Serikali na CCM acheni kumpa Tundu Lissu umaarufu wa bure!

Nimekuwa kimya na mtazamaji kuhusiana na suala hili la Tundu Lissu lakini baada ya kuangalia kwa muda nimegundua madhaifu mengi sana kwa upande wa serikali katika kukabiliana na yanayojiri kwenye suala hili.

Serikali na CCM wamekuwa reactive badala ya kuwa proactive ambapo matokeo yake wanafanya makosa mengi ya msingi hasa mahusiano ya umma.

Serikali na viongozi wa juu wa CCM kukimbizana na Lissu kwenye vyombo vya habari ili kujibu hoja zake ni ujinga wa kiwango cha juu kwa sababu kufanya hivyo ni kujiweka wazi kwenye maswali ambayo hanaya majibu ya kisiasa bali kiuchunguzi. Kimantiki taasisi ya kiuchunguzi wa makosa ya jinai haiwezi kutoa majibu ya uchunguzi kama uchunguzi haujakamilika lakini pia hata yakitolewa huwa yanatolewa kitaalam na kwa uangalifu mkubwa sana bila kujali mwathirika/waathirika wanafikra zipi.

Lissu akiwa anahojiwa na waandishi wa habari bila kuwepo maafisa wa serikali ni faida kwa serikali na CCM kuliko ofisa wa serikali na CCM kuwepo pia katika mahojiano hayo. Mahojiano yake katika kipindi cha HARDtalk bila uwepo wa ofisa wa serikali yaliinufaisha zaidi serikali kuliko muhojiwa. Hata pale alipotoa shutuma, mtangazaji alimwambia aache kutoa shutuma ambazo anaowatuhumu hawapo ili wazijibu.

Ni ujinga kwa serikali kudhani kuwa kinachofanyika hapa Tanzania hakijulikani katika makorido ya watawala wa Ulaya na Marekani na kwa maana hiyo wanakwenda kujibu tuhuma za upotoshaji. In fact, watawala wa Ulaya na Marekani wanajua hata yale yanayosemwa ndani ya Ikulu ya Magogoni nchini achilia mbali anayoyasema Lissu. Kwa maana hii, kama Lissu anayosema ni kweli au uwongo watakuwa wanajua.

Kwa mfano, juzi Gazeti la The New York Times la Marekani ambalo lina mahusiano ya karibu sana na majasusi wa Marekani lilipewa audio yenye maongezi ya mwana mfalme, Mohammed bin Salman akiwaambia watu wake wa karibu kuwa atatumia risasi kama Jamal Khashoggi hatarudi Saudi Arabia na kuachana na ukosoaji wa serikali. Hii inaonyesha kuwa kila anachokisema na kukifanya ndani ya nyumba yake kinajulikana kwa majasusi wa nchi ya Marekani.

Hii ina maana kuwa serikali inapoteza muda kujitetea kwenye suala la Tundu Lissu na demokrasia kwa sababu watawala wa Ulaya na Marekani wanajua kama ni kweli au uwongo.

Serikali lazima waelewe kuwa anachokitaka Tundu Lissu ni reaction ambayo ni reactive kutoka serikalini ili aendeleze marumbano na mijadala kwenye vyombo vya habari ya ndani na nje.

Ninakumbuka kwa mara yangu ya kwanza kusafiri katika nchi za Ulaya nilipewa ushauri kuwa ukimuona mtu anakuchokoza au kukuchochea unachotakiwa ni kutoonyesha hisia au kujibu. Kutoonyesha hisia au kujibu kutamfanya akose sababu ya kuendelea kukuchochea au kukuchokoza lakini kikubwa zaidi ataona anachofanya ni ujinga na kuachana na uchochezi au uchokozi.

Serikali ikikaa kimya hata wale wanaomuhoji Lissu watachoka kwa sababu kutakuwa hakuna reaction kutoka serikalini. Kukosa reaction kutoka serikalini ina maana hata mahojiano yanakuwa hayahitajiki (redundant). Serikali lazima waelewe dhana ya Newton's third law of motion. No force, no reaction lakini kikubwa zaidi uendeshaji wa serikali ni sawa na mbio za masafa marefu(marathon). Kuna wapiga kelele wataibuka na baadaye watapotea.

