Serikali na CCM lazima wawe makini na hatari hii la sivyo.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali na CCM lazima wawe makini na hatari hii la sivyo....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mcfm40, Jul 17, 2012.

 1. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,142
  Likes Received: 1,779
  Trophy Points: 280
  Ndugu WanaJF,
  Kwa muda sasa nimeweza kuona kwamba kuna mambo ambayo serikali ya CCM imekuwa inayafanya ambayo yanaweza kuhatarisha amani ya nchi hii. Mambo hayo ni haya yafuatayo:

  Moja. Kudhibiti vyombo vya habari vya ili mara zote vihakikishe vinaipendelea seriakali na chama. Hili lilifanyika kwa kumtoa Tido na kuirudisha TBC kwenye enzi za TVT. Sasa hivi mambo ambayo TBC inafanya yanatia aibu! Wanatoa habari za upande mmoja bila kubalance na za upande mwingine! Si hivo wao pamoja na mgazeti umma yanatoa habari kwa kutia chumvi ili kupendelea upande wao na kuficha pale ambapo serikali pia inamakosa. Rejea swala la ulimboka na mgomo wa madaktari, swala la mauaji yaliyotokea Ndago, na habari nyingi za wapinzani zinabadilishwa ili waonekane wao ndio wana makosa. Kwa mfano Ndago, swala la wafuasi wa CCM kuanzisha vurugu halisemwi kabisa na walionzisha vurugu wala hawajakamatwa. Ikumbukwe kwamba hivi vyombo vya habari vya umma vinalipiwa kwa kodi za watanzania wote na tuna haki ya kupata unbiased news. Si ajabu TBC na mgazeti mengi ya umma siku hizi yamesusiwa na watanzania. Ikumbukwe kuwa Tanzania sasa hivi wananchi wengi wanaunga mkono mabadiliko na kukandamiza upande mmoja sana sana kutaamsha hasira za watu na si ajabu waandishi wa habari hasa wa vyombo wakaanza kupigwa wanapojitokeza kwnye matukio mbalimbali kwa kutozingatia weledi. Vyombo vya habari vya CCM havina tatizo kwa sababu ndio wajibu wao kuteteta chama chao. Lakini chombo cha umma kinachochangiwa na kodi za watanzania wote kinapokuwa biased wanajihatarishia usalama wao wenyewe.


  Mbili. Kulidhibiti Bunge na mijadala ya wabunge ili wasiikosoe serikali. Mkakati huu umefanyika kwa kuhakikisha kwamba Sita anaondolewa kwenye nafasi ya uspika na kumweka spika ambayo anjua wazi kwanini yupo pale na kazi hiyo anaifanya vema kweli kweli. Kulinda maslahi ya serikali na chama, na sio ya wananchi. Wote tu mashahidi wa yanayoendelea bungeni hasa katika kuuminya upinzani. Matokeo ya huu uonevu umesababisha hasira bungeni na malumbano yasiyokuwa na tija. Wapinzani hawana tena uhuru wa kuikandia na kuikosoa serikali. Wakati wa Sitta mwongozo ukiombwa kwa ajili ya kuvuruga hoja za wapinzani spika Siita alinukuliwa wakati mmoja akiwaambia wabunge wawe na ngozi ngumu kwa sababu kwenye siasa za upinzani hutegemei mpinzani wako aseme yale yanayokupendeza wakati wote. Leo hii tunakosa uongozi wa namna hii kwenye bunge letu. Kutokuwa makini kwa "Kiti" kumelifanya bunge kuwa kichekesho. wabunge wa CCM wamejisahau wamekuwa watetezi wa serikali badala ya kuhihoji na kuipeleka mchakamchaka. Halii hii ya upendeleo bungeni inaonwa na wanachi na inapandisha hasira zao na kufanya upinzani hata huku mtaani unakuwa km uhasama. Si jabu kusikia watu wanapigana hata kuuana kwa sababu hizi. Kiti cha spika kijirekebishe la sivyo kitachangia kuleta vurugu za kisiasa Tanzania.

