Serikali na Hatima ya ATCL

Hapa ndipo ninapoishiwa nguvu. Kweli tumeji-convince matatizo ya Air Total Confusion yalianza na SAA? Shirika lilikuwa haliuziki ndiyo maana tukaaungikia SAA. Yeyote aliyewahi kusafiri na hilo shirika kabla ya SAA atashangaa ni hali nzuri gani aliyokuwa akiizungumzia Nyanganyi! Hili shirika lilikuwa mahututi tayari, SAA walilisindikiza tu kaburini na kutuachia kazi ya kulifukia!
 
Kwa kweli nimepokea habari za kusitishwa huduma za Air Tanzania (ATCL) kwa masikitiko makubwa kabisa. Kwa muda mrefu hapa ndani ya JF tumekuwa tukujitahidi kutoa tahadhari juu ya mwenendo mzima wa uendeshaji wa Kampuni hii kwa lengo moja tu, nalo ni kuwafanya wadau wanahusika na ATCL watupie macho na kuinusuru. Kelele nyingi zilipigwa na hata kufikia baadhi miongoni mwetu kukata tamaa kutokana na kutokuonekana kwa any positive move toward solving the Air Tanzania core problem.

Tulijitahidi kueleza wasiwasi tuliokuwa nao juu ya team inayoongoza ATCL, ama hakika inatia simanzi...hivi kweli Shughuli za Kampuni kama ATCL zinasitishwa eti kwa kukosa kuweka nyaraka katika mpangilio? Kana kwamba kushangaa huku hakutoshi...eti waliambiwa waziweke kwenye mpangilio tangu december 2007? tunadanganyana? si kweli...

Nionavyo mimi ni kuwa serikali imechelewa kufanyia kazi hali mbaya ya uongozi wa ATCL na serikali inahusika moja kwa moja na usitishwaji wa shughuli za ATCL. Usitishwaji huu unafanywa kama njia ya ku-deal na uongozi mbovu lakini katika gharama ya wafanyakazi ambao they are not part of failed management team.

Ninashauri kuwa serikali iwe wazi juu ya suala hili ili kuepusha mgogoro usio wa lazima baina yake na wafanyakazi. Ikumbukwe kwamba wakati serikali ilipounda Air Tanzania Co. Ltd. (ATCL) baada ya kusitisha shughuli za Air Tanzania Corporation (ATC), wafanyakazi bila ya ridhaa yao walipelekwa kwa mwajiri mpya ambaye hawakuwa na makubaliano ya aina yeyote. Matokeo yake mwajiri mpya bila ya kujali muda wa utumishi wa wafanyakazi hao na bila ya kujali stahili zao walizokuwa wakizipata kwa mwajiri wa zamani, aliamua kufanya vile alivyotaka na bila ya serikali kuingilia kati hatimaye wengi wa wafanyakazi wa ATCL walioingizwa toka ATC wamepoteza maslahi yao na baadhi wakafukuzwa bila kujali historia ya maslahi yao. Nadhani katika historia ya ATCL kitendo kilichofanyika katika kipindi hicho ninadiriki kusema kilikuwa ni kitendo cha kiukandamizaji na uonevu. Hata wale ambao walistaafu hawa walifanya hivyo huku wakinung'unika lakini serikali ilibariki vitendo vyote viovu vilivyofanyika.

Sasa ninachotaka kushauri kwa wafanyakazi ni kuwa:
Ni ukweli usiopingika kuwa kurudi kwa ATCL hewani kutategemea serikali kuweka fedha za kuanza kufanya kampuni irushe ndege zake tena, lakini jambo hili kila nikijaribu kuliangalia kwa makini sana sioni kama serikali iko tayari kufanya hivyo, aidha serikali huenda itarudi na version nyingine ya Air Tanzania ya kichina ambayo wafanyakazi wanaweza wakajikuta wanatumbukizwa tena katika matatizo kama yaliyojitokeza wakati wana hamishwa kwa mwajiri mpya ATCL. Kwa mantiki hiyo basi, serikali ikutane haraka na viongozi wa wafanyakazi wa ATCL ili waweze kuambiana ukweli wa mambo na kuona ni jinsi gani wafanyakazi watapatiwa mafao yao ili wasijikute tena wanaingia katika mkumbo ule ule wa wafanyakazi wa jumuiya ya Afrika Mashariki au walimu.

