MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
- Thread starter
- #141
Kukanusha na kurumbana ni vitu viwili tofauti. CCM na Serikali wanachofanya ni kurumbana.Umeandika mengi lakini umesukumwa zaidi na mapenzi kwa chama tawala, unaweza kupuuza au kutomjibu mtu kama anachosema ni uongo, lakini kama mambo mengi yanayodaiwa ni ya kweli utajitahidi kukanusha kwa kuwa hata kama ni uongo ukisemwa kwa muda mrefu unakuwa ukweli na hili serikali inalijua.
Pili mimi nataka msikae kimya mkanushe kwa kujibu hoja, kwa mfano anasema Magufuli anaminya demokrasia, sasa nyinyi mnatakiwa mtuonyeshe ni kwa kiwango gani Magufuli ametanua demokrasia kwa watu. Anasema anafanya manunuzi bila kufuata sheria ya manunuzi, tuonyesheni ni kwa namna gani mchakato wa manunuzi ulifanyika na bunge kushiriki. Anasema mlikula pesa za tetemeko Bukoba, tuonyeshe ni namna gani waathirika walipata pesa. Mambo yako mengi sana. Wewe unashauri wakae kimya huo ni ushauri wa ovyo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kukanusha serikali walishakanusha, sasa kuendelea kurumbana tena wakitumia viongozi wa juu wa chama na serikali ni ujinga wa kiwango cha juu.
Hili suala sio kama wimbo eti CCM na serikali wanaimba kila mara. Hata wimbo hufika kipindi ambacho unachuja na kukosa waimbaji.