Watu wenye fikra pana wanaomfahamu Lissu hawashangai na kile anachokisema bali wanachoshangaa ni jinsi ambavyo viongozi wa juu wa CCM na serikali wanavyojibishana naye kwenye vyombo vya habari.

Kwa mtu mwenye fikra pana na anamfahamu vizuri Lissu atajua hupenda sana kujionyesha mbele ya watu/hadhara (limelight) lakini pia hufurahia sana (relish) kama kuna reaction bila kujali kama ni nzuri au mbaya. Waingereza huita Attention seeking behaviour. Lissu anachokitafuta kwa CCM na serikali ni kukimbizana au kujibishana naye kwenye media akiwa ndiye focal point.

Mpaka sasa malengo yake kwa kiwango kikubwa yamefanikiwa kutokana na ujinga wa viongozi wa juu wa serikali na CCM ambao wengi wao hawajui ukubwa na umuhimu wa vyeo vyao. Eti Katibu Mkuu wa chama tawala CCM anajibishana na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama cha upinzani CHADEMA, Tundu Lissu? This is beyond stupidity.

Lissu anatakiwa arumbane na wanachama wa kawaida wa CCM na sio viongozi wa juu wa chama. Majibu ya hoja za Lissu kuhusu shambulio lazima yajibiwe na taasisi rasmi za uchunguzi na sio kila kiongozi wa serikali.

Hawa viongozi wa CCM na serikali hawakujifunza makosa waliyoyafanya kwa Mange Kimambi baada ya kumkuza na kupata followers wengi kutokana na kujibishana naye. Makosa yaleyale wanayarudia kwa Tundu Lissu.

Katika dhana ile ile ya Attention seeking behaviour, Ninajua pia Lissu atapenda sana akirudi nchini akamatwe akiwa uwanja wa ndege ili kutimiza Newton's third law of motion ambapo matokeo yake yatakuwa kumpa umaarufu wa bure lakini kikubwa zaidi hata waliokuwa hawaamini aliyokuwa anayasema nwataamini niya kweli. Ninawaomba sana serikali wasimkamate siku akiingia nchini bali wamuache tu. No force, no rection.

Ninakumbuka mwaka 1995 wakati Augustino Mrema akiwa mpinzani maarufu nchini, kila alipobebwa waliombeba walipigwa mabomu na vitendo hivyo vilizidi kumfanya maarufu mpaka Mwalimu Nyerere alipotumia busara na kuwambia polisi, “Kwa kuwa wanaotaka kumbeba Mrema wapo, waacheni wambebe. Wambebe hata kama watakuwa wanapokezana kama machela (jeneza), waacheni.” Polisi walipotii agizo la Baba wa Taifa, la kuacha kuwapiga mabomu, Mrema naye kama shani hakubebwa tena. Mwl. Nyerere alitumia dhana ya Newton's third law of motion. No force, no reaction.

Tuliona pia huko Kenya, baada ya wapinzani kuamua kumuapisha Raila Odinga kuongoza Kenya baada kutangaza kwamba hamtambui Uhuru Kenyatta kama kiongozi aliyechaguliwa kwa njia halali, polisi waliwaacha wafanye hivyo na matokeo yake kitendo hicho kikaonekana nicha kijinga.

Huko Venezuela tumeona kiongozi wa upinzani akifanya kama alivyofanya Raila Odinga lakini dhumuni lake lilikuwa ni kutaka polisi wawazuie ili mapigano yatokee ambayo yangekuwa ni sababu ya Marekani kuingia kimabavu katika nchi hiyo kwa kisingizio cha kuzuia mauwaji. Serikali ya Rais Madulo ikajua janja yao na ikamuacha Juan Guaidó ajiapishe bila kumuingilia kwa kutumia nguvu ya polisi/jeshi. No force, no reaction. Uamuzi wa polisi/jeshi kumuacha ajiapishe kumeua malengo ya Marekani ya kuingiza majeshi Venezuela.

CCM na Serikali lazima waelewe kuwa hoja sio Lissu anatumiwa na ''mabeberu'' bali hoja ni jinsi gani wataweza kuzuia njama za ''Mabeberu'' kwa sababu ''mabeberu'' kuwatumia watu sio jambo jimpya.