Ni vema serikali ikawa wazi sasa kulikoni kuja kuwasumbua wafanyakazi ambao kwa muda mrefu walisimama imara kuhakikisha Air Tanzania inakuwepo katika vipindi vigumu vya uongozi usiokuwa makini.
 
Nimesoma gazeti la leo likanikumbusha mbali sana kuna maswali nilikuwa naulizwa nikiwa darasa la tano na saba majibu ni....MUSTAPHA NYANGANYI
leo hii kwa bahati mbaya naskitika kupingana na yule yule mabae kwa wakti huo niliona bila kujaza jina lake ningefeli masomo darasani na si mwingine
.M.NYANGANYI
Ndugu zangu napenda kumshauri mzee wangu wa muda mrefu kwa kweli siku alipoteuliwa kuongoza nilimsikitikia sana maana nilijua ipo siku atakuwa wa kwanza kumwambia rais sasa basi kadri ya heshima na uadilifu alio nao..huwa akiona mambo kombo achoki kuachana nayo..leo hii nimesoma gazeti la mwananchi akisema kama bodi itaonekana imehusika basi ajiuzulu..Bila jazba ningependa kumwambia mzee wangu nyangangyi muda umefika sasa wa kusema basi...am going kabla ya wafanyakazi kuanza kuropoka...sijui nini kinaendelea uko tanzania lakini nimekuwa nikipata uchafu mwingi unaofanyika huko kutoka kwa ndugu yangu mmoja ambae alikuwa huko zaidi ya miaka 20
Swali langu namuuliza Mh nyanganyi kwa haya chini kwanini usiachie ngazi kiustaarabu

NO.1
MAHUJAJI
Nafikiri mpaka sasa anajua nini kilichotokea kwa mahujaji kuwafedhehesha pale airport kama yatima...katika kuchunguza tuliona raia mwema wakituinyesha barua mbalimbali za baadhi ya viongozi wakikana kuhusika kwao na mwisho kuweka wazi barua aliondika mh nyanganyi kusema atachukua jukumu kuwapeleka kama management wameshindwa..nyanganyi unakumbuka
managemente waliandika kwamba katika mchakato mzima na bei mliotaka kuleta ambayo katika uchunguzi tulikuta mahjujaji wametoa bei tofauti na nyie mkapeleka bei tofauti ATCL..Ndio maana wataalamu wakakutalia kwa kusema ni hasara ya mwaka na hawawezi hiyo biashara....je kulikuwa na nini??ndani mh???

BILLION 1...iliotolewa na serikali kuhakikisha mnawapeleka mahujaji hata kama wamechelewa matokeo yake mkaunda kamati ambayo mlikuwa kila siku nasikia mkigawana lakitatu mpaka mahujaji wakaisha wote..ulikuwa hujui pesa za wananchi walipa kodi mmoja wapo aliwepo mwanao???

PILI
(UJIO WA AIRBUS)
Wakati ndege ikiletwa ulikuwa ukijua matatizo yake na ukaombwa kusimamisha uletaji wa ndege hiyo na kuletewa ushahidi hiyo ndege si nzuri na iweje mkalipa doller 360,000 wakati min kwa soko la wakati huo kimataifa ni 260,000 na ukaletewa na baadhi ya sehemu ambazo mngeweza kukoidsha kwa bei nafuu na kupata afadhali ya trainning bure laikini mkakimbilia kwenye 360,000 ,,,mkiambiwa mmetafuna pesa za wananchi bodi yako itakataa hili???

