWA NA WAFANYAKAZI AMBAO HAWAJALIPWA MISHAHARA YAO MPAKA LEO HII....NADHANI KUNA TATIZO KUBWA SANA KAMA KIONEKANAVYO HAPO CHINI...MH RAISI HIVI SASA TUANZE KUWAFUNDISHA ADABU HAWA VIONGOZI WA MASHIRIKA YA UMMA WANAOIBA WAKIJUA UMEWACHAGUA NA HIVYO HAKUNA MKONDO WA SHERIA UTAKAOWAFWATA
NA KATIKA KUANZA NA HILI TUNAOMBA

MH MUSTAFA NYANGANYI NA MKURUGENZI WAKE BWANA DAVID MATTAKA WAWE FUNDISHO KWA WALE WOTE WALIOPEWA DHAMANA YA KUONGOZA MASHIRIK YA UMMA KUANZA KUYAHESHIMU KWA KUWAFIKISHA KWENYE MKONDO WA SHERIA(MAHAKAMANI),HARAKA IWEZEKANAVYO
NINA UHAKIKA KAMA MH UJUAVYO BWA DAVID ALIONDOLEWA KWA UBADHIRIFU PALE PPF NA KWA USWAHIBA WAKO UKAAMUA KUWASAKAZIA MASIKINI WAFANYAKAZI WA ATCL..NAAMINI KAMA ALIPOONDONDOLEWA
ANGEFIKISHWA KWENYE MKONDO WA SHERIA LEO HII ASINGE FANYA UBADHIRIFU WA HALI YA JUU KAMA UNAVYOSOMA HAPO CHINI.....

LENGO LETU SI TU WAJIUZULU MANAGEMENET NA BODI YAKE ,LA HASHA KUNA USHAHIDI WA KUTOSHA KATIKA YALIOANDIKWA HAPO CHINI KUHUSU WIZI WA MALIZ A KAMPUNI HIVYO NI LAZIMA WARUDOSHE MALI ZA WATANZANIA.....HAIWEZEKANI GARI USED INANUNULIWA DUBAI KWA MILLION 25,000 MTU KWA MOYO WAKE WOTE NA KWA ROHO YAKE YOTE NA NAFSI YAKE ANAANDIKA GARI IMENUNULIWA KWA DOLLER 72,000.....
MFANO MDOGO NI HIZO NDEGENDOGO SOKO LA DUNIA KILA SEHEMU NI USD MILL4.5 LAKINI UNAAMBIWA WAMENUNUA KWA USD MILLION7.5....MFANO MWINGINE NI UNUNUZI WA AIRBUS...SOKO LA DUNIA NI 260,000USD LAKINI WAKANUNUA 360,000USD LEO HII WANGEKUWA WAPI KWA DIFF YA 100,000USD AMA 3MILLION USD KWA KILA NDEGE NDOGO WALIONUNUA...JE SWALI LANGU UKIACHA PESA WANAZOPATA KUTOKA KWA MARUBANI KAMA KAMISHENI DOLLER 3000USD INAINGIA MIFUKONI MWAO MOJA KWA MOJA NA USHAHIDI UPO....KUNA HAJA GANI YA WAO WAJIUZULU TU..

TUNAOMBA RAISI, WOTE WALIOSHIRIKI KUIUA ATCL WAFIKISHWE MAHAKAMANI MARA MOJA
WAKO SWEETBABY
UKIPENDA MALOVE
 
Unahitaji Kuelimishwa!
Kwanza, Serikali haijatoa fedha zozote kwa ATCL baada ya kujitoa from South Africa. Pili, Serikali inabidi itoe maelzo ya jinsi gani imeisaidia ATCL financially, badala ya kuja na lugha ya kutoa siku saba. Tatu, Mataka ndiyo mtendaji mkuu wa ATC, Board members na Mwenyekiti wao Balozi Nyanganyi ni washauri kutokana na uzoefu wao kusaidia kuliendesha shirika la ndege. BALOZI Nyanganyi aliacha shirika la ndege likiwa na ndege kibao alikpokuwa waziri wa mawasiliano, huduma zilikuwa safi. nilikuwa nikisafiri kwenda Uingereza na ATC, serikali haitaki kusema ukweli "what happened", same stories "Mikataba mibovu" ndiyo imeliuwa shirika hili. Kina MATAKA NA NYANGANYI, wamekabidhiwa shirika halina ndege, madeni kibao, no money, sasa mnataka hawa watu wafanye mazingaombwe. Please hembu tuwe wachambuzi wa mambo na kutafuata ukweli badala ya kupenda kupiga gumzo.
 
Unahitaji Kuelimishwa!
Kwanza, Serikali haijatoa fedha zozote kwa ATCL baada ya kujitoa from South Africa.

Hapa jukwaani tunaongelea ukweli na wala si ubabaishaji, ATCL ilikuwa inachotewa pesa kutoka hazina kila mwezi kiasi cha 500m/=, muulize Mattaka Au Nyang'anyi juu ya hilo. Suala la msingi ni Mwenyekiti na CEO waeleze hizo pesa walizitumiaje, kukopeshana magari au kulipana posho za vikao. Pia waulize walitaka wachotewe kutoka katika pesa za walipa kodi hadi lini?

Vilevile kama serikali haijatoa fedha YEYOTE, je zile ndege mbili za D-8 fedha zake zimetoka katika mifuko ya nani?


Pili, Serikali inabidi itoe maelzo ya jinsi gani imeisaidia ATCL financially, badala ya kuja na lugha ya kutoa siku saba. Tatu, Mataka ndiyo mtendaji mkuu wa ATC, Board members na Mwenyekiti wao Balozi Nyanganyi ni washauri kutokana na uzoefu wao kusaidia kuliendesha shirika la ndege.

Ni vema ukaelewa kazi za Mtendaji Mkuu ni zipi na za Bodi zipi. Mtendaji Mkuu anawajibika kuendesha na kusimamia shughuli za kila siku za ATCL.
Bodi ina wajibika kusimamia shughuli za ATCL kwa niaba ya Serikali, ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi yote ya kisera kwa niaba ya serikali.
Hata siku moja bodi haiwezi kuwa ni washauri wa ATCL.


BALOZI Nyanganyi aliacha shirika la ndege likiwa na ndege kibao alikpokuwa waziri wa mawasiliano, huduma zilikuwa safi. nilikuwa nikisafiri kwenda Uingereza na ATC, serikali haitaki kusema ukweli "what happened", same stories "Mikataba mibovu" ndiyo imeliuwa shirika hili.

