Serikali mmekurupuka uamuzi wa level seat mnagombanisha abiria na trafiki

Wamajanga

Senior Member
Jun 24, 2014
133
47
Yaani ni hivi jeshi la usalama barabarani nilisikia limetangaza kuwa ni marufuku kupandisha abiria wengi na mpaka kusimamisha hiyo ni nzuri kwa gari nyingine ila si kwa daladala zinazofanya kazi zake dar es salaam mana gari zilizokuwepo tu hazitoshi hasa haya maeneo ya mbagala,gongo la mboto,mbezi,tegeta na kwingineko sasa hiyo amri yao itawapa tabu sana wakazi wa dar na wajue hawatusaidii ila wanatutesa na nahisi hawajui tabu tunayoipata
Wasiwe watu was kuamka na kukurupuka mnatuumiza sisi watu wa chini.
Nahisi tumeelewana
 
Town bus kusimama hakukwepeki nendeni ulaya mtaona town basi watu wanasimama sasa ndio Tanzania ? Haya mabasi wa mwendo kasi wameyadesign wengi wazimame wachache wakae
 
nivema mamlaka husika likaliangalia kwa kina swala hilo maana ningumu kutekelezwa hususa dar kama wanataka wa ulete ukolon tena Tz sawa ila kukurupuka sio dili
 
Hayo mabasi ya mwendo kasi pia yanaoptions za watu kusimama...yaan unasimama huku umeshika vile vishikizi...hii kusimama ipo kuanzia marekan ulaya china south africa...sasa leo hapo kwa mfuga mbwa ndo ipigwe marfuku...mbona siamin...
 
Mbona hii hamsemi Nairobi? kule ukisimama kila mtu ana faini yake, konda, abiria mpaka dereva ..daladala zikiwa nyingi na treni za town zikaanza tunaweza na sisi tuwe mfano wengine waige kwetu, si lazima tuige kwa wenzetu daily.
 
Mbona hii hamsemi Nairobi? kule ukisimama kila mtu ana faini yake, konda, abiria mpaka dereva ..daladala zikiwa nyingi na treni za town zikaanza tunaweza na sisi tuwe mfano wengine waige kwetu, si lazima tuige kwa wenzetu daily.

Nairobi ni tofauti na hapa kwetu inawezekana miundo mbinu yao ni mizuri kuliko ya kwetu vile vile magari ni na population ndogo kuliko yetu tusipende kujilinganisha na wengine wakati tupo nyuma sana.
 
May Walete Basi Nyingi, Halafu private car zisiwepo, don't quote me wrong, I have a car, lakini tunaweza tukawa ktk foleni tupo may be Gari 500 lakini kila Gari ina abiria moja au 2, lakini je tukitumia public inaweza ikawa Gari 10 tuuu
 
Hao wenye kukaa na kutunga sheria hizo hata daladala hawapandi,hivi kuna mtu anayependa kusimama na kubanana tu kwenye daladala?huko kusimama tu maeneo mengine hadi uwe na nguvu ya kupanda hiyn daladala kwa shida ya usafiri ilivyo halafu ndio mnasema hakuna kusimama.
 
Yaani ni mambo ya ajabu sana yanafanyika ktk nchii hakuna sheria na hizo zilizokuwepo hakuna mtekelezaji mambo ya ajabu kabisa hasa kwa jeshi la police kufanya kazi kwa kukurupuka,
Mie nina wasi wasi uwa hawafanyi utafiti, na wengi wa police zetu hawajawahi kutoka na wala kusoma magazeti au kuangalia tv au majarida, kwani kwa akili za kawaida tuu, uwezi ukafikia maamuzi yanayoenda kugusa maisha ya watu wengi bila kufanya utafiti,
Kwa uzoefu mdogo nilio nao kutokana na kusafiri sehemu tofauti kwa wenzetu ambao wametuzidi mbali kimaendeleo, utaona kabisa wakati wa rush our yaani wakati watu wanaenda na kutoka makazini yaani asubui na jioni mabasi, tren uwa vinakuwa vimejaa abiria kiasi kwamba yote utakuta yamesimamisha abiria ukizingatia wenzetu wamewekeza kwenye usafiri hasa wa mijini kwa kiwango cha juu mnoo, hasa kwa maeneo niliyofanikiwa kufika kama beijing, hongkong, istanbul na karibu miji mitatu au minne mikubwa ya afrika kusini.
Sasa kwa sisi ambao kwanza hatuna hata kampuni moja ya umma unayotoa usafiri na ambayo kwanza inaendeshwa yaani kwa ruzuku, miundombinu mibovu, na aina ya vyombo tunavyotumia kubeba abiria ambavyo ni vidogo kwa ujazo na hata kukiwa hakuna foleni hafikidhi viwango, ondolea mbali vyote vina milikiwa na wamiliki binafsi ambao hawapati ruzuku. Toka serikalini na hao police ndio wanaongoza kuwabuguzi madereva na makondakta wa daladala,
Sasa kwa sababu kama hizo chache hapo juu utaona jinsi gani polisi wanadhamilia kuwaongezea wanainchi usumbufu ambao tayari wanao miaka mingi,
Mie ningewashauli tu polisi siku nyingine kabla ya kufikia maamuzi kama haya ni bora mkaenda kwa wenzetu waliotutangulia mkajifunze ili mtoe maamuzi yatakayotafuta ufumbuzi na sio kuongeza tatizo,kwani kwa uzoefu nilionao ni kwamba makatazo na maamuzi mengi ya serikali na vyombo vyake vipo kwa ajiri ya kutoa maamuzi ambayo mwisho wa siku ni sisi wanyonge ndio tunaoumia,
Mfano mdogo tena wakijinga, serikali wakati wanatafuta mbimu ya kuzuia au kupunguza uharibifu wa mazingira walikuja na mpango wa kuhakikisha wanapunguza matumizi ya mkaa na kuvipa au kuwapa maafisa misitu mamlaka ya kukagua na kuweka vizuizi vingi kwa wafanyabiashara ya mkaa kiichotokea ni kwamba kipimo kimoja kilikuwa kinauzwa sh 500 kikapanda mpaka sh2000 sasa kwa mfano huo tuu mdogo utaona jitihana za serikali zinavyomdidimiza mtu wa chini bila kufanya utafiti,
Mheshimiwa raisi najua wewe ni mfuatiliaje sana na msomaji sana wa habari iwe ndogo au kubwa, naomba lifanyie kazi suala hili hapa chini
Tanzania ni nchi iliyoruhusu kuingizwa magari yaliyotumika na kitu kilichotumