Serikali mmetutelekeza na mbaazi basi ruhusuni tuuze nje mahindi ili tupate pesa ya pembejeo za msimu mpya.

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
10,939
28,375
Wakuu.

Tukubali jamaa wametutelekeza wakulima wa mbaazi nchi nzima , hawajatuacha njia panda , wametuacha kwenye mataa hivo hiyo hasara tulie nayo , ruhusuni tuuze mahindi kidogo nje ili tugharamie msimu mpya wa kilimo , au fungeni mipaka mahindi ya Zambia yasiingie ndani ya nchi msitutie umaskini wa lazima.
 
Ni genge la wanafiki, mtasubiri sana. Wanasubiri jambo lenye ku-kick waje wafanye maigizo hadharani na kusifiwa ilhali hamna lolote raia wanateketea huku. Kuna mbuzi sio raia wa nchi hii wanatutamani eti..
 
Suala la kuruhusu mahindi ya nje ya tanzania yaingie nchini tena yanauzwa kwa bei rahisi huku ya hapa kwetu wakigoma yasitoke nje sio fair.

Mahindi ya zambia yanaingia nchini,kwa bei ya 4000- 6000 kwa debe moja,mahind ya hapa kwetu ni 7000-8000 watu wananunua ya zambia ya hapa watu hawayauzi wateja hamna.

Sasa hapo sijajua wanawasaidiaje wakulima na wafanyabiashara wa mahindi. Wachukue hatua watu watashindwa kulima msimu huu.
 
Hii si ndo Serikali ya kutetea wanyonge!!!! Mbaazi zisageni mzipike uji na ugali. Na mahindi hamtauza nje. Serikali bado inaendelea kuwatetea wanyonge wakulima na wafanyakazi!!!
 
mkuu inasikitisha sana, mwaka huu uku kwetu watu wameacha mbaaz shamban bila hata ya kuvuna, mbaazi kilo tsh 80-150??? alafu bado wanasema vijana tujiajiri, how ????
 
Ni genge la wanafiki, mtasubiri sana. Wanasubiri jambo lenye ku-kick waje wafanye maigizo hadharani na kusifiwa ilhali hamna lolote raia wanateketea huku. Kuna mbuzi sio raia wa nchi hii wanatutamani eti..
Hawaeleweki ujue
 
Back
Top Bottom