Ndugu yangu wewe ndiye hasa husemi ukweli, wakati Balozi Nyang'anyi akiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi ATC ilikuwa haitengenezi faida zaidi ya hasara. Kumbukumbu za mahesabu ya ATC zinaweza kubainisha haya ninayoyaandika. Zaidi ya hapo wakati wa Balozi Nyang'anyi ATC ilikuwa haendi Uingereza kama unavyodai. Na kama Balozi Nyang'anyi aliendelea kuwepo baada ya kumng'oa Rwebangira (Mmoja kati ya GM wengi waliopita ATC), basi atakuwa na maswali mengi ya kujibu juu ya Mradi uliyoiletea hasara ATC wa International Operations (IOPS). Katika kipindi hicho ATC ilikodi ndege moja ya aina ya Boeing 767 kutoka Ethiopian Airlines kwa ajili ya safari za UK nadhani na Rome, Italy. Mradi ambao haukudumu kwa muda mrefu baada ya kuingizia ATC hasara ya mamilioni ya fedha.

Kina MATAKA NA NYANGANYI, wamekabidhiwa shirika halina ndege, madeni kibao, no money, sasa mnataka hawa watu wafanye mazingaombwe. Please hembu tuwe wachambuzi wa mambo na kutafuata ukweli badala ya kupenda kupiga gumzo.


Hawa jamaa unavyojaribu kuwasafisha ndiyo unazidi kuwachafua kabisa, kama hawa jamaa wangekuwa ni wakweli na wanania safi sidhani kama wangeliweza kukubali kuingoza ATCL wakati wakijua kuwa ATCL ina matatizo ambayo wao hawana uwezo wa kuyatatua. Isitoshe kama wali-oversight wakati wanapewa nyadhifa hizo kwanini hawakutumia busara zao kuomba kujiuzulu kama kweli wameona hawawezi kutimiza matakwa ya mwenye mali, walikuwa wanangoja nini au walikuwa wanafanya biashara gani wakati wote huo?.[/QUOTE]

Mwisho kabisa bado nitasimamia ushauri wangu ambao nimekuwa nikiutoa kila siku, Serikali haina budi kukodisha menejimenti kutoka kwenye makampuni yaliyobobea katika kutoa huduma za kimenejimenti za usafiri wa anga. Menejimenti itakayokodishwa inaweza kupewa mkataba wa miezi 36 hadi 48 huku serikali ikiwaajiri watanzania (hapa ninapendekeza vijana) ambao watafanya kazi sambamba na wataalam hao ili waweze kupatiwa uzoefu ambao utakuwa ndiyo mhimili wa uongozi baada ya mkataba kumalizika. Sasa hivi ATCL haina capacity ya kufanya kazi zake au kubuni mipango mbalimbali kwa kufanya tafiti ambazo zitakuwa zimetoa mwanga na mwelekeo wa kutosha katika uendeshaji na usimamiaji wa shughuli za kila siku. Kwa kukodi menejimenti ya wataalam ni rahisi kutumia researches ambazo ziko ready made ambazo wataalam hao watakuwa nazo kutoka na uendeshaji wa menejimenti nyingi na tofauti. Hizo tafiti ambazo zimekwisha fanyika ni rahisi kuzihuisha (Customize) na hali halisi ya ATCL na kupata mwelekeo ulio sahihi.

Endapo serikali itaamua kuendelea na ATCL katika mfumo ule ule usiobadilika basi drama ndani ATCL hazitakwisha.

In short katika ulimwengu wa leo wa Mashirika ya ndege ATCL inaendeshwa kiubabaishaji kabisa.
 
Invincible
JF Senior & Premium Member Join Date: Sat May 2006
Location: Songeaonline
Posts: 768
Rep Power: 24

Thanks: 60
Thanked 319 Times in 195 Posts
Credits: 41,995

Re: ATCL yaondolewa IATA!

--------------------------------------------------------------------------------

Kuna mwandishi wa habari mwenye heshima inayodidimia (controversial) anaitwa Makwaia wa Kuhenga aliandika makala katika gazeti la Daily News miezi si mingi iliyopita. Nimesahau ni toleo gani. Alimsifu bwana David Mataka kwamba ameweza kuliletea ufanisi shirika la ATCL.

Najua huyu mwanahabari ni mwana CCM mkereketwa. Lakini uandishi wa aina hii unamporomosha yeye na vinavyomzunguka.
__________________
Tanzania - Dola dhaifu, Viongozi wababe, Wananchi usingizini


MKUU INVINCIBLE:::HUYU JAMAA ANAKUJA KUCHUKUA CHAKE KILA MWISHO WA MWEZO PALE ATCL.....NA SIO SIRI WALA CHA KUFICHA WATU WALISHAULIZA HIZI PESA ZINATOLEWA KIVIPI IKABAKI KAMUULIZE MATTAKA....HII NDIO ATCL YA SASA
USISHANGAE HATA SIKU MOJA HATA WAKIONDOLEWA ATAANDIKA MADA YA KUSIKITIKA
KAKOSA MPUNGA KUNA UCHAFU MWINGI TU PALE UNAFANYIKA ILA NAFIKIRI WATU WAMECHOKA
\
IMAGINE KILA IJUMAA MATTAKA ANACHUKUA MILLION 1....WANADAI YA KUKIDHI MAITAJI YA WIKIENDI USHAHIDI UPO...NA KAMA AMUAMINI MKITAKA WATU WAKANYEE GEREZANI WALETE EXT AUDITOR WAONE KAMA WATU HAWAJAKIMBIA NCHI....

KUNA HUYO MUHUNI ANACHUKUA KILA MWEZI AJAAJIRIWA NA KAMPUNI......

KUNA HILI LINGINE AMBALO NI LA KINYAMA ,,KUNA MABINTI WAMELETWA KAMA KUJA KWENYE TRAINNING IMEMALIZIKA KUTOKANA NA KUTEMBEA NA MABOSI DIR..NA MANAGER'S KILA MWISHO WA MWEZI KUNA DIR NA MANAGER WAKE WAMAMURU WAWE WANALIPWA KIASI KADHAA ....MI SIJAELEWA BADO....MKIAMBIWA RUSHWA YA NGONO HAISHI HAMTAKI...KUNA KIBINTI KIMOJA MASKINI KINAANZIA NA ""G""">>>>>"Y.
kameolewa majuzi hakana wiki watu walikuwa kwenye harusi wanamsabahi bwana wake huku wakijua kuna manager mmoja pale atcl anamcharaza kama majiya kunywa.......
tuwaachie wenyewe wafanyakazi atcl
 
Jamani, hivi nyinyi hamjiulizi kwa nini serikali haijatoa tamko hadi leo?? Mataka na balozi nyanganyi wameeleza wazi tatizo ni nini, pesa haijatoa hata sumni SINCE Ahadi hizo zianze last two years. Issus zote za madeni yaliyoachwa baada ya kutenguana na afrika kusini hayajalipwa. Tatizo si uongozi, viongozi tatizo ni FEZWA!!! Na ukiwa na madeni hakuna benki itataka kukukopesha. Serikali imesikia yote yaliyosemwa na uongozi wa ATC mbona hakuna majibu?? Na sababu ni kubwa ni UTEKELEZAJI WA MAAGIZO SERIKALINI, HUU URASIMU LAZIMA TU-UTAFUTIE DAWA. Tusubiri kama serikali itasema kuwa iliwapa shilingi ngapi ATC na wakashindwa kufanya kazi, hembu wabongo tuwe wapembuzi wa mambo. Mimi siko bongo lakini ninafuatilia habari hizi kwa utaratibu na kumake sense out of it.
 