......Wakati ndege ikisubriwa kuja kuna watu walienda kukaa kule zaidi ya miezi sita na mkiwalipa doller 400 kwa siku..mh nyanganyi unalijua hili mpaka mwingine ikabidi nasikia aje kwa ukulazimishwa na bodi yako......
je 400*30*6=72,000usd kwa mtu mmoja mlikuwa hamjui ipo siku mtakosa pesa za mafuta,wakati ndege ikiletwa kulikuwa na matatizo mengi ikalazimu kuita kampuni ya mauritius ufanya aintanance na sijuikama kweli mnailipa 200usd kwa mwezi mlio bongo tujulisheni.....

MARUBANI WA AIRBUS****
Mlipoileta mkaamua kuleta marubani wa kukodisha ,ambao nasikia wametofautiana na baadhi ya watu kuhusu ten pers wameletwa wengine
tena...sasa labda nikuabalishe mh NYANGANYI Kwa hili usipojiuzulu basi utajiuzulu maisha...una taarifa hawa matubani mliowaajiri mnawalipa euro 16,000 na kuna kila mmoja kwa kila masaa 300..na katika hili kuna mtu anachukua euro 3000 kutoka kila mtu kama ahasante????????????
Pili unajua hii kampuni EASYWAY inawaleta hao marubani kama kuja kufanya traiinning kwenye airbus ya AIRTANZANIA inayopakia abiria wenye hekima zao..je uoni hatari uajiri marubani frdsh kutoka shule gafla waje kufanya trainning kwenye ndege za abiria!!!na kuchea na roho za watu is it fair??
 
AJIRA MBOVU

swala la ajira nahisi si la kuongelea sana maana hata wewe umehusika kuna baadhi ya watu walikuja kwako ukawaelekeza waende kumuona dav na hivi sasa wamejazana matokeo yake ..umejaza watu ambao si qualified kwa minajili ya kujuana na uswahiba...mwisho unafikia kulalamika hmna pesa za mafuta is this fair kweli???wakati mkiwaajiri hamkuwa mnajua kwamba ipo siku wanaitaji mishahara mwisho wa mwezi...matokeo yake mnaendelea kuajiri watu kwa kuwahonga mapenzi na mwisho kuaribu furure ya watoto wadogo hapo..mfano kuna binto ameolewa hivi karibuni habari zakusikitsha ameajiri muda si mrefu na kudanganywa kwa mapenzi na mmoja wa mameneja matokeo yake akapitiwa mpaka na kurugenzi..nafikiri inaitajika hekima ya hali ya juuu hapo tanzania..

MIKOPO
Mmekuwa mkikopeshana pesa za kampuni bila kujua ipo siku mtaishiwa na kuaminiATCL Ni kisima cha hela..kuna wakurugenzi wako wengi tu wanadaiwa na kampuni kuanzia 10million mpaka 25million,,naomba kuuliza hujui kuna sheria za mashirika mkopo wa kampuni unaruhusiwa iwapo mhusika ataweza kulipa ndani ya miezi 6????je million 15 wanalipaje ndani ya miezi 6..na hili unalijua mh nyanganyi kabla ujaletewa ushahidi????

SAFARI
KUMEKUWA NA SAFARI ZA MARA KWA MARA AMBAZO ZIMEIGHARIMU KAMPUNI ZAIDI YA MILLION 72 KWA MKURUGENZI MMOJA.BADO MILLION KAMA 115 KWA CEO WAKO KWA AJILI YA SAFARI AMBAZO MPAKA LEO HII NI WEWEE NDIWE ULIKUWA UNAJUA NA BODI YAKO ANAELEKEWA WAPI NA KIMAHESABU MWAKA MMOJANA NUSU WAMETUMIA MILLION 172 JE WAKIPEWA MIAKA MIWILI???MOLA WASAIDIE WAJA WAKO

ACTING ALLOWANCES

Kumekuwa na malipo ya ajabu ajabu yasiyo na maana ambayo yamepelekea kwa namna moja ama nyingine kutufikisha hapa tulipo..mfano CEO amekuwa nje ya nchi ama mkoa mara kwa mara na matokeo yake kukabidhi madaraka ,,mwisho wa siku mtu huyo huyo anapokea mshahara wake na act allowances...kwa mwezi mzima ATCL imekuwa ikitoa zaidi ya sh milion 15 kwa ajili ya act allowances za watu mbalimbali!!!je kama mw wa BODI ulikuwa ujui ,na kama ulijua kwanini usiwajibike kama mstaarabu tukujuavyo???

