kiwiko
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 1,307
- 2,065
Narudia tena. Hii salamu haifai kwanza inahusishwa na biashara ya utumwa kuendelea kutumiwa na mwafrika ni kumdhalilisha mwafrika.
Pili huwezi jua nani uumpe na nani usimpe maana huwez kuwa unafanya kazi ya kukadiria miaka kila siku mpaka akili inachoka kupelekea kuleta migongano kwenye jamii kisa mtu kuona kadharauliwa akinyimwa shikamo na mtu anayemzidi umri. Salamu imekaa kibaguzi sana hasa wakubwa wakiitumia kubagua na kukandamiza waliowazidi umri. Serikali ifute hii kuondoa yote haya.
Mwisho, tutumie salamu kama tunavofanya kwenye makabila au kwenye dini zetu ambako salamu ni moja na maisha yanakwenda vizuri bila migongano. Hata nchi nyingi tu salamu ni moja na maisha yanasonga salama tu.
Tukifuta hii salamu itaongeza mwingiliano zaidi wa rika(social interaction) itakachopelekea ukuaji wa ujuzi na maarifa kutoka rika la chini kwenda rika la juu. Nidhamu ya woga itaondoka.
Serikali na BAKITA tunasubiri tamko.