Serikali mulikeni haya matumizi ya energy drink!

waujua vizuri ulanzi? Basi mie hadi kuutengeneza naweza, yaan kwa ulanzi hapana hasa ule uliogemwa siku hiyo hiyo wee, utamu wake sasa kunoga kwene kukita lyo lyo lyo. Afu ukakekema chwaaaaaaah stimu yaki hinu penapo wacha kujova cc.
😂😂😂😂 Unavyouzungumzia huo ulanzi inaonekana waupenda mno... endelea kuenjoy mdogo wangu
 
Kazi ya Serikali ni kulinda watu mkuu...wewe kitu kina madhara ...Serikali kimyaaaa inakusanya Kodi!?
Acha kuwa kasuku..nani kakwambia hivyo vinywaji vina madhara?kwani unadhani tbs na vyombo nyengine vya serikali hawajazikagua?
 
Sijawahi tumia energy drink..ningependa kujua kwa watumiaji huwa wanajisikiaje wakishatumia icho kinywaji...😊


Mimi nilishakunywa Mo energy, aisee ilinipekekesha, nilipatwa na maumivu sehemu za nyonga, yawezekana mafigo yangu yalikuwa dhaifu kuchuja kemikali za hiyo juice. Sijui kwa watumiaji wengine.
 
Caffein ni bases(alkali) za nitrogen zinazopatika kwenye mmea wa chai na kahawa zinazo fanya kazi ya kuongeza nguvu mwilini
Faida inaongeza nguvu
Kukata usingizi
Kuongeza mkojo kutoka kwa wingi
Kuongeza umakini na uharaka wa kutenda jambo kwa muda mchache ndani ya sekunde chache sana
Hasara
Kuongeza kasi mapigo ya moyo kwa watu wenye mshtuko wa moyo kufa ni chap
Kukata maziwa kwa mama mnyonyeshaji
humfanya mtu kua na hasira
Kukunyima usingizi kwa kunywa mda wa kulala
Hitimisho
Kawaha chai na energy drink(vinywaji nishati) ni bora kwa afya na uraibu na madhara ni tofauti na pombe na ni halali kwa sisi waislamu ila hakikisha unakunywa kilochopitiwa na tbs na chapa inayoaminika
 
Mimi nilishakunywa Mo energy, aisee ilinipekekesha, nilipatwa na maumivu sehemu za nyonga, yawezekana mafigo yangu yalikuwa dhaifu kuchuja kemikali za hiyo juice. Sijui kwa watumiaji wengine.
Alafu hiyo mo energy si peke yako..Kuna mtu aliwahi patwa na hali Kama yako alivyokunywa..nikajua labda atakuwa na matatizo yake binafsi..
 
Unajuaje kama wanakuwa na uchovu au wanahitaji wasisinzie Ili kufanya kitu fulani nk nk

Mbona mimi huwa natumia nikitaka kwa mfano kama na activities za ucku au nina uchovu mwingi na natumia kwa maelezo yaliyopo na hakuna shida yoyote.

Bora hizo energy drinks kuliko ma soda na mawanga yamewajaa mavitambi hovyo hovyo.

Naona tupo wote kwenye mstari mmoja.
 
Sikukipenda hiki kinywaji toka mwanzo,maana nilijaribu tumbo lilijaa gass siku nzima.
 
Kazi ya Serikali ni kulinda watu mkuu...wewe kitu kina madhara ...Serikali kimyaaaa inakusanya Kodi!?
Hivi Leo hii ukisikia: "Eeee bwanaee kumbe energy drinks zinatengenezwa na maji wanayopigia deki mortuary!!" Hivi utasubiri Serikali itamke?
 
kama wanafanya kazi shughuri za kutumia nguvu waache watumie hazina madhara kazi ipo kwenye sisi vijana wa mjini
 
Back
Top Bottom