MALIPO YA BODI}+KUTOLIPWA MISHAHARA WAFANYAKAZI
Mh mwenyekiti.kidogo bado kichwa kinauma kwa nini usingoke....BODI yako nasikia mmekuwa mkilipana kwa doller nyingi tu kwa masaa machache
la hasha swala si kulipana doller 5500 kwamasaa 2..swala je kutolipwa wafanyakazi wakomishahara na wewe kukaa kimya huoni hili swala ni muhimu zaidi,,,huoni kama si wafanyakzai wewe usingekuwapo kwenye BODI..IWEJE unadiriki kuchukua usd 5500 kulipana kwa masaa machache wakati kuna watu zaidi 50 hawajalipwa mishahara yao...na mwisho inasemekana wengine kuamua kuresign ....je kwa hili kun uhalali wa kuendelea na BODI YAKO???

TRAIINING YA MARUBANI
Mh mwenyekiti.kama ninavyouliza na nilivyouliza mwanzoni.. hii ndege yenu mmeileta ina mwaka sasa lakini muda wote hamko wala kufikiria kuwapeleka marubani kwenye trainning matokeo yake mnaendelea kuwaleta marubani wa nje na kuwalipa pesa nyingi kisa mnakula ten perc..hamwonei kampuni huruma kweli.hata kama hii swala ni la management mikataba yao lazima iletewa kwenu kwenye bodi ,,mmekaa kimya mnakimbizana na kulpa watu euro huku zingine mkijua zinaenda wapi!!!matokeo yake mnashindwa hata kulipa hoteli wanazokaa na kutia aibu kampuni!!!!kwa nini mnangangania marubani wanje??
y????????????????????????????????????????????????? ????????????????
kuna nini huko!!!tunaomba serikali kama imedhamiria kuliona shirika likisimama wapeleke wazawa trainning badala ya kuishia kuwalipa wazungu pesa na kuwalipia hotelini doller 150 kwa siku kwa mtu mmoja..je kuna haja ya kuwa na BODI mhe mwenyekiti????
 
KULETA MARUBANI WASIO NA RATES
ndugu mwenyekiti..kumekuwa na malalamiko ya ajabu ajabu huko kwenye kampuni yako!!!kuhusu hawa marubani wa kizungu mnaowaleta..labda kwa taarifa yako tu kuna kampuni inaitwa easyway...kampuni hii imekuwa ikiwafanyia trainning wanafunzi wanaotoka fresh from school na baadae kuwapeleka kwenye mashirika kufanya trainning..kwa bahati mbaya shirika lako limekubwa na style hii kuwachukua watu kuja kufanya traiining na hivyo kutishia maisha ya watu!!1je huoni si haki kucheza na roho za watu kama managemente yako inavyoona na kama umeliona hili je kuna haja ya kuwa na
BODI YAKO???mhe mwenykiti!!

UBADHIRIFU WA MAGARI
nafikiri hata majuzi tulikuwa hapa washington tukzungumzia sana huo uuhuni miliwafanyia wafanyakazi kwa kuwaleteta ma lexus ya bei mkijua mtwadanganya kwa wizi mlioutenda..mh mwenyekiti kwa ruhusa ya bodi yako management ilichukua zaidi ya million 290usd kwa ajili ya kuleta magari ..wengi walijua magari yanakuja na hivyo kupunguza matatizo ya wafanyakazi....matokeo yake managemente yako wakiongozwa na DM-walienda kule wakanunua magari mabovu kwa bei ya chini na walipoyaleta wakaonyesha pesa tofauti na bei walionunulia..na hivyo kushindwa ulipia kodi..mpaka sasa nasikia ni magari 5 tu ndio yaliyotolewz kati ya 21.....habari zaidi zinasema hayo magaro yapo kwenye YADI ya mmoja wa maswahiba wa DM..NA WEWE UKJUA HILI WANALIPA ZAIDI YA USD 3500 KWA MWEZI TENA ON TYME HUKU WATU HAWALIPWI MISHAHARA YAO JE KUNA UMUHIMU WA KUENDELEA NA BODI YAKO MH MWENYEKITI!!!!