Kuna Mzee mmoja aliwahi kunipa ushauri kwa maneno haya, Ukimya hukuvisha nguo ya utulivu na hukukinga na haja ya kutoa visingizio lakini pia jawabu fasihi kabisa kwa mpumbavu ni kutomjibu.

Nimalizie kwa kusema, Serikali na viongozi wa juu wa CCM lazima watambue kuwa hata kukaa kimya ni jibu kwa sababu hakuna serikali hapa duniani ambayo haijawahi kutuhumiwa kutaka kuua au kuua raia.
Eti "Anapenda sanaa Televisheni" Tundu Lissu bwana:D:D:D:D
 
Leo naona umelala vizuri na akili zako ziko sawa sawia...

Nakubaliana na hili.

Lakini kumbuka kuwa hata hizo taasisi za kiuchunguzi unazotaka ziwe ndizo zinasema zinakaliwa na makada wa CCM haohao!!

Unakubaliana na mifano ya akina Mrema ambao hawakuwahi kupigwa Risasi? Umekubaliana kuwa cctv camera ilikuwa haki zong’olewe kwenda kufichwa kwa Maliyamungu Bashite? Unakubaliana na walinzi wa Getini kujificha wakati Tundu Lisu anashambuliwa?
 
Eti "Anapenda sanaa Televisheni" Tundu Lissu bwana:D:D:D:D

CCM wamesahau kuwa bila wao kumtuma Maliyamungu Bashite kumpiga Risasi leo hii Tundu Lisu asingekuwa huko Marekani, kiini na chanzo cha kusababisha Tundu Lisu awepo huko ni wao lawama zotee ni kwa Bashite na kikundi chake
 
Tatizo ni kwamba ukiwa na madaraka unaamini sana katika kile ambacho madaraka yanaweza kufanya, matokeo yake unakuwa mbali na kile ambacho madaraka hayawezi kufanya. Hapa ndipo penye hekima na akili.

Ukiwa na bunduki unakuwa unaamini sana katika kile ambacho bunduki inaweza kufanya kuliko kila ambacho bunduki haiwezi kufanya.

Zana yoyote yaweza tawala akili ya mwanadamu.

In short, artificial produces artificial.

Asante sana ndugu....

Mchango mfupi lakini uliobeba maana na mantiki ambayo ukiamua kuichambua, utapata kitabu cha kurasa 2,000!!
 
Mda huu Tundu Lisu asingekuwa yupo Dodoma kama siyo Daud Arbaty Maliyamungu Bashite kumtwanga kwa Risasi mpaka kusababisha awepo huko alipo sasa, lawama zote pelekeni kwa Bashite kwa mbinu zake za hovyo.
 
Serikali aigombani na lissu ata siku moja bali ccm ndo inagombana na lissu we angalia vizur unasema serikali sababu wengi wao ni watumishi wa serikali mama ako akiwa mwalimu na akikupiga nyumbani kisa ujasafisha chumba chako uwezi sema mwalimu kakupiga hapo anakua ni mama ako sasa lissu amepigwa na watu ambao wana sare za jeshi wala kitambulisho cha uajili serikalini uwezi sema serikali mana yanayotokea yote ayafanani na serikali ata mama samia alienda kama yeye na sio serikali kumuona lissu ndugai maamuzi yake ni tofauti na katiba sheria na taratibu zote wanavunja sheria za nchi ingekua kwingine wangeshitakiwa mana wanavunja sheria

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unakubaliana na mifano ya akina Mrema ambao hawakuwahi kupigwa Risasi? Umekubaliana kuwa cctv camera ilikuwa haki zong’olewe kwenda kufichwa kwa Maliyamungu Bashite? Unakubaliana na walinzi wa Getini kujificha wakati Tundu Lisu anashambuliwa?

HAPANA, siyo ktk mtazamo huo...

Nilichokubaliana naye ni kuwaomba wanasiasa wenzake huko CCM kukaa kimya na badala yake kuruhusu vyombo vya kiuchunguzi kufanya kazi....

Kutoka kwa vyombo hivyo, ndipo tutapata majibu ya maswali haya na kuyajadili....

Umenielewa sasa?
 