Jamani, hivi nyinyi hamjiulizi kwa nini serikali haijatoa tamko hadi leo?? Mataka na balozi nyanganyi wameeleza wazi tatizo ni nini, pesa haijatoa hata sumni SINCE Ahadi hizo zianze last two years. Issues zote za madeni yaliyoachwa baada ya kutenguana na afrika kusini hayajalipwa. Tatizo si uongozi, tatizo ni FEZWA!!! Na ukiwa na madeni hakuna benki itataka kukukopesha. Serikali imesikia yote yaliyosemwa na uongozi wa ATC mbona hakuna majibu?? Na sababu ni kubwa ni UTEKELEZAJI WA MAAGIZO SERIKALINI, HUU URASIMU LAZIMA TU-UTAFUTIE DAWA. Tusubiri kama serikali itasema kuwa iliwapa shilingi ngapi ATC na wakashindwa kufanya kazi, hembu wabongo tuwe wapembuzi wa mambo. Mimi siko bongo lakini ninafuatilia habari hizi kwa utaratibu na kumake sense out of it.
 
Jamani, hivi nyinyi hamjiulizi kwa nini serikali haijatoa tamko hadi leo?? Mataka na balozi nyanganyi wameeleza wazi tatizo ni nini, pesa haijatoa hata sumni SINCE Ahadi hizo zianze last two years. Issues zote za madeni yaliyoachwa baada ya kutenguana na afrika kusini hayajalipwa. Tatizo si uongozi, tatizo ni FEZWA!!! Na ukiwa na madeni hakuna benki itataka kukukopesha. Serikali imesikia yote yaliyosemwa na uongozi wa ATC mbona hakuna majibu?? Na sababu ni kubwa ni UTEKELEZAJI WA MAAGIZO SERIKALINI, HUU URASIMU LAZIMA TU-UTAFUTIE DAWA. Tusubiri kama serikali itasema kuwa iliwapa shilingi ngapi ATC na wakashindwa kufanya kazi, hembu wabongo tuwe wapembuzi wa mambo. Mimi siko bongo lakini ninafuatilia habari hizi kwa utaratibu na kumake sense out of it.

ok tuseme serekali hakutoa fedha kwa uongozi wa atc, sasa hizo hela walizo kuwa wanafuja walitoa mfukoni kwao.
 
HTML:
ATCL yawatupia mzigo Mramba, Chenga, Lowassa 

Leon Bahati


SAKATA la kusimamishwa kwa Shirika la Ndege Tanzania Tanzania (ATCL) katika kuto huduma limechukua sura mpya baada ya Ikulu pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Basil Mramba na Andrew Chenge kuhusishwa hivyo kutakiwa kutoa maelezo.


Wengine ambao nao watatakiwa kutoa maelezo kuhusiana na suala hilo ni Ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi pamoja na maofisa watendaji wa Wizara ya Miundombinu wakati ikiwa chini ya mawaziri wawili wa kwanza wa serikali ya awamu ya nne, Basil Mramba na Andrew Chenge.


Habari za kuaminika zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana zilieleza kuwa maelezo yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa ATCL, Balozi Mustapha Nyang'anyi kwa Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa wiki iliyopita, zimehusisha vigogo hao katika kiini cha matatizo ndani ya shirika hilo.


Wiki iliyopita, Dk. Kawambwa alimpa siku saba Nyang'anyi kutoa maelezo yanayohusu sababu zilizosababisha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Anga (TCAA) kunyang'anywa ATCL leseni ya kurusha ndege.


Nyang'anyi aliwasilisha maelezo hayo wiki iliyopita na kutaja baadhi ya mamlaka hizo za serikali kuwa zilipatiwa maelezo ya kina kuhusu hali ilivyo ndani ya ATCL pamoja na mapendekezo yanayotakiwa kufanywa, lakini hakuna kilichofanyika katika kuliokoa shirika hilo.


Waziri Kawambwa pamoja na timu ya wataalamu wake waliyapitia maelezo hayo mwishoni mwa wiki walibaini kuwa katika kufikia maamuzi ya utetezi huo, inabidi wapate maelezo ya kina kwa mamlaka hizo ambazo kwa nyakati tofauti siku za nyuma, walitakiwa tarifa ili wanusuru shirika hilo.


Dk. Kawambwa jana aliliambia gazeti hili kuwa bado wanaendelea kushughulikia maelezo hayo ya bodi na kuahidi kutoa tamko rasmi baada ya kukamilisha mchakato.


Chanzo chetu ndani ya wizara hiyo, zilisema kuwa mkakati huo umefikia mahali pagumu kwa kuwa mbali na kupata maelezo ya vigogo kadhaa, itabidi wachunguze msimamo wa serikali tangu ilipoazimia kuvunja mkataba na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA).


"Utetezi wa bodi umetupa wakati mgumu na wala sifikiri kama maamuzi yanaweza kutoka mapema," kilieleza chanzo hicho kikifafanua:


"Ofisi nyeti sasa zimehusishwa... Maamuzi hayawezi kufikiwa mpaka tupate kauli zao, kama ni kujikwaa itajulikana ni wapi."


Ingawa chanzo hicho hakikuweza kuweka bayana namna watakavyoweza kupata maelezo ya mamlaka hizo, lakini kimeweka wazi kuwa chunguzi huo, utafanywa pia kwa kuzingatia mikakati na mipango ya serikali kwa ATCL kuanzia utawala wa serikali ya awamu ya tatu.


Kulingana na maelezo ya bodi, serikali ya awamu ya nne ilipoamua kuvunja mkataba na SAA, iliweka maazimio ya kutoa fedha za kuifufua ATCL jambo ambalo halikutekelezwa.


Miongoni mwa mambo ambayo yamo kwenye maelezo hayo na ambayo pia Balozi Nyang'anyi aliwahi kulieleza gazeti hili ni serikali kutotekeleza ahadi yake ya kulipa deni la ATCL linalofikia Sh19 bilioni pamoja na mtaji wa dola za Marekani 67 milioni.


Wakati huo huo, serikali imetoa zaidi ya dola 100,000 kwa ajili ya kusafirisha maofisa wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Anga (TCAA) kwenda kukagua karakana zinazotumika kufanyia matengenezo ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) nchini Kenya na Afrika Kusini.


Sehemu ya fedha hizo pia itatumika kwa ajili ya kununua vipuri vya ndege ambavyo ni kwa ajili ya matengenezo madogomadogo ya dharura kwenye karakana ya ATCL.


Habari zilizopatikana jijini Dar es salaam jana na kuthibitishwa na Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa zilisema kuwa mkakati huo ni sehemu ya kuhakikisha kuwa ATCL inarejeshewa haki yake ya kurusha ndege waliyonyang'anywa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Anga (TCAA).


Katika kufanikisha hilo, alisema serikali imekusudia kutumia dola za Marekani 273,000 kwa ajili ya kufanikisha kusudio hilo.


