Serikali Mseto nchini Israeli chini ya Benjamin Netanyahu na Benny Gantz kuapishwa Alhamisi. Mike Pompeo yupo Jerusalem kuhakikisha utulivu unakuwepo

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,398
Serikali mpya ya dharura ya umoja wa kitaifa inatarajiwa kuapishwa rasmi nchini Israeli mapema kesho.

Serikali hiyo itaundwa na vyama vya Likud, Blue and White, Shas,United Torah Judaism, Labor na chama cha Derech Eretz.

Waziri mkuu Benjamin Netanyahu anatarajiwa kutangaza ajenda ya Marekani ya kuhakikisha theluthi tatu ya ukanda wa Magharibi inakuwa sehemu ya kudumu ya Israeli

Itakumbukwa kuwa mwezi January raisi Donald Trump alitangaza kuwa mpango mpya wa Marekani "Vision of Peace Plan" kati ya Israeli na Palestina ni wa kuhakikisha kwamba theluthi tatu au asilimia 30 ya ukanda wa Magharibi au West Bank unakuwa sehemu na makazi ya kudumu ya Israeli jambo ambalo Palestina imelikataa katakata

Mike Pompeo aliwasili mjini Jerusalem jana jioni kushuhudia pamoja na masuala mengine kitendo cha waziri mkuu wa sasa Benjamin Netanyahu akikabidhi jukumu ya kutangaza kuwa asilimia 30 ya ukanda wa magharibi sasa ni sehemu na makazi ya kudumu ya Israeli.

Mike Pompeo angeweza kuzungumza na Netanyau pamoja na Benny Gantz ambae ataongoza serikali ya mseto kwa pamoja na Netanyahu ni wa kutoka chama cha upinzani kwa njia ya simu ya video au video conferencing au njia ya simu ya kawaida lakini kitendo cha kusafiri na kutua Jeresalem kinaashiria umuhimu wa Pompeo kuwepo hapo.

Benjamin Netanyahu ambae anaongoza taifa la Israeli kwa miaka 11 sasa, anaachia madaraka makubwa ya uwaziri mkuu na hata nafasi ya kuwa naibu waziri mkuu baada ya uamuzi wa mahakama kuu kuwa tuhuma anazokabiliwa nazo za rrushwa na ufisadi zinamfanya asiweze kuendelea kuwa waziri mkuu wa Isralei kwa asilimia 100.

Ndani ya miaka mitatu, serikali mpya ya umoja wa kitaifa itakuwa ikingozwa kwa pamoja na bwana Bennie Gantz ambae zamani alliwahi kuwa mnadhimu mkuu wa jeshi la ulinzi la Israeli IDF na ndie aliekuwa spika wa bunge la Israeli ya Knesset akiwakilisha chama cha Blue and White..

Benjamin Netanyahu ataendelea kuwa waziri mkuu huku Gantz akiwa waziri wa ulinzi na naibu waziri mkuu kwa miezi 18 na baada baada ya hapo Gantz atakuwa waziri mkuu huku Netanyahu akiwa naibu wake.

Katika makubaliano ya kuunda serikali ya mseto Netanyahu na Gantz wamekubaliana kwamba yeye (Netanyahu ataendelea kuwa na sauti juu ya uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali na pia ataendelea kuishi kwenya makazi yake ya sasa. hii inampa ahueni bwana Netanyahu kwani ikiwa mwanasheria mpya serikali atakuwepo ataweza kupendekeza Netanyahu kuondolewa kwenye nafasi ya uwaziri mkuu.

Pia wamekubaliana kwamba endapo mahakama kuu itamwondoa madarakani bwana Netanyahu kutokana na kukutwa na hatia ya ufisadi basi bwana Gantz atapaswa kuitisha uchaguzi mkuu.

Pia nafasi za waziri wa sheria na ile ya mambo ya nje zimeenda kwa watu wa Blue and White bwana Avi Niseenkorn wakati bwana Gabi Ashkenazi ambae pia ni mnadhimu mkuu wa zamani wa IDF anakuwa wazri wa mambo ya nje. Hivyo Israeli itakuwa na majenerali wa zamani bwana Gantz akiwa waziri wa ulinzi na Ashkenazi akiwa wazri wa mambo ya nje.

Mpangp mpya wa Marekani juu ya ugawaji wa sehemu hiyo ya ukanda wa magharibi unaipa Israeli uwezo mkubwa wa kutawala kijeshi eneo hilo, sehemu kubwa ya ardhi ya eneo hilo na pia sehemu zote za Jerusalem na makazi yote ya kudumu ya waisraeli.

Nchi za Umoja wa ulaya zikiongozwa na Ufaransa, Ireland na Belgium zimeripotiwa kutishia kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Israeli endapo itavunja sheria za kimataifa pindi itakapojitangazia kuwa sehemu hiyo ya ukanda wa magharibi ni yake.

Kitendo cha raisi Donald Trump kumtuma bwana Pompeo harakaharaka kwenda Jerusalem na kuhakikisha mpango huo unatekelezwa ni kitendo cha raisi Trump kujitafutia kura zaidi kwa kuzingatia kwamba kampeni zake za uraisi zinategemea masuala kama hayo pamoja na jinsi gani ameongoza vita dhidi ya ugonjwa COVID-19

Ndoto za Palestina kuwa na haki ya kumiliki ardhi ndani ya ukanda wa Magharibi zimepunguzwa nguvu kubwa kutokana na sasa Israeli kufundi kuongozwa na majenerali wa zamani wa jeshi la IDF ambao tayari wameagiza idara ya ujasusi wa ndani ya Shin Belt kuhakikisha kila raia wakiwemo waisraeli wenyewe, anachunguzwa mienendo yake wakiwepo wapalestina khasa kwa kutumia vita dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.