Huna tofauti na jiwe, amekuwepo serikali miaka yote ila amekuja kujua nchi inaliwa akiwa raisi

Sent using Jamii Forums mobile app

Ha ha ha ha ha ha wewe nitakupa lunch tena sio kidogo na bila aibu anathubutu kusema nchi ilikuwa inaliwa. As if yeye alikuwa ni rais wa nchi nyingine ndio karudi Tanzania wakati alikuwepo na bungeni alikuwepo kwenye kamati pia
 
Nimekuwa kimya na mtazamaji kuhusiana na suala hili la Tundu Lissu lakini baada ya kuangalia kwa muda nimegundua madhaifu mengi sana kwa upande wa serikali katika kukabiliana na yanayojiri kwenye suala hili.

Serikali na CCM wamekuwa reactive badala ya kuwa proactive ambapo matokeo yake wanafanya makosa mengi ya msingi hasa mahusiano ya umma.

Serikali na viongozi wa juu wa CCM kukimbizana na Lissu kwenye vyombo vya habari ili kujibu hoja zake ni ujinga wa kiwango cha juu kwa sababu kufanya hivyo ni kujiweka wazi kwenye maswali ambayo hanaya majibu ya kisiasa bali kiuchunguzi. Kimantiki taasisi ya kiuchunguzi wa makosa ya jinai haiwezi kutoa majibu ya uchunguzi kama uchunguzi haujakamilika lakini pia hata yakitolewa huwa yanatolewa kitaalam na kwa uangalifu mkubwa sana bila kujali mwathirika/waathirika wanafikra zipi.

Lissu akiwa anahojiwa na waandishi wa habari bila kuwepo maafisa wa serikali ni faida kwa serikali na CCM kuliko ofisa wa serikali na CCM kuwepo pia katika mahojiano hayo. Mahojiano yake katika kipindi cha HARDtalk bila uwepo wa ofisa wa serikali yaliinufaisha zaidi serikali kuliko muhojiwa. Hata pale alipotoa shutuma, mtangazaji alimwambia aache kutoa shutuma ambazo anaowatuhumu hawapo ili wazijibu.

Ni ujinga kwa serikali kudhani kuwa kinachofanyika hapa Tanzania hakijulikani katika makorido ya watawala wa Ulaya na Marekani na kwa maana hiyo wanakwenda kujibu tuhuma za upotoshaji. In fact, watawala wa Ulaya na Marekani wanajua hata yale yanayosemwa ndani ya Ikulu ya Magogoni nchini achilia mbali anayoyasema Lissu. Kwa maana hii, kama Lissu anayosema ni kweli au uwongo watakuwa wanajua.

Kwa mfano, juzi Gazeti la The New York Times la Marekani ambalo lina mahusiano ya karibu sana na majasusi wa Marekani lilipewa audio yenye maongezi ya mwana mfalme, Mohammed bin Salman akiwaambia watu wake wa karibu kuwa atatumia risasi kama Jamal Khashoggi hatarudi Saudi Arabia na kuachana na ukosoaji wa serikali. Hii inaonyesha kuwa kila anachokisema na kukifanya ndani ya nyumba yake kinajulikana kwa majasusi wa nchi ya Marekani.

Hii ina maana kuwa serikali inapoteza muda kujitetea kwenye suala la Tundu Lissu na demokrasia kwa sababu watawala wa Ulaya na Marekani wanajua kama ni kweli au uwongo.

Serikali lazima waelewe kuwa anachokitaka Tundu Lissu ni reaction ambayo ni reactive kutoka serikalini ili aendeleze marumbano na mijadala kwenye vyombo vya habari ya ndani na nje.

Ninakumbuka kwa mara yangu ya kwanza kusafiri katika nchi za Ulaya nilipewa ushauri kuwa ukimuona mtu anakuchokoza au kukuchochea unachotakiwa ni kutoonyesha hisia au kujibu. Kutoonyesha hisia au kujibu kutamfanya akose sababu ya kuendelea kukuchochea au kukuchokoza lakini kikubwa zaidi ataona anachofanya ni ujinga na kuachana na uchochezi au uchokozi.