KWA HAYO MACHACHE BADO MUDA UNAO KUTANGAZA LINI UMECHOKA ULIWEZI TENA ESP WAKATI HUU KAMPUNI HAINA HELA............
 
--------------------------------------------------------------------------------

Je hayo magari yatatolewa lini??na aliehusika kuyaleta na kushindwakuyatoa aliwajibika???
kuna fununu kuna baadhi ya waliohusika katika kuleta magari haya ama kwa kwenda kuyaangalia ama kusaini kati ya moja ya makaratasi...swala hili liko mikononi mwa takukuru na baada ya kuona hilo wameongezewa mshara hawana hata miezi 3
kutoka laki 480 mpaka 700..na wa laki saba mpaka 950,,unajua hili.kama ndio unaonaje kwa uadilifu wako uwe wa kwanza kuwaambia wafanyakazi ahasanteni kwa yote milyonitendea nasikitika nilikuwa najua niko na watu watakaoisimamisha kampuni matokeo yake ndio haya...na mwisho kuwajulisha
 
mimi bado nawashangaa hawa ndugu zetu wa TCAA...how come rubani anatoka shulen ana masaa 250 tu anakuja moja kwa moja kurusha ndeege yenye abiria 150...je mnalijua
hili endapo PILOT AKIZIDIWA hamna kitu tena...tunaokota ..........*****
???
 
Tuhuma za wafanyakazi atcl zifanyiwe kazi haraka sana

--------------------------------------------------------------------------------

Tuhuma za wafanyakazi ATCL zifanyiwe kazi haraka
Basil Msongo
Daily News; Sunday,December 14, 2008 @09:42

Najivunia kuwa Mtanzania, naipenda nchi yangu, wakati wowote nipo tayari kuitetea sifa ya nchi hii na kamwe sitamuonea haya ye yote aliye kikwazo cha maendeleo ya Tanzania aidha kwa kufahamu au kutofahamu, kwa kutumiwa au kwa maslahi yake binafsi.

Ni kutokana na mtazamo huo, nadiriki kusema kwamba yanayotokea sasa katika Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) yanasikitisha na ni aibu, hivyo serikali inapaswa kuchukua hatua haraka ikiwa ni pamoja na kuzifanyia kazi tuhuma za wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Kauli za wafanyakazi hao zimenifurahisha, si kwamba nimethibitisha kuwa ni za kweli, ni kwa sababu wamesema wanachoamini, wameeleza hisia zao na kutoa msimamo, nashawishika kuamini kuwa waliyasema hayo kwa kuongozwa na uzalendo na si chuki binafsi, aidha kwa Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, David Mattaka au viongozi wengine.

Naamini kuwa serikali imeelewa, tatizo ATCL si upungufu wa ndege au ukosefu wa fedha tu, wafanyakazi hawana imani na utawala ulio chini ya Mattaka na Bodi ya Wakurugenzi inayoongozwa na Balozi Mustafa Nyang’anyi.

Kuna mambo ya msingi yanayostahili kufanyiwa kazi haraka, hayahitaji uchunguzi au utafiti, hayahitaji mwongozo wa sera au fedha za kigeni, mfano, kurudisha uhusiano mzuri kati ya menejimenti na wafanyakazi.

Hata kama ATCL itakidhi masharti ya usalama, hata kama ndege zake zote zitakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa asilimia 100, ni ndoto kwa kampuni hiyo kupata mafanikio kama hakuna uhusiano mzuri kati ya utawala na wafanyakazi.