Hata hivyo, Dk. Kawambwa hakuwa tayari kuelezea kwa undani taarifa ya serikali kutoa zaidi ya dola 100,000 kwa ajili ya kusafirisha maofisa wa TCAA na ununuzi wa vipuri, kwa maelezo kwamba ni suala la kiutendaji zaidi.


Wakati huo huo, Ofisa Uhusiano wa TCAA, Abel Ngapemba alithibitisha kuwa wataalamu wake wanaendelea kupitia nyaraka mbalimbali za ATCL zilizopelekwa mahususi kusahihisha kasoro zilizoonekana ndani ya shirika hilo.


Hata hivyo, alisema ni vigumu kueleza iwapo kuna uwezekano wa ATCL kurejeshewa leseni yake katika siku za karibuni kwa maelezo kuwa wataalamu wa TCAA, kwa sasa wametingwa kiasi kwamba imekuwa vigumu kupata upenyo wa kueleza hatua waliyofikia.


"Wataalamu wetu wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana. Hata walipo siyo rahisi kuwasiliana nao maana 'wako-buzzy' (wametingwa) sana," alisema Ngapemba.


ATCL ilikuwa imeahidi kukamilisha mpango wa masahihisho wa nyaraka zake ndani ya siku 10 ambazo ziliisha jana.


Ngapemba alisema kuwa ATCL tayari imewasilisha vielelezo hivyo na sasa inasubiri maamuamuzi ya TCAA.


TCAA waliinyang'anya ATCL baada ya kubainika kuwa na kasoro kadhaa kwenye nyaraka zake za kuendeshea shirika ambazo ni kinyume na kanuni za Umoja wa Mashirika ya Ndege Duniani (IATA).


Serikali iliamua kuingilia kati na kusaidia fedha za kufanikisha mpango wa ATCL kurejeshewa leseni yake baada ya kubaini kuwa shirika hilo linakabiliwa na hali mbaya ya fedha.

wengi wataumbuka tusubiri!!!
 
Jamani, hivi nyinyi hamjiulizi kwa nini serikali haijatoa tamko hadi leo?? Mataka na balozi nyanganyi wameeleza wazi tatizo ni nini, pesa haijatoa hata sumni SINCE Ahadi hizo zianze last two years. Issues zote za madeni yaliyoachwa baada ya kutenguana na afrika kusini hayajalipwa. Tatizo si uongozi, tatizo ni FEZWA!!! Na ukiwa na madeni hakuna benki itataka kukukopesha. Serikali imesikia yote yaliyosemwa na uongozi wa ATC mbona hakuna majibu?? Na sababu ni kubwa ni UTEKELEZAJI WA MAAGIZO SERIKALINI, HUU URASIMU LAZIMA TU-UTAFUTIE DAWA. Tusubiri kama serikali itasema kuwa iliwapa shilingi ngapi ATC na wakashindwa kufanya kazi, hembu wabongo tuwe wapembuzi wa mambo. Mimi siko bongo lakini ninafuatilia habari hizi kwa utaratibu na kumake sense out of it.

MKUU ASHANY2:
NATUMAINI U MZIMA HERI YA XMASS NA MWAKA MPYA,HONGERA KWA MAWAZO YAKO ILA NAOMBA NIKUULIZE AMA WAULIZE WALIOKUTUMA MASWALI YAFUATAUYO

1:UNUNUZI WA AIRBUS
UNUNUZI WA NDEGA YA AIRBUS UMEKUWA KITUKO CHA MWAKA HATA UKILETA MTU KUJA KUFWATILIA NATUMAINI WENGI WATAKIMBILIA NAIROBI WATIMULIE MBALI...JE HIZO PESA WALIZITOA WAPI???KUNA DIR NA ENG WALIKAA KULE KWA PAMOJA WALIZALISHA JUST 78,000USD KWA KUKAA KULE HIZO HELA WALIPATA WAPI??

2:UNUNUZI WA MAGARI YA MITUMBA
KWANZA UNAJUA NIKOSA KUNUNUA MITUMBA SERIKALINI??SASA BASI WAULIZE WAKATI WAKIENDA KULIPIA MAGARI YALIOCHAKAA NA KUNUNUA KWA MILLION 20 NA MENGINE MILLION 3 NA KUJA NA KMAKARATASI YAMEANDIKWA MALANDCRUISER MILLION 72,000 MENGINE MILLION KUMI HIVI KISIMA CHA HIZI PESA UNAWEZA KUWAELEKEZA MKUU ASHANY2WALITOLEA WAPI KAMA HAWAKUPEWA NA SERIKALI???/KWA TAARIFA YAKO KABLA AATUJAJA NA BREAKING NEWS STANBIC BANK WAMEKAMATA MAGARI ZAIDI YA MATATU LEO HII HUKU WAKITAFUATA MENGINE YALIOTOLEWA KAMA MDHAMANA .....

3:UNUNUZI WA NDEGE NDOGO
WAKATI WAMEINGIA WALIPEWA JUKUMU LA KUNUNUA NDEGE NDOGO AMBAZO KA TAARIFA YAKO TU ..NARUDIA KWA TAARIFA YAKO TU HIZ\I NDEGE KWENYE SOKO LA DUNIA NI BILLION 4 LAKINI KWENYE KUNUNUA WANAPOJUA WAO NA KAMISHENI YAO WAMEANDIKA NDEGE IMENUNULIWA BILLION 7.5 UNALIJUA HILI UNAWEZA KUTUSAIDIA JIZI PESA ZOTE WALIPATA WAPI...

4:SAFARI ZA NDANI NA ZA NJE
MKUU NAOMBA NIKIHAKIKISHIE NA KAMA UNAWEZA KUPATA MTU WA KUANGALIA MAHESABU PALE WAKWAMBIE KAIKA MWAKAMMOJA ALIOKAA MH MATTAKA ALIWEZA KUTUMIA SH MIILLION 110 MPAKA MAJUZI TUNAONDOKA..NA DIR WA OPERATION ALIWEZA KUTUMIA MILLION 77 MPAKA SASA KWA KUGAWANA ZA SAFARI WACHA MSAIDIZI WAKE AMA ANEMSAIDIA KAMA SIJAKOSEA ANAITWA SOMEBODY MANJI
ALITUMIA SI CHINI YA MILLION 58,HIYO MPAKA TUNAONDOKA.....UNAWEZA KUTUSAIDIA NA KUWAAMBIA UMA HIZO PESA WALICHIMBA KISIMA KIPI...

KWA TAARIFA YAKO TENA STANBIC BANK LEO WAMEKAMATAA MAGARI 2 YA ATCL WAKITAFUTA MMENGINE 4 WALIOTOLEWA DHAMANA ...MI SIKO TANZANIA KAMA WEWE ILA NAPENDA KUWA MKWELI KWA AJILI YA WATANZANIA....