Serikali ikikaa kimya hata wale wanaomuhoji Lissu watachoka kwa sababu kutakuwa hakuna reaction kutoka serikalini. Kukosa reaction kutoka serikalini ina maana hata mahojiano yanakuwa hayahitajiki (redundant). Serikali lazima waelewe dhana ya Newton's third law of motion. No force, no reaction lakini kikubwa zaidi uendeshaji wa serikali ni sawa na mbio za masafa marefu(marathon). Kuna wapiga kelele wataibuka na baadaye watapotea.

Watu wenye fikra pana wanaomfahamu Lissu hawashangai na kile anachokisema bali wanachoshangaa ni jinsi ambavyo viongozi wa juu wa CCM na serikali wanavyojibishana naye kwenye vyombo vya habari.

Kwa mtu mwenye fikra pana na anamfahamu vizuri Lissu atajua hupenda sana kujionyesha mbele ya watu/hadhara (limelight) lakini pia hufurahia sana (relish) kama kuna reaction bila kujali kama ni nzuri au mbaya. Waingereza huita Attention seeking behaviour. Lissu anachokitafuta kwa CCM na serikali ni kukimbizana au kujibishana naye kwenye media akiwa ndiye focal point.

Mpaka sasa malengo yake kwa kiwango kikubwa yamefanikiwa kutokana na ujinga wa viongozi wa juu wa serikali na CCM ambao wengi wao hawajui ukubwa na umuhimu wa vyeo vyao. Eti Katibu Mkuu wa chama tawala CCM anajibishana na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama cha upinzani CHADEMA, Tundu Lissu? This is beyond stupidity.

Lissu anatakiwa arumbane na wanachama wa kawaida wa CCM na sio viongozi wa juu wa chama. Majibu ya hoja za Lissu kuhusu shambulio lazima yajibiwe na taasisi rasmi za uchunguzi na sio kila kiongozi wa serikali.

Hawa viongozi wa CCM na serikali hawakujifunza makosa waliyoyafanya kwa Mange Kimambi baada ya kumkuza na kupata followers wengi kutokana na kujibishana naye. Makosa yaleyale wanayarudia kwa Tundu Lissu.

Katika dhana ile ile ya Attention seeking behaviour, Ninajua pia Lissu atapenda sana akirudi nchini akamatwe akiwa uwanja wa ndege ili kutimiza Newton's third law of motion ambapo matokeo yake yatakuwa kumpa umaarufu wa bure lakini kikubwa zaidi hata waliokuwa hawaamini aliyokuwa anayasema nwataamini niya kweli. Ninawaomba sana serikali wasimkamate siku akiingia nchini bali wamuache tu. No force, no rection.

Ninakumbuka mwaka 1995 wakati Augustino Mrema akiwa mpinzani maarufu nchini, kila alipobebwa waliombeba walipigwa mabomu na vitendo hivyo vilizidi kumfanya maarufu mpaka Mwalimu Nyerere alipotumia busara na kuwambia polisi, “Kwa kuwa wanaotaka kumbeba Mrema wapo, waacheni wambebe. Wambebe hata kama watakuwa wanapokezana kama machela (jeneza), waacheni.” Polisi walipotii agizo la Baba wa Taifa, la kuacha kuwapiga mabomu, Mrema naye kama shani hakubebwa tena. Mwl. Nyerere alitumia dhana ya Newton's third law of motion. No force, no reaction.

Tuliona pia huko Kenya, baada ya wapinzani kuamua kumuapisha Raila Odinga kuongoza Kenya baada kutangaza kwamba hamtambui Uhuru Kenyatta kama kiongozi aliyechaguliwa kwa njia halali, polisi waliwaacha wafanye hivyo na matokeo yake kitendo hicho kikaonekana nicha kijinga.

Huko Venezuela tumeona kiongozi wa upinzani akifanya kama alivyofanya Raila Odinga lakini dhumuni lake lilikuwa ni kutaka polisi wawazuie ili mapigano yatokee ambayo yangekuwa ni sababu ya Marekani kuingia kimabavu katika nchi hiyo kwa kisingizio cha kuzuia mauwaji. Serikali ya Rais Madulo ikajua janja yao na ikamuacha Juan Guaidó ajiapishe bila kumuingilia kwa kutumia nguvu ya polisi/jeshi. No force, no reaction. Uamuzi wa polisi/jeshi kumuacha ajiapishe kumeua malengo ya Marekani ya kuingiza majeshi Venezuela.