Ufuatiliaji huo wa lazima au Surveillance Powers unahusisha kuchungua simu za mikononi khasa wale wanaowasiliana na waathirika wa COVID-19.

Utawala wa Palestina unaongoza sehemu ya ukanda wa Magharibi umeomba kiasi cha dola milioni 120 ili kuzitumia kubapambana na ugonjwa wa COVID -19 ambao mpaka Jumatatu walikuwapo wagonjwa 449 na vifo vinne.

Asilimia 17 ya idadi ya watu hawana ajira na robo tatu ya wakazi hao wanategemea misaada kutoka nje

Richard na vyanzo mbalimbali.
 
Mike Pompeo anahakikishaje utulivu kuwepo kwenye tukio la kuapisha?
Watu wana jeshi liko active tangu nchi haijaanzishwa wewe unamtaja Pompeo ambaye kwanza atapokea ulinzi kutoka kwao.
 
Mike Pompeo anahakikishaje utulivu kuwepo kwenye tukio la kuapisha?
Watu wana jeshi liko active tangu nchi haijaanzishwa wewe unamtaja Pompeo ambaye kwanza atapokea ulinzi kutoka kwao.

Armata, tulia utafune chakula, halafu kama chakula hicho ni kitamu basi wewe wameza tu.

Usikimbilie kumeza chakula kabla hujatafuna utaumia koo.
 
Armata, tulia utafune chakula, halafu kama chakula hicho ni kitamu basi wewe wameza tu.

Usikimbilie kumeza chakula kabla hujatafuna utaumia koo.
Usilete misemo, leta namna Pompeo atakavyohakikisha usalama katika tukio la kuapisha. Pompeo ni special force au jasusi? Si ni secretary atakayevaa suti na kukaa jukwaani. Yeye ndiye anaenda kulindwa pale, yani anaongeza mzigo kwa Mossad na polisi.
 
Usilete misemo, leta namna Pompeo atakavyohakikisha usalama katika tukio la kuapisha. Pompeo ni special force au jasusi? Si ni secretary atakayevaa suti na kukaa jukwaani. Yeye ndiye anaenda kulindwa pale, yani anaongeza mzigo kwa Mossad na polisi.
Nadhani uwepo wa Pompeo ni kuonyesha uungaji mkono wa Marekani katika makubaliano hayo.

kumbuka ule mpango wa amani ya Mashariki ya kati uliobuniwa na Trump ambao wapalestina wameukataa ila serikali ya awali ya Netanyau iliukubali, huenda hii serikali mpya ya Israel itaendelea kuunga mkono.
 
Mzee Trump ameshindwa kushiriki hafla hii muhimu? Mapenzi yake kwa taifa teule la Yakobo ni ya kupigiwa mfano na kila mpenda amani.
 
Nadhani uwepo wa Pompeo ni kuonyesha uungaji mkono wa Marekani katika makubaliano hayo.

kumbuka ule mpango wa amani ya Mashariki ya kati uliobuniwa na Trump ambao wapalestina wameukataa ila serikali ya awali ya Netanyau iliukubali, huenda hii serikali mpya ya Israel itaendelea kuunga mkono.
Hii statement ndio iko sahihi. Sio eti Pompeo anaenda kuimarisha usalama kwenye uapishaji kama mleta mada alivyosema.
 
Mzee Trump ameshindwa kushiriki hafla hii muhimu? Mapenzi yake kwa taifa teule la Yakobo ni ya kupigiwa mfano na kila mpenda amani.
Kwahio mataifa mengine sio mateule

Elimu Mlizosoma Simeshindwa Kuwakomboa Aseee.....

Sent using My COVID-19
 
Hii ni fursa ya Iran kulipa kisasi cha General mkakamavu Soleimani, Pompeo kajileta mwenyewe anga za middle East, sasa Iran wafanye kweli. US walidondosha mtu mzito mno sasa ni zamu yao, Pompeo hachomoki middle East.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usilete misemo, leta namna Pompeo atakavyohakikisha usalama katika tukio la kuapisha. Pompeo ni special force au jasusi? Si ni secretary atakayevaa suti na kukaa jukwaani. Yeye ndiye anaenda kulindwa pale, yani anaongeza mzigo kwa Mossad na polisi.

NImetumia neno utulivu na sio usalama.

Hayo ni maneno mawili tofauti.

Nina uhakika akili yako hujaiazima popote pale.

NImesema Pompeo katumwa na Trump kuhakikisha kunakuwepo utulivu katika shughuli nzima hadi kuapishwa serikali mpya ya mseto.

Israeli pamekuwepo tatizo la kisiasa (political deadlock) ambapo Netanyahu na Gants wamekuwa wakivutana juu ya kuunda serikali mpya ya mseto.

Pil, kuna suala la kuhakikisha ukanda wa magharibi kuwa unahodhiwa na Israeli kwa asilimia 30 linatekelezwa kama raisi Trump alivyopanga.

Gantz aliingia siasa miaka miwili ilopita kwa ahadi ya kumtoa Netanyahu lakini suala la COVID-19 na mgongano wa kisiasa limekuwa linavuta muda.

Hivyo kamtuma Pompeo kwenda Jarusalem na kuhakikisha kunakuwepo utulivu (kati ya Netanyahu na Gantz) na wanahakikisha serikali mpya inaapishwa leo jioni.

Soma tena mada uelewe.
 
Back
Top Bottom