NAKUTAKIA KILA LA KHERI NA XMASS NJEMA NATUMAINI MTAJIPANGA UPYA MKIJA KUTOA MAJIBU
 
Mtajiwa mskini ni nguvu zake mwenyewe...kweli kabla ujafa ujaumbika
habari zilizotufikia punde yala mashangingi yalionunuliwa na Kampuni ya ndege ya ATCL....yamekamatwa na YONO ACT MART kwa niaba ya STANBIC BANK.na hii ni kutokana na madeni ya pesa waliochukua kwa kutumia dhamana ya magari hayo....wakiongea na chanzo husika kinasema yono walikwenda usiku wa kuamkia majuzi na kufanikiwa kukamata mashangingi zaidi ya 7 na kuacha moja lenye matatizo....

MH NYANGANYI, CEO DAVID MATTAKA kuna haja ya kundelea na uongozi a kampuni hii kweli kama imefikia hivyo..mi niko nje najaribu kuwasiliana na baadhi ya ndugu zangu wabunge ikiwezekana hata kwenye kikao kijacho niwatumie data waanzishe hoja za kuwafukuza nafikiri hili ni shirika la watanzania si shirika la watu wangoni na watu wa kondoa...hivyo basi ni bora tujipage kuanza kulinyanyua kwa uongozi mwingine!!!!

polen wafanyaakazi nina kadada changu pale sijui hata kama wamepata kamshahra chao mbuzi masikini
 
mod tunaomba ikae kwa muda kabla ya kuamishwa tupate maoni ya watu
SOURCE-MWANANCHI 27/12/2008
SERIKALI KUIFUMUA ATCL KESHO?

Serikali kesho itatoa uamuzi wa nani awajibishwe kutokana na uzembe iliosababisha shirika la ndege la tanzania ATCL kuzuiwa kutoa huduma kwa kunyanganywa leseni ya usafiri wa anga(AOC)
Uamuzi huo utatolewa baada ya Waziri wa miundo mbinu DK KAWAMBWA pamoja na jopo lake la wataalamu kupitia ripoti iliowasilishwa na mwenyekiti wa bodi wa atcl bw mustafa nyanganyi
Habari zilizotufikia j na kuthibitishwa na Katibu Mkuu wa miundo mbinu mh Omar Chambo zilisema DK kawambwa anatarajia kupasua jipu mapema asubuhi
"Ni kweli uamuzi utatolewa jumatatu alisema mh omar"
Waandishi wa habari mtaitwa na mtaelezwa alisema chambo alipokuwa akizungumza na mwananchi jumamosi jana..
ATCL ailinyanganywa haki ya kuruka mapema mwezi huu baada ya kubainika kasoro kadhaa kwenye nyaraka zake za utendaji,na kufanya bodi kupewa siku saba kutoa taarifa nini kilichofanyikana kuahidi kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika walihusika na uzembe huu
Chanzo chetu cha wizara kimesema uwezezekano mkubwa wa BODI NA MENEJIMENT YAKE KUFUTILIWA MBALI kama si KULAZIMISHWA KUJIUZULU baada ya kubainika na uzembe kiutendaji...kwa mujibu wa habari hizo menejiment ilikuwa na taarifa juu ya dosari hizo miezi kadhaa iliopita na baadhi ya barua kuonyeshwa kuwakumbusha tunazo hapa
mh katibu alisema
""KAMA WAMEWEZA KUTOA AHADI YA SIKU KUMI KUREKEBISHA KASORO ILIKUWAJE WAKASHINDWA NDANI YA MIEZI MITANO...HAYO NI MAMBO YALIOJADILIWA WAKATI WA UTETEZI WA BODI
WAKATOA MFANO BAADA YA TATHIMINI KUFANYIKA ILIBAINIKA ATCL INAITAJI DOLLER 273,000 ILI KUFANIKISHA KUONDOA DOSARI HIZO ZILIZOKUWEPO KIWANGO AMBACHO KINGEWEZA KUTOLEWA NA MENEJIMENTI HUSIKA NA KILIKUWA NDANI YA UWEZO
MOJA YA UTETEZI WA BODI NI KWAMBA SERIKALI AIJAWAPA HELA NA KULIPA DENI LA BILLIONI 19.
VILEVILE BODI ILILALAMIKA KUWA IMEWASILIANA NA OFISI ZOTE KUANZIA WAZIRI MKUU MPAKA WAZIRI MHUSIKA ,,KATIKA KUJADILI HOJA HIYO ILIELEKEZWA HAIUSIANI NA TATIZO LA KUNYANGANYWA LESENI YA ATCL KABISA KWA SABABU PAMOJA NA HILO BADO SHIRIKA LILIKUWA LINAENDELEA KUPATA FAIDA NA KUWEZAKUWALIPA WAFANYAKAZI WA ATCL WALIO KARIBU 370
""""KWANZA WANGESEMA KUWA NI KUTATUA DOSARI ZILIZOKUWEPO LISINGEKUWA NI SWALA LA SIKU MOJA AMA MWEZI MMOJA
NI JAMBO AMBALO LINGEFANYWA TARATIBU NA WALA LISINGEIATHIRI BIASHARA HIYO KILIELEZA CHANZO

HABARI NYINGINE ZILIELEZA KUWA BAADHI YA WATENDAJI WA MENEJIMENT YA ATCL WALIZEMBEA KWA MAKUSUDI KATIKA KUTUMIA TAALUMA YAO NA KUZUZIA DOSARI ZILIZOJITOKEZA...KIBAYA ZAIDI ILIDOKEZWA WAFANYAKAZI WENGI HASWA WALIO KWENYE MENEJIMENT WANAFIKA OFISINI KWA MUDA WANAOTAKA WAO NA WENGINE HATA KUTOFIKA KABISA NA HUKU IKIELEZWA WENGI WANA OFISIS ZAO PALE MJINI KARIBU NA MAKAO MAKUU YA ATCL NA HIVYO KUFANYA SUALA LA UTENDAJI KUWA DHAIFU KUTOKANA NA KUFUATILIA AMA SHUGULI ZAO AMA BIASHARA ZAO BINAFSI...KATIKA KUONYESHA HILI CHANZO CHETU TULIONYESHWA BAADHI YA MAKARATASI YA BIASHARA AMBAYO MMOJA WA WALIO KWENYE UONGOZI WA ATCL AMEKUWA AKISHINDA KUTWA NZIMA BANDARINI NA HIVYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI IPASAVYO...
TUNAMTAKIA KILA LA KHERI MH WAZIRI NA MAAMUZI YOYOTE YATAKAYOINUFAISHA ATCL NA WATANZANIA WOTE BILA KUJALI MASLAHI BINAFSI YA URAFIKI NA USWAHIBA ULIOPO
 