Sina mamlaka ya kusema tuhuma za wafanyakazi wa ATCL ni za kweli au la, lakini nina wajibu wa kuiomba serikali isizipuuze, ufanywe uchunguzi ili kufahamu tatizo ni nini na nani kasababisha. Busara itumike ufumbuzi upatikane haraka iwezekanavyo, Watanzania wana haki ya kujivunia alama hiyo ya Tanzania na si kusononeka.

Upendeleo, kujuana, huyu ni mwenzetu, na rushwa visiwe na nafasi katika mchakato wa kurudisha hadhi ya ATCL, ye yote anayeonekana kuwa ni kikwazo cha mafanikio katika kampuni hiyo awekwe kando kwani ni chombo cha Watanzania, fahari ya Watanzania, mali ya Watanzania na ipo kwa ajili yao, hivyo maslahi ya taifa yazingatiwe.

Ni kwa kuzingatia hilo, ikithibitika kuwa kuna udhaifu wa kiutendaji katika menejimenti, wahusika waondolewe haraka, jukumu hilo wakabidhiwe wenye uwezo wa kuiongoza ATCL kwa ufanisi, watakaoiwezesha kampuni kumudu ushindani kwa kibiashara katika usafiri wa anga ndani na nje ya Tanzania.

Sioni tatizo kumuondoa Mattaka katika uongozi wa kampuni hiyo kama ikithibitika kuwa yeye ni tatizo ATCL, na pia sitashangaa endapo Bodi ya Wakurugenzi itavunjwa kwa manufaa ya umma kama imeshindwa kusimamia menejimenti.

Ninaamini kuwa Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa; wapo makini kutafuta ufumbuzi wa matatizo ATCL, na sina shaka kuwa uamuzi wa serikali utakuwa wa haki na utazingatia maslahi ya taifa.

Kwa kuwa wafanyakazi wa ATCL wameonyesha nia ya kuandamana kwenda Ikulu, Waziri Kawambwa akazungumze nao, wapewe nafasi ya kusema waliyonayo, na awaeleze serikali inafanya nini ili kurudisha hadhi ya kampuni hiyo.
 
Kama ambavyo tumeeleza kwa kirefu kwenye kijarida cha cheche toleo la leo (angalia thread hapa) muda mfupi uliopita tumehakikishiwa kuwa hatimaye Shirika letu la ndege la ATCL limeondolewa kutoka katika ushirika wa vyombo vya safari za Anga IATA.

Vile vile vyanzo vya uhakika vimedokeza kuwa kufuatia taarifa yetu ya kina kuhusu jinsi ATCL ilivyotafunwa ambapo tumetaja majina (to the delight of our dedicated critics) ndani ya masaa 48 yajayo kuna mkutano muhimu utafanyika (wenu mtiifu nimedokezwa dondoo zake); mkutano huo unaweza kubadilisha ATCL katika siku chache zijazo.

"Kuna wakati mtu anaweza akavumilia uzembe akiamini mtu anaweza kurekebishwa na kueleweshwa; lakini inafikia mahali lazima tuzeme enough is enough" amesema afisa mmoja wa serikali ambaye tumempenyezea ushahidi wa ubadhirufu uliokubuhu wa ATCL!
 

Attachments

  • ATCIATAsuspension.pdf
    101.1 KB · Views: 128
Last edited by a moderator:
Afadhali yametokea haya. Hawa jamaa walikuwa wanaelekea kuua abiria wao! Kila mara nilipofikiri kusafiri kwa ATC tumbo lilikuwa linakoroma!! Mataka alisema hatajiuzulu. Tuone sasa!
 
Jemadari wetu JK ndugu Kikwete wa Chalinze karibu na Darisalama yupo ama yuko safarini ?
 
Mwanakijiji nakuomba mkuu, wiki ijayo usije ukasahau kudiscuss hili soo mpya la Ngeleja kutaka kununua Generator za dowans.