  Tatu. Kudhibiti vyombo vya usalama na kuhakikisha vinaibebba serikali muda wote. Hili ndio limekuwa tatizo sugu kabisa. Mauaji na mateso kwa wapinzani wa serikali siku hizi ni SUNNA. Uchunguzi unaofanyika haujulikani unakoishia hasa jambo linapokigusa chama tawala na serikali. Jambo likihusisha wapinzani linavaliwa bango kweli kweli. mfano swala la ulimboka (mwenyekiti wa madaktari) mpaka leo serikali haitaki kuunda tume huru ya uchunguzi. Rejea hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni leo kuona jinsi serikali inavyohusika na kupuuza manyanyaso ya raia has wa upande wa pili. swala la Ndago kwa mfano hakuna anayezungumzia uchokozi uliofanywa na vijana wa kihuni wa CCM. Bali linalosemwa ni Mbunge wa CCM alikashifiwa. Hii ni sawa na kusema kwa hiyo vijano walorusha mawe walifanya sawasawa tu? Jeshi la polisi linataka kutuambia kwamba mbunge wako akitukanwa una haki ya kumuadhibu mtukanaji? Matusi ya Lusinde hadharani wameyasahau? Akitukanwa wa CCM ni kosa, lakini akitukanwa wa upinzani ni sawa tu? Na je kwa nini hawakuwakamata wale vijana waliokuwa wananzisha vujo pia ili wahojiwe kwa nini waliingila mkutano halali wa chama kingine? Na waseme nani aliwatuma kufanya hivyo. Hi ni double standards katika kushughulikia uhalifu. Wakamatwe walioua na waliochochea mauaji ili tujue haki imetendeka. La sivyo polisi nao wanaamsha hasira za wananchi na matendo kama haya yataendelea kwa mtindo wa kulipiza kisasi kama haitatendwa au kuonekana ikitendeka.

  Hizi zote tatu zimekuwa ni mbinu za CCM kutaka kupunguza upinzani dhidi yake ili wananchi wasijue udhaifu wa serikali yao na sababu za wao kuendelea kuteseka na maisha magumu. Kwa wapendwa CCM na serikali hizi mbinu ni za hatari na zinaweza kuliingiza Taifa katika machafuko. Acheni vyombo vya umma vifanye kazi kwa haki kwa ajili ya watanzania wote. Hamuwezi kulazimishwa kupendwa. Na mkijaribu kufanya hivyo mtaipeleka nchi kubaya. Wananchi wakihisi vyombo vya umma vinafanya kazi yake bila upendeleo basi hata nyie seriakali mtakuwa na la kujivunia lakini mkiendelea kutumia vibaya vyombo hivi vinavyolopiwa kodi na watanzania wengi ambao siki hizi wana mwamko mkubwa wa kisiasa basi mjue mnaliingiza Taifa kwenye machafuko. Tukiiendelea hivi uchaguzi mkuu ujao mauaji ya kisiasa yatazidi yale ya Kenya kwa sababu Tanzania sasa hivi mwamnko wa kisiasa upo juu. Mark my words!
   
 2. S

  SHIMBONONI Senior Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mkuu,
  Ubarikiwe sana kwa Uchambuzi makini!
   
 3. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Nne- kudhibiti mahakama. Hakuna pa kupumulia!
   
 4. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  respect mkuu maneno ya busara haya na uchambuzi makini.
   
 5. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Eti ccm ni mgonjwa aliyekitandani kwa zaidi ya mwaka anasubiri kuaga dunia,
   
 6. mujemaso

  mujemaso Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 95
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  Respect kwa uchambuzi makini. Hilo la nne aliloongeza mdau ndo msumari wa mwisho kwenye jeneza! Hii ni ishara ya binadamu kupoteza utu, unapataje ujasiri wa kuficha ukweli wakati wanyonge wanaangamia? Asilimia kubwa ya watu walioajiriwa wana asili ya familia maiskini, wana ndugu masikini lakini hilo haliwagusi wako tayari kujipendekeza kwa kutekeleza matakwa ya hao wanaowanyanyasa wanyonge!
   
 7. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuchochea migomo ya wafanyakazi kama vile madaktari,walimu nk ili ionekane serikali imeshindwa kutawala/nchi isitawalike.
   
 8. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kumwagia wananchi tindikali kama kule igunga ili kuwatisha
   
 9. k

  kibugumo JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 1,347
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  kubambikia wapinzani kesi ili waonekane ndio wanaohatarisha amani ya nchi,wamenukuliwa mara nyingi sana wakisema
  CDM wana ajenda ya siri ya kuhakikisha nchi haitawaliki.
   
 10. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Ishara nyingine kwamba serikali haipo, waliopo ni walalamishi tu. Serikali halali huchukua hatua kwa mamlaka iliyopewa kihalali. Sasa kama wote tunalalamka tu ni nani atakayetoa maamuzi? Ama kweli utawala wa manyani!!
   
Loading...