THERE IS NO DOUBT THIS YR CHRISTMASS HASS BEEN UNPLEASANT TO ATCL WORKERS AND THEIR FAMILIES..IN VIEW OF BITTING DOUBLE -DIGIT INFLATION,THE POOR WORKERS WILL FIND THIS FESTIVE TOO LONG TO BEAR
SUPRISINGLY ,TH AIRLINES OBVIOUS SHUTDOWN HAS RESULTED IN FINGER POINTING WITH EACH BLAMEING THE OTHER FOR THE FALL.
THE COMPANY'S CHAIRMAN BLAMED THE GOV FOR NOT HEEDING SEVERAL sos SENT OUT FOR FINANCIAL HELP
HE URGED GOV TO INJECT SOMETHING LIKE $67 MILLION EASY LIKE THAT TO REVIVE BUT WHICH COST OTHER AUTHORITIES HAVE PUT AT BETWEEN $300MILLION AND $600MILLION..
THE CHIEF EXEC DAVID MATTAKA HAS BLASTED THE STARS FOR THE MISHAP,HEAPING BLAME ON WHAT HE CALLED "UNDONE DOCOMENTS"
THE REAL FIRE WORKS ,HOWEVER ,SPARKED FROM THE WORKERS WHO FEW FEW DAYS AGO LASHED OUT AT THE AIRLINE BOARD OF DIRECTORS AND MANAGEMENT FOR A SLOOPY PERFOMANCE AND MINCED NO WORDS CALLING FOR THEIR IMMEDIATE REMOVAL...
OF COURSE NOT MOST OF MY READRESWILL ACCEPT THE UNDONE DOCUMENTS "APOLOGY FOR SOMETHING SO SERIOUS LIKE THAT...IN BONGOLANDA DOCUMENTS HAVE NEVER BEEN A PROBLEM..IF YOU WANT TO PROOF FOR THIS LOOK NO FURTHER,EVIDENCE IS ALL OVER THE PLACE,REMEMBER THE DOCUMENTION THAT LED TO THE ""RICHMOND AND EPA" SAGA
"""THE BLAME IF AT ALL SHOULD GO TO THE DIRECTOR GENERAL OF TCAA.MARGRETH MUNYAGI..OURVERY OWN IRON LADY WHO BROOKS NO NONSENSE,IN THE SHORT RUN,YES SOMEPOWERS COULD BID FOR HER NECK,BUT IN LONG RUN,SHE IS NOTHING BUT A PURE HEROINE
IF HER DECISION IS BASED ON SERIOUS TECH REASONS..WHICH IS IMPLICIT IN THE RELEASEDLITERATURE,THEN WE ALL OWE HER A GLASS OF

""""" CHAMPAGNE"""
ON OTHR HAND ATCL CRISIS PRESENTS IS YET ANOTHER OPPOTUNITY FOR THE PUBLIC TO DECIDE WHETHER IT SHOULD BE RESUSCITATED AND FLOATED BACK TO SKIES,WITHOUT DICHOTOMIZING ITS CHRONIC OPERATION ILLS,
GOVERNENT ,AS USUAL IS MORE THAN WILLING TO SEE IT FLYING TOMORROW,BUT WHY THE HASTE WHEN WE HAVE NOT CHECKED THE EFFICACY OF ITS WINGS???
IF TANZANIANS ARE SERIOUS THIS TIME ARROUND ABOUT COMMISSIONING A VIABLE AND SUSTANABLE AIRLINE,THEY NEED TO DO A LITTLEHOMEWORK BEFORE THEY PROCEED ,THEY NEED TO REALIZE THAT ATCLAS PARASTATAL PER SE HAS BEEN LIVING ON BORROWED TIME..
TH ATCL IS NOW GASPINGTERMINALLY IN THE INTENSIVE CARE UNIT ,AND SOON MAY REST IN PEACE...
 
Sweetbaby na Mwanaizaya,
Makala zenu nzuri ila kuandika kwa herufi kubwa (shouting) kwa kweli kumenifanya nishindwe kusoma au kuruka mistari ili niwahi. Endeleeni kumkoma nyani ..........
 
ATCL staff still go penniless
STAFF REPORTER
Daily News; Monday,December 29, 2008 @21:15

Over 300 workers of the bankrupt Air Tanzania Company Ltd (ATCL) celebrated Christmas penniless last week and they clock in for work today demanding overdue December salaries amounting to some 400m/-. The pay demands include salaries and flying crew allowances.

Paschal Norbert, the branch chairman of the Communications and Transport Workers Union of Tanzania (COTWU), told the 'Daily News' that the ATCL workers were now worrying over their New Year pay, saying they are “facing terrible circumstances,” as the ATCL management keeps mum on the issue.

Our team was yesterday told that the management was attending “a very important meeting” and that nobody was available to comment on the workers’ claims. Mr Norbert said all the contributions to the statutory pension funds, workers unions as well as Savings and Credits Co-operative Society (SACCOS) had also ceased indefinitely.

Operations at the national carrier head office had almost stopped – following confiscation of its five vehicles that were bought in May last year on a loan from Stanbic Bank, until the 400m/- loan was paid to the bank. The COTWU boss told the 'Daily News' that the loan had been outstanding since April last year, although it was not immediately clear what the loan conditions were, but the bank was apparently worried that the customer might not pay up.

The five vehicles now held by the bank include Toyota Land Cruisers - SU 37079, SU 37081, SU 37082, SU 37083 and 37084 which were bought from Dubai - and another three vehicles. But the only working vehicle is the Toyota Land Cruiser SU 37085 which is used by the Chief Executive Officer, Mr David Mattaka. On December 10, 2008, the Tanzania Civil Aviation Authority revoked the ATCL licence, but the Minister of Infrastructure Development, Dr Shukuru Kawambwa, summoned the ATCL board and gave it seven days to explain why the airline was in such bad shape.
 
Mali za ATCL zakamatwa
Gloria Tesha
Daily News; Monday,December 29, 2008 @21:15

Benki ya Stanbic Tanzania Limited, Makao Makuu ya Kinondoni, Dar es Salaam, inayashikilia magari sita ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), baada ya kushindwa kulipa deni la Sh bilioni mbili iliyochukua kama mkopo.

Fedha hizo zinazodaiwa kushindwa kulipwa kwa miezi miwili sasa zilikopwa na wafanyakazi wa kampuni kwa mikopo na kutokana na kushindwa kuwalipa mishahara watumishi wake, makato ya kila mwezi yameshindikana kukatwa.

Taarifa zilizopatikana kutoka ATCL na katika benki hiyo jana zilithibitisha kushikiliwa kwa magari matano aina ya Toyota Land Cruiser VX, kuanzia Jumanne jioni wiki iliyopita na gari la sita limekamatwa likiwa mjini Moshi, Kilimanjaro na lilipelekwa katika benki hiyo jana na kufanya idadi ya magari hayo kuwa sita.

Namba za magari hayo ambazo ‘HabariLeo' jana ilizipata katika eneo la chini la maegesho yalikohifadhiwa magari hayo japo uongozi wa benki uliokuwapo haukuwa tayari kuzungumza kwa madai kuwa msemaji yupo likizo, ni SU 37079, SU 37081, SU 37082, SU 37086, SU 37083 na lililofikishwa jana ni SU 37084.

Habari zaidi kutoka eneo la benki yalikohifadhiwa magari hayo zilieleza jana kuwa yataendelea kushikiliwa mpaka deni hilo lililipwe na uamuzi huo ulifikiwa baada ya hofu kuwa huenda kampuni hiyo ikafa na hivyo benki hiyo ikakosa kila kitu.

Gazeti hili lilifika makao makuu ya Stanbic makutano ya barabara za Ali Hassan Mwinyi na Kinondoni, na mhudumu wa mapokezi alieleza kuwa wasemaji waliokuwapo hawakuwa tayari kulizungumzia, na mwenye dhamana ya kutoa taarifa hiyo ni Mkurugenzi Mkuu, Bashir Awale, yuko likizo.

Hata hivyo, taarifa za ndani ya benki hiyo zililieleza gazeti hili kuwa deni wanaloidai ATCL ni Sh bilioni mbili kwa mwezi huu na kwamba uamuzi wa haraka ulichukuliwa baada ya akaunti ya kampuni hiyo kwa benki hiyo kuonyesha haina fedha za kulipa deni hilo wala haitarajii kuwa nazo kwa siku za karibuni.

Chanzo chetu cha habari ndani ya ATCL kilieleza kuwa magari hayo yalikamatwa tangu wiki iliyopita isipokuwa la Mkurugenzi Mtendaji ATCL, David Mattaka. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ATCL, Balozi Mustafa Nyang'anyi, alithibitisha jana kupata taarifa ya kukamatwa kwa magari hayo na ameitisha kikao cha dharura kitakachokaa leo makao makuu ya kampuni hiyo.

Alisema pamoja na suala hilo, pia watajadili mambo mengine likiwamo la kurejeshewa leseni ya kurusha ndege waliyonyang'anywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Desemba 8, mwaka huu.

ATCL ilinyan'ganywa leseni hiyo baada ya kubainika kuwa na dosari za kiufundi zinazosababisha kutokuwa na viwango stahili vya kiusalama vya kuwaruhusu kurusha ndege; ukaguzi uliowataka warekebishe dosari hizo ulifanywa Oktoba mwaka jana na leseni hiyo iliisha kazi tangu Aprili mwaka huu, lakini walikuwa wakiongezewa muda mpaka iliposhindikana wakanyang'anywa leseni hiyo.

"Hilo jambo na mimi nimepewa taarifa, lakini kusema ni kiasi gani au ni deni linahusu nini, mimi siyo menejimenti, mpigie Mattaka, ila ninachoweza kusema ni kwamba deni hilo si kitu cha ajabu maana tulikabidhiwa kampuni na deni la shilingi bilioni kumi na tisa," alisema Balozi Nyang'anyi na kuongeza: "Ufafanuzi zaidi sina.

Mnashangaa hilo, kuna na la BP, pia waliokuwa wanatusambazia chakula kwenye ndege… na mengine mengi, yote hayo tutayajadili kesho katika kikao cha dharura na menejimenti nilichokiitisha, tutazungumza hayo na mengine mengi."


Alisema katika kikao hicho pia watazungumzia mishahara ya wafanyakazi ambayo mpaka jana walikuwa hawajapata na pia kupanga namna ya kurudi tena katika uzalishaji mara watakaporejeshewa leseni ya kurusha ndege tena.

Mattaka alipoulizwa jana kuhusu kushikiliwa kwa magari, alikanusha kwa kudai taarifa hizo si za kweli, lakini alikiri kuwapo kwa kikao cha Bodi na Menejimenti alichokiita kuwa ni kikao cha kawaida si cha dharura. "Hizo habari umetoa wapi? Si kweli, nasema si kweli?" alisema huku mwandishi akiendelea kumhoji.

"Kuhusu kikao ni kweli kipo, lakini si cha dharura, ni cha kawaida……naomba unitafute kesho baada ya kikao kuhusu hilo unalotaka kujua," alisema Mattaka. Hivi sasa TCAA inaendelea kupitia nyaraka za ATCL na kuna taarifa kuwa leo wanaenda kukagua namna ya wafanyakazi wa kitengo cha dharura ndani ya ndege wanavyoweza kuchukua hatua pindi tatizo linapotokea.
 
Hii ndio Danganyika,watu hawajari ni ubinafsi mtupu unaoendelea ebu be in the shoes of someone who is left pennilesss hasa kipindi hiki cha sikukuu yaani utamwonea huruma.
Mbaya zaidi watoto hawakuelewi kabsaaa.
Poleni ndugu zangu naona sasa mtetezi wetu ni MOLA tuu ndo aliyebaki
 
TCAA yairejeshea leseni ATCL, lakini hawana fedha za kuanza kurusha ndege, kazi iko!!

ATCL taabani
Tesha
Daily News; Tuesday,December 30, 2008 @21:15

Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) imeirejeshea leseni ya kurusha ndege Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) jana lakini uongozi wa kampuni hiyo umesema hauwezi kurusha ndege kutokana na kutokuwa na mtaji.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Margaret Munyagi alisema jana kuwa cheti cha kuonyesha kukidhi viwango walivyotakiwa kimesainiwa jana mchana na tayari ATCL wanaweza kuanza kurusha ndege leo.

“Sisi tumemaliza sehemu yetu, asubuhi tulienda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kukagua kitengo cha kukabiliana na dharura katika ndege za ATCL na baadae tulisaini cheti cha kuonyesha wamekidhi viwango na sasa leseni yao wamerejeshewa,” alisema Munyagi.

Munyagi alisema kampuni hiyo pamoja na mambo mengine imeweza kukidhi matakwa ya viwango vya kiufundi, kitengo cha kukabiliana na tatizo linapotokea, usahihi wa nyaraka za marubani, vipuri vya ndege vyote vikithibitisha usalama wa ndege kuwa angani hivyo kazi kwao kurudi katika uzalishaji.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ATCL, Balozi Mustafa Nyang’anyi alisema jana kuwa pamoja na kurejeshewa leseni, ndege za kampuni hiyo haziwezi kuruka kutokana na kukosa mtaji na kuongeza kuwa mtaji walioomba serikalini tangu mwaka jana wa Sh bilioni 91.2 hawajapata.

“Hata tupewe leseni leo (jana), hatuna uwezo wa kurusha ndege kwa kuwa hatuna mtaji wowote, tunamsubiri mwenye mali ambaye ni serikali atupe mtaji ili tuweze kuona namna tutakavyoanza safari,” alisema Balozi Nyang’anyi.

Wiki tatu zilizopita TCAA iliinyang’anya ATCL leseni ya kurusha ndege baada ya kuonekana ina dosari za kiufundi zinazosababisha kutokidhi viwango vya kiusalama vya kurusha ndege na hivyo kuchukua uamuzi wa kukagua nyaraka za kampuni hiyo kwa kipindi hicho.

Balozi Nyang’anyi ambaye hakuonyesha kuthibitisha moja kwa moja taarifa za kurejeshewa leseni hiyo, alisema naye alipata taarifa jana mchana kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TACC, Munyagi kuhusu kurejeshewa leseni hiyo na kumtaka mwandishi kupata taarifa zaidi kwa Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, David Mattaka.

