Serikali na Bunge Geu: Kubadili kanuni na sheria kwa hila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali na Bunge Geu: Kubadili kanuni na sheria kwa hila

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Big Dady, Feb 9, 2011.

 1. B

  Big Dady Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wana JF, yaelekea tunashangaa sana yaliyojiri bungeni jana. Kwa wana demokrasia yameamsha hasira tena, lakini ndio hali ya nchi hii. Hebu tujikumbushe:

  1. Ili kukwepa Mrema Lyatonga asigombee Urais kupitia CCM mwaka 1995, CCM iliweka vigezo kwa mgombea wao kuwa na digrii moja. Lyatonga akalazimika kuingia upinzani.

  2. Mwaka 2000 CCM waliondoa kipengele hicho ili kumwezesha Aman Karume kugombea urais wa Zanzibar maana hakuwa na digrii.

  3. Mwaka 2006 Hamad Rashid wa CUF alishinikiza kuwepo neno 'kambi rasmi ya upinzani bungeni' ili CUF ipate fursa ya kuongoza kamati tatu muhimu. Alidhani na kuamini kwamba CUF itakuwa kambi ya upinzani daima kwa sababu ya wabunge toka Pemba. Safari hii mambo yamegeuka si CUF tena, ni CHADEMA kilicho chama cha upinzani Bungeni. Kuona hivyo Hamad huyo huyo, amekula njama na swahiba zake CCM wanabadili kanuni ili Chadema kikose haki ya msingi kuisimamia serikali. Na kwa sababu ya ule mwafaka za Zenji, jamaa wamekubali.

  So, hii ndio CCM na serikali yake ni vigeugeu kila wakati. Litakalofuata ni hili, siku Chadema ikishinda kwa asilimia 45 na CCM wakapata 41, basi CCM wataungana na vyma vingine ili kuweka kanuni ya Chama kinachoshinda kulazimika kufikisha asilimia 50. Watafuta kanuni za sasa na kuweka zingine ili uchaguzi urudiwe. Hapa kinachotangulizwa si maslahi ya taifa bali ya wao na wapambe wao.
   
 2. H

  Haika JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Nimeona muujiza wa mwaka jana!!
  Yani mtu mzima unawasha mike kuzomea!!!

  Nawaonea huruma ambao hawakufanya vile, kwani wamechanganywa kwenye kapu lenye samaki wabovu.

  Sauti ya Mnyonge CDM imesikika, na lilikuwa lengo lao.

  Navyojua mie lengo la kutoka nje ni kutuwakilisha katika hii hoja ya kubadili kanuni bila mwongozo wa kueleweka. Namna ya kutuwakilisha ndio hiyo. Sauti imefika mbali zaidi ya wote wangeruhusiwa kutoa hoja kwa maneno!!
  Hongereni sana.

  Wasiwasi wangu ni kuwa wangapi katikati yenu mna vifua, na ngozi ngumu ya kuhimili haya hadi miaka na miaka?
  Nadhani mnajua hii sio njia fupi,
  Cha muhimu mjue tu, mtakapokuwa mnatetea wanachi wa kawaida, tutakuwa nyuma yenu, ila mtakapobadilika na sie tunageuka,
  Nadhani ni wachache (najua wapo) washabiki wa individuals, lakini pia tupo sie washabiki na wafuasi wa ideas.
   
 3. cabhatica

  cabhatica JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 1,074
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Wakati wa kuchagua naibu spika kura zilionyesha wazi kwamba vyama vingine havikumuunga mgombea kutoka CDM. Leo vyama hivyo vinataka kushirikiana kuunda upinzani. Mwenye akili na afahamu!
   
Loading...