Serikali mnaficha nini richmond-cheyo


P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
39,870
Likes
8,691
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
39,870 8,691 280
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali, John Cheyo, ameitaka serikali kuweka bayana ukweli kwamba Kampuni ya kufua umeme ya Richmond haikupewa fedha yoyote badala ya kuacha suala hilo likiendelea kuzungumzwa bila mwisho.

“Kwa nini hili jambo lisisisemwe? Kwa nini tunaishi kwenye giza? Tunakwenda uchaguzi na Richmond, tunarudi na Richmond. Kwa majibu, hakuna malipo yaliyotolewa, sasa tunagombana nini,” alisema Cheyo.

Alitoa kauli hiyo jana wakati kamati yake ilipokutana na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na Katibu Mkuu, David Jairo aliyewaambia wabunge kuwa miongoni mwa mambo yanayohitaji utekelezaji, ni kutengeneza jina zuri la wizara yake baada ya kusakamwa na mambo mengi na kuwa gumzo la kila siku.

Jairo alitaja mambo ambayo yamefanya wizara hiyo isakamwe kuwa ni suala la Richmond na Dowans pamoja na IPTL na akasisitiza kwamba jambo la msingi litakalozingatiwa ni kufanya kazi kwa uwazi na kuepuka kuiletea aibu.

Cheyo ambaye kamati yake iliwahoji watendaji hao maswali mbalimbali sanjari na kupendekeza Wizara igawanywe ziwe mbili ili kurahisisha utendaji, alishauri ufafanuzi kuhusu Richmond utolewe bayana baada ya Katibu Mkuu kuhojiwa kuhusu agizo namba tisa la kutaka wizara ieleze kama serikali haikupata hasara kutokana na Richmond.

Katika kujibu, ilielezwa kwamba serikali haikupata hasara na kwamba kinyume chake, Richmond ilipewa adhabu kwa kuchelewa kufikia mkataba wa kuzalisha umeme katika wakati uliopangwa kulingana na makubaliano yaliyowekwa kwenye mkataba.

Majibu hayo ambayo hata hivyo yalikosewa kwa kuitaja Richmond badala ya Dowans, yalisababisha baadhi ya wabunge akiwemo Mbunge wa Mpendae, Issa Kassim Issa (CCM) na Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Owenya (Chadema) kuhoji kwa kutaka kufahamu undani wa mchakato uliozingatiwa katika kufanya malipo mbalimbali kwa Richmond.

Baada ya Kaimu Ofisa Mkuu wa Fedha wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Anitha Chengola kufafanua kwamba shirika lake halijawahi kulipa malipo kwa Richmond, Cheyo alielekeza kwamba vipo vitu ambavyo Serikali inapaswa kuweka bayana kuliko kuwaacha watu kuendelea kusema.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Sophia Simba, katika mkutano wa Bunge wa Juni mwaka jana, wakati akijibu juu ya hoja za watu mbalimbali za kutaka watuhumiwa wa Richmond wafikishwe mahakamani, aliweka bayana kwamba kampuni hiyo haikulipwa fedha yoyote.

Simba alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka bungeni aliyetaka Serikali kuchukua hatua za utashi wa kisiasa kwa kuwachukulia hatua za haraka watuhumiwa wa Richmond, Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu (BoT) na IPTL ili kuweka nchi katika sura nzuri ya kupambana na rushwa.
 
ELNIN0

ELNIN0

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2009
Messages
3,866
Likes
309
Points
180
ELNIN0

ELNIN0

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2009
3,866 309 180
Serikali ilijiuzuru kwa hili soo la Richmond, sasa bado mnataka nini tena - roho ya mtu?

Richmood si mnamjua - kigogo hagusiki yule. Tuache hayo tuanze ukrasa upya ili yale yasije yakatokea tena.

Waugwana hawana visasi ila huwa wanadhibiti mabaya yaliyopita yasirudie tena hali kadhalika EPA na mengineyo. tufungue ukurasa mpya 2010 watanzania wenzangu.

kukazania Richmood, EPA na mengineyo hayatafanya maisha yetu yawe bora, cha msingi ni kuangalia mfumo mzima uliopo, pamoja ya hili za zanzibar ili wenzetu wasikaangane kama mishikaki kwenye uchaguzi ujao.

2010 - NEW CHAPTER........
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
197
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 197 160
Wakubwa wanaogopa kumwagana kwa wazo kua ukimwaga mboga nami namwaga ugali, wanajua Lowassa anajua maovu yao mengi tu, na kuna habari kuwa anawasikilizia watachukua hatua gani dhidi yake na marafiki zake ili nae aingie vitani rasmi, siunajua baada ya kuporomoka kwake yeye na karamagi wakafungua vijigazeti fulani uchwara wakishirikiana na magazeti ya New Habari cop, ili kuwaangamiza wale wote wanaopingana nao .
 

Forum statistics

Threads 1,237,470
Members 475,533
Posts 29,289,704