Mattaka hakupatikana kuzungumzia suala hilo baada ya gazeti hili kufika ofisini kwake na kuelezwa kuwa yupo katika kikao siku nzima jana na alipotafutwa katika simu ya mkononi, iliita bila majibu.

Kabla ya taarifa za kurejeshewa leseni Balozi Nyang’anyi aliliambia gazeti hili jana kwa njia ya simu kuwa itachukua muda kwa ATCL kuanza safari kwani hivi sasa wanashughulikia mtaji wa kuwezesha hilo kufanyika na serikali haijasema lini fedha zitapatikana.

Nyang’anyi alisema kutokana na matatizo lukuki yanayoikabili kampuni hiyo, bodi pamoja na menejimenti wataendelea na kikao leo kujadili mambo matatu ikiwamo mishahara ya wafanyakazi, namna ya kurusha ndege na kuendelea kufuatilia mtaji serikalini.

Alisema deni la Sh bilioni 19 walilolipokea baada ya kufa mkataba kati ya Serikali na Shirika la Ndege la Afrika Kusini, bado linaendelea kuifanya kampuni hiyo ishindwe kujiendesha pamoja na kushindwa kulipa mishahara ya watumishi ya zaidi ya Sh milioni 400 inayodaiwa.

Kuhusu deni la Sh bilioni mbili linalodaiwa na benki ya Stanbic Tanzania Limited, alisema katika kikao cha jana, menejimenti iliieleza bodi kuwa inadaiwa na benki hiyo Sh milioni 40 na si bilioni mbili lakini taarifa za benki hiyo za jana na juzi zilidai kuwa mkopo wa ATCL ni Sh bilioni mbili na ndiyo sababu ya kuyashikilia magari sita ya kampuni hiyo aina ya Land Cruser VX mpaka deni litakapolipwa.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo alisema bodi imeiagiza menejimenti kufuatilia deni hilo pamoja na kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanalipwa mishahara mapema iwezekanavyo. Mpaka jana mishahara ya wafanyakazi hao haikuwa tayari.

Wiki iliyopita akihojiwa na gazeti hili, Balozi Nyang’anyi alisema mtaji wa Sh bilioni 91.2 sawa na dola za Marekani milioni 76 walizoiomba serikali mwaka jana zilikuwa zitumike pia katika kuandaa kitaalamu nyaraka za ndege mpya ambazo ukaguzi wake unafanyika Afrika Kusini na Kenya ambazo ni Air Bus 320 (ya kukodi), Dash 8 mbili ambazo ni Bombadia Q 300 zilizonunuliwa na serikali lakini hilo halikufanyika.

Hata hivyo hivi karibuni, Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu ilipeleka wataalamu wa TCAA nchini Kenya na Afrika Kusini kufanya ukaguzi katika karakana zinazotumika kukagua ndege hizo ili kujiridhisha, ikiwa ni utekelezaji wa hatua za serikali kulinusuru shirika hilo zilizoelezwa kuanzwa na Waziri mwenye dhamana, Dk. Shukuru Kawambwa.

Huko wizarani jana, Waziri Kawambwa hakupatikana kuzungumzia hili baada ya taarifa za ofisi yake kusema kuwa yupo safarini lakini Ofisa Habari wa Wizara, Issa Mbura alisema siku chache zijazo wizara itatoa taarifa njema kupitia vyombo vya habari kuhusu hatima ya ATCL.
 
Habari ndiyo hii!!


Daily News 31 Dec.08 imeandika kuwa TCAA imeirudishia ATCL licence to fly na hivyo itaanza kuruka sasa. Lakini cha kushangaza ni kuwa - IATA bado imeifungia ATCL na haitaifungulia mpaka warekebishe mambo yao, hasa ya kiusalama wa anga na abiria.

TCAA imepewa pressure na serikari na vigogo wake mpaka imekubali kuwafungulia leseni bila kujali kuendelea kufungiwa na IATA na bila kujali kuwa ndege za ATCL hazina service ya kuaminika kutokana na ukata. Maamuzi hayo ni ya kusikitisha na kutojali usalama wa watanzania.

Kufungiwa na IATA kuna maana ndege za ATCL zisiruke na kama nchi italeta ubishi basi inaweza kuruka nchini mwao tu, kwani nchi nyingine hawataruhusu ndege za ATCL kuingia anga zao huko kwani zinaweza kuleta ajali. Pia ndege za mataifa mengine zinapoingia anga yetu huwa na wasiwasi sana kwani huenda wakakutana na ndege mbovu na sisizofuata taratibu za kimataifa huko angani na kusababisha hatari huko juu.

Hatua ya TCAA ni kuonyesha ukaidi wa Serikali yetu na itaweza kuleta madhara kwa raia.
Ni Bora TCAA ifanye kazi zake kwa - ki-professional and kuwa independence. Wasikubali pressure za kisiasa.

Jambo ya pili ni hatua ya Bodi ya ATCL kuwakodisha maconsultant wa Price Water Coopers kwa fedha nyingi sana. Kampuni kama TAC Associates au Kampuni ya Tija ya Taifa ingekuwa ya nafuu sana kulinganisha na Price WaterCoopers

Pia:

ATCL haikuitisha zabuni ya kazi hiyo waliyopewa Price Water Coopers, Rushwa imetembea kutokana na urafiki wa Partner Mndolwa za Price Coopers na Mr. Nyanganyi na Mataka
Hii pia ni kinyume cha taratibu za Public Procurement regulatory Authoryt - Dr. Angalia hapo

Kampuni ya Price Water Coopers pia ni wakaguzi wa mahesabu wa ATCL. Hivyo kwa taaluma yao huirihusu wao kujiingiza katika kazi za manajimenti ya kampuni. Wakaguzi huru kuruhusiwa kuwa Management Consultant kwa kampuni wanayoikagua ni kunyume cha professional ethics zao na pia kunawasababishiwa kukosa independence - Bodi ya wakaguzi iliyolala, na inayoongozwa na maPartners hao wa PriceCoopers wanatakiwa kukemea hili

Ukaguzi wa ATCL kwa kutumia Price Coopers Waters imegharimu zaidi ya millioni harobaini wakati TAC Associates walikuwa wanakagua kwa shillion million zisizozidi kumi

PriceCoopers imepeleka wafanyakazi ATCL akiongozwa na Mkuu wa idara ya fedha, mkuu wa ukaguzi ndani, hivyo hawa watendaji wakuu wamekuwa kwa muda mrefu wanapeleka kazi kwa mwajiri wao wa zamani. Hou ni Eliasaf Methew, William Haji (kaondoka) na dada wa kichaga binti Lyimo wa Kimara.

Kuna rushwa tupu inanuka ATCL katika mambo ya procurement.
 
Haya tena politiks kwenye utendaji...kazi kweli...nini tufanye kama abiria???naomba msaada wa mawazo.....maana kama wamefanya kisiasa...na kulindana....tutakaokuwa victims ni sisi kina kalagabhahoo.....
 
Back
Top Bottom