CCM na Serikali lazima waelewe kuwa hoja sio Lissu anatumiwa na ''mabeberu'' bali hoja ni jinsi gani wataweza kuzuia njama za ''Mabeberu'' kwa sababu ''mabeberu'' kuwatumia watu sio jambo jimpya.

Kuna Mzee mmoja aliwahi kunipa ushauri kwa maneno haya, Ukimya hukuvisha nguo ya utulivu na hukukinga na haja ya kutoa visingizio lakini pia jawabu fasihi kabisa kwa mpumbavu ni kutomjibu.

Nimalizie kwa kusema, Serikali na viongozi wa juu wa CCM lazima watambue kuwa hata kukaa kimya ni jibu kwa sababu hakuna serikali hapa duniani ambayo haijawahi kutuhumiwa kutaka kuua au kuua raia.
Mkuu hakika ushauri wako kwa CCM na Serikali ni mzuri sana.HONGERA kwa maono hayo.Lakini kwa bahati mbaya ushauri wako hautazingatiwa kamwe kwani CCM yenu ya sasa bila dola HAIPO.HAIPO KABISA.CCM ya ushindani wa kisera aliondoka nayo mh.mstaafu,Dr.Kikwete.
 
Naona mmeanza kukataana wenyewe kwa wenyewe na bado siku mbaya juu yenu imekaribia. Mtamwacha Jpm na Bashiru peke yao huku IGP akilia ya kwake.

Kwa Lissu ukimjibu ukikaa kimya damage iko pale pale, Lissu ataendelea kuwatesa maana bado hamjamjua mnamchukulia poa.

Maumivu aliyo nayo Lissu hakuna ambaye anayajua. Mungu ampe nguvu. na kweli Magu ni mpango wa Mungu hataamini kitakachotokea
 
Ni ushauri wenye mantiki kwa serikali, kosa kubwa lililofanyika toka mwanzo ni kujiangaisha na mpuuzi kama Tundu Lissu, ni mtu anayetafuta sifa binafsi kwa masllahi yake, anaungwa mkono na wapiuuzi wachache wasioipend serikali. Serikali iachane kujishughulisha naye.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ingeachana naye tokea mwanzo ingekuwa vizuri zaidi,tusingeyaona haya mambo MAKUU YA AJABU.YA AJABU.
 
Serikali na viongozi wa juu wa CCM kukimbizana na Lissu kwenye vyombo vya habari ili kujibu hoja zake ni ujinga wa kiwango cha juu kwa sababu kufanya hivyo ni kujiweka wazi kwenye maswali ambayo hanaya majibu ya kisiasa bali kiuchunguzi. Kimantiki taasisi ya kiuchunguzi wa makosa ya jinai haiwezi kutoa majibu ya uchunguzi kama uchunguzi haujakamilika lakini pia hata yakitolewa huwa yanatolewa kitaalam na kwa uangalifu mkubwa sana bila kujali mwathirika/waathirika wanafikra zipi.
Ni kweli wanatakiwa watakao jibu watumie matokeo ya uchunguzi na si siasa tu, bahati mbaya hakuna dalili kuwa kuna uchunguzi unao fanyika hata progress polisi hawajatoa, hii inawafanya wengi wahisi kuwa hakuna kinacho endelea. Sasa wanapokurupuka kujibu ndiyo wanamwaga petroli kwenye maji, na vibaya zaidi hawako coordinated kabisa.
Kwa nchi nyingi kwenye tukio kama hili hata kama uchunguzi hauja kamilika huwa kuna viashiria ya kuwa uchunguzi unaendelea hapa kwetu ikiwapendeza wanakaa kimya na kimya hasa hasa mpaka "unahisi" hakuna kinacho endelea na kwa tukio la LISU kuna mambo mengi yamefanyika au kunenwa ambayo hata kama hutaki kuamini unayosikia mwisho uta amini tu.
Bahati mbaya siono dalili ya kujirekebisha. Cha kufurahisha wengi wanamwona Lisu kama Lisu hawamsikilizi vizuri kuhusu nini anasimamia. Ndio maana tumesikia kuwa ni mjeuri, anatukana, kichaa etc lakini anayosema kuhusu UTAWALA BORA wengi hawaoni, na hili la UTAWALA BORA kwangu mimi ndiyo anapoichoma serikali na anaichoma vibaya kweli.
 