Hii ni criminal act on his part sababu PPRA inazungumzia suala la serikali kutoruhusiwa kununua used stuff. Sasa Rostam anasema hizo generator wao walinunua mpya, it might be true but by the time serikali inataka kununua kutoka kwao sip mpya tena.
 
mwanakijiji kweli unasoma nyakati!!!!sasa unafikiri tuwasaidieje hawa ndugu zetu nafikiri kuna kipindi jf ilijaa ATCL news na hakuna mabadiliko...
 
Kama ambavyo tumeeleza kwa kirefu kwenye kijarida cha cheche toleo la leo (angalia thread hapa) muda mfupi uliopita tumehakikishiwa kuwa hatimaye Shirika letu la ndege la ATCL limeondolewa kutoka katika ushirika wa vyombo vya safari za Anga IATA.

Vile vile vyanzo vya uhakika vimedokeza kuwa kufuatia taarifa yetu ya kina kuhusu jinsi ATCL ilivyotafunwa ambapo tumetaja majina (to the delight of our dedicated critics) ndani ya masaa 48 yajayo kuna mkutano muhimu utafanyika (wenu mtiifu nimedokezwa dondoo zake); mkutano huo unaweza kubadilisha ATCL katika siku chache zijazo.

"Kuna wakati mtu anaweza akavumilia uzembe akiamini mtu anaweza kurekebishwa na kueleweshwa; lakini inafikia mahali lazima tuzeme enough is enough" amesema afisa mmoja wa serikali ambaye tumempenyezea ushahidi wa ubadhirufu uliokubuhu wa ATCL!

...halafu bado Mustapha Myang'anyi anasema atajiuzulu pale tu ITAKAPODHIBITIKA kuwa bodi yake imehusika katika kufanya shirika hilo kufungiwa! Uthibitisho upitena?
 
halafu bado Mustapha Myang'anyi anasema atajiuzulu pale tu ITAKAPODHIBITIKA kuwa bodi yake imehusika katika kufanya shirika hilo kufungiwa! Uthibitisho upitena?

labda anasubiri kutupiwa mawe na watanzania ndipo ajue wamechoka nje ya hapo hatoki....majuzi nilikuwa naongea na dir mmoja na manager wake wanahusika kwenye hii kashfa anasema yeye atakuwa wa mwisho kuresign ..hata kwa bakora ataakikisha wote wameanza ndipo afwate yeye..nikasema kweli kazi ipo hapo..haya nawaachia watanzania wenyewe
 
...halafu bado Mustapha Myang'anyi anasema atajiuzulu pale tu ITAKAPODHIBITIKA kuwa bodi yake imehusika katika kufanya shirika hilo kufungiwa! Uthibitisho upitena?

Uthibitisho anaoutaka yeye ni upi?Its simple..Management goofed big time, the board failed to deal with them decisively and in a timely way.As a result ATCL has been grounded.No business means loss to the GOT.
 
Mwanakijiji nakuomba mkuu, wiki ijayo usije ukasahau kudiscuu hili soo mpya la Ngeleja kutaka kununua Generator za dowans.

Hii ni criminal act on his part sababu PPRA inazungumzia suala la serikali kutoruhusiwa kununua used stuff. Sasa Rostam anasema hizo generator wao walinunua mpya, it might be true but by the time serikali inataka kununua kutoka kwao sip mpya tena.


Moelex.. angalia kwenye Cheche la leo.. tumeshadokeza
 
Kuna mwandishi wa habari mwenye heshima inayodidimia (controversial) anaitwa Makwaia wa Kuhenga aliandika makala katika gazeti la Daily News miezi si mingi iliyopita. Nimesahau ni toleo gani. Alimsifu bwana David Mataka kwamba ameweza kuliletea ufanisi shirika la ATCL.

Najua huyu mwanahabari ni mwana CCM mkereketwa. Lakini uandishi wa aina hii unamporomosha yeye na vinavyomzunguka.
 
Back
Top Bottom