Serikali: Mradi wa SHULE BORA utawafikia Wanafunzi 3,800,000 na Walimu 54,000

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,789
11,930
SHULE BORA ni mradi wa Serikali ya Tanzania unaofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo la UKAID wenye lengo la kukuza na kuboresha ufundishaji na ujifunzaji shuleni ili kuboresha Elimu na kuhakikisha watoto wote wa Kitanzania wa kike na wa kiume wanapata elimu bora.

Akizungumzia mradi huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin J. Rwezimula amesema “Mtaji mkubwa wa mradi huo umewekwa katika kuendeleza rasilimali watu kuanzia Elimu ya Awali na Msingi.”

Rwezimula.jpg

Ameongeza kuwa uandaaji wa rasilimali watu unajumuisha uandaaji na uendelezaji wa program na mikakati mbalimbali inayolenga kuongeza maarifa na ujuzi Nchini katika ngazi ya elimu ya Awali hadi ya Juu ili kuwawezesha vijana kujenga uchumi mara tu baada ya masomo.

Amesema Serikali imetenga fedha katika utekelezaji wa hatua mbalimbali na kuweka mazingira ya vutivu kwa wahisani na wadau mbalimbali wa elimu.

Mradi huu una thamani ya Shilingi bilioni 271 (Paundi Milioni 89) na unatekelezwa katika kipindi cha miaka 6 kuanzia Mwaka 2021 hadi 2027.

Fr-rusfXwAMyddF.jpg

Ameeleza malengo ya jumla ni kuimarisha ubora wa elimu, uimarishaji mifumo ya usimamizi na ufuatiliaji na tathimini na kuweka mazingira salama ya kufundisha na kujifunzia.

Mradi huo unatekelezwa katika Mikoa Tisa (9) ya Tanzania Bara ambayo ni Katavi, Rukwa, Dodoma, Singida, Mara, Simiyu, Pwani, Tanga na Kigoma.

Jumla ya Halmashauri 67 na zaidi ya Shule za Msingi za Awali 5,757 zitanufaika na utekeleza wa mradi huo.

Amesema “Takribani Wanafunzi 3,800,000 na Walimu 54,000 watafaidika katika program hiyo.”

Ametoa wito kwa waratibu kushirikisha wadau wa habari na wengine wanaohusika na kuacha kuficha taarifa muhimu kwa Wananchi.
 
Back
Top Bottom