Ni kweli kwani Bashite ndiye yupo busy mitandaoni kupambana na Tundu Lisu hata viongozi wa CCM wengi wapo chini ya Bashite hawana uwezo wa kupinga chochote anachopanga ikiwemo shambulio la Tundu Lisu, yafaa magufuli aandae mkutano wakutane na Tundu Lisu wazungumze utafutwe muafaka badala ya kuendelea kumsikilza Bashite ambaye ana roho mbaya akitaka kuwaua Wapinzani wote
Hivi akina mzee mahiga, warioba,....mbona busara wanazo hata za ziada, ni kwamba hawamshauri Magufuli au wamemziria nchi?, Nchi hii ni kubwa huwezi kuongoza peke yako ukafika kokote, mbaya zaidi hao vijana walio mzunguka ni janga wanahitaji kuongozwa kwa karibu kwani busara zao ni ndogo mnoo/hazipo kabisa. Wao ni kutumia kalamu ya "mkuki" kusaini makubaliano na kila anaye tofautiana na serekali
Ng'ombe ni wetu sote kila mmoja wetu anamtakia azae majike ili idadi iongezeke kwa kasi..
 
Penye ukweli hakuna mbinu yoyote itakayofaa hapo maana siku zote ukweli na uongo hutengana. Wakae kimya au wajibu haiwezi kubadilisha ukweli ukawa uongo utabakia kuwa ukweli. Kwangu mimi ni kosa kubwa lililofanyika mwanzo na baada ya kutokea vile ilibidi wapeleleze na kukamata watuhumiwa lakini kwasababu siyo wote waliokubaliana na huo uamuzi ndiyo maana polisi wamekaa kimya tu hata hawajafanya chochote hali ambayo sasa inafanya hata watu wenye uelewa wa kawaida tu kuona kuwa kuna walakini katika hilo tukio. Kuna matukio yanatokea usuku unafanyika upelekezi watu wanakamatwa sasa hapo mchana kabisa iweze hata mtuhumiwa wa kushukiwa tu hakuna. Katika mazingira hayo sioni option nzuri zaidi ya kuamuwa kufanya upelelezi wa nani alifanya hivyo hata kama mwenzao kumtosa kwa ajiri ya mustakabali wa taifa letu maana ni kama tunagawanyika makundi makubwa mawili. Umesema Lisu anaungwa mkono na watu wachache wasioipenda serikali siyo kweli anaungwa mkono na watu wengi wasiopenda mauwaji yanayoendelea. Huo ndiyo ukweli hata kama ni mchungu ila kuna kikundi cha watu wachache wanaoratiba hayo mauwaji ndiyo wanahangaika sana kujitetea lakini kila siku wananchi wazidi kugundua ukweli mwisho kila mwanachi atajuwa ukweli ndipo serikali itabidi ichukuwe hatua ambazo wananchi wanataka kwasababu serikali ni ya wananchi haiwezi kujifanyia inabotaka ikawaacha wananchi na matarajio yao.karibia kila siku ukweli unawekwa wazi zaidi. Mfano hadi leo seriakali haijafafanua ni nani hasa aliyeagiza kuondolewa kwa wale askari wa getini ili kufanikisha hilo shambulio. Na haiwezekani mtu mdogo tu akaamuru askari wanaolinda viongozi wa serikali waondolewa getini. Hilo swali ni vigumu kulijibu ndiyo maana hadi sasa ni kimya kama vile serikali haipo. La CCTV nalo hivo hivo katika majibu yanayotolewa na serikali ni Lisu na dereva warding wahojiwe lakini siyo kujibu hizo hoja mbili
 
Umeongea jambo moja tu lakini ukalirefusha sana nadhani una sababu binafsi ya kufanya hivyo na faida yake unaijua wewe, maana lengo lako serikali na ccm wakae kimya kwa vile wanaaibika kwa kumjibu Lissu. Lakini kuna kitu ulitakiwa kukieleza ingawaje umekimbilia taasisi ndiyo ijibu. Kitu hicho ni Je, serikali haina jukumu la kufanya uchunguzi wa shambulio la Lissu, na kama inalo imelitekeleza inavyotakiwa? Kama imetekeleza basi ina majibu na kama haijatekeleza lazima ikose majibu au itoe majibu viza. Lissu ni mwanasiasa mkubwa na mwenye mvuto kitaifa na sasa kimataifa, kukaa kimya bila kusema ukweli kuhusu shambulio lake kama kweli serikali haijahusika ni kuuaminisha Umma na Dunia maana "Silence means yes". Serikali ilikosea tangu siku shambulio linapangwa (kama kweli ni wao na dalili zote zinaonesha) na aliyelipanga ni miongoni mwa maafisa wajinga kuwahi kuwemo kwenye serikali. Kosa hili linailenga serikali kwa sababu inaonesha aina ya mashambulio ya kijinga yanayolandana. Tofauti iliyopo kati ya shambulio hili na la Dr. Ulimboka ni ndogo sana maana Lissu alifuatailiwa na watu aliowataja ni wa serikali, Dr Ulimboka aliitwa na mtu aliyemtaja kwa jina la Ramadhani Igondu na ikathibtika ni wa Serikali, kisha wote baada ya ufuatiliaji na tuhuma za wazi kwa serikali wakashambuliwa na kuumizwa vibaya na wote walikimbizwa nje ya nchi kwa ushauri na msaada wa taasisi zao (Chama cha Madaktari na CHADEMA). Katika matukio yote mawili kosa la kipropaganda la kijinga likafanyika kwani Baada ya matukio walitengenezwa watu wa siasa kieneza uongo ili kujificha kwenye kivuli cha " ni shambulio la uhasama" utadhani watanzania na Dunia nzima ni wapumbavu wote. Kwa Lissu likaongezeka kosa la kijinga la Serikali kutojitokeza hadharani angalau kujikosha kwa kukemea, lakini pia washauri wabovu wakashauri Lissu anyimwe fedha za matibabu (Mashauri huyu ni mjinga No.2 kwenye issue hii). Nikupe mfano, kitendo cha Mama Samia kwenda hoapitali Nairobi kiligeuza upepo wa shutuma japo kwa kitambo na kama kingekuwa na mwendelezo kingebadili kabisa upepo wa Shetani mbaya, lakini kwa vile hakuna mwenye akili kwa sasa serikalini na Chamani Bali nguvu ndo dira waliacha njia hii na wakaweka katazo la kumtembelea Lissu. Acha wavune matunda ya upumbavu wao maana ushauri wako kwa sasa hauwasaidii zaidi ya kuwafanya waonekane wahusika zaidi. Chochote wanachokifanya kwa sasa kinawadidimiza zaidi kwenye shimo la uhisika. Waliyakoroga ni wajibu wao kuyanywa.

Sent using Jamii Forums mobile app
you nailed the whole truth
 
Mkuu mwenyewe juzi nimeliongea hili, NI UPUMBAVU KIWANGO CHA SGR kwa viongoz wa serikali kujibishana na Lisu. Lisu hatafuti majibu nani kampiga Risasi coz kila siku anawataja na kutoa kejeli na dhihaka kibao. Lisu nao anataka MAJIBISHANO aendelee kupata KIKI.Hakuna jibu lolote Lisu atapewa ye na wafuasi wake wakakubali bila ya suspects wake kutajwa. Yaani tayari wana majibu yote ya uchunguz mfukoni. Ni mambo ya kipumbavu kwa kiongoz wa serikali asiye ma taaluma yyt ya kipelelezi na hausiki na jeshi la polisi kumjibu lisu. Nafikiri jpm kazungukwa na VILAZA wengi kiasi kushindwa kumsaidia pale panapohitajika msaada wa maana na kazungukwa na watu ambao nao wanapenda kiki za kisiasa na sio weledi. Swala la lisu kila kiongoz anataka kujionesha naye kasaidia serikali ili Mwisho kama ni cheo au favour flani apate kutoka kwa mkulu.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
ndio unagundua kama ni Upumbavu wa serikali ya awamu ya tano leo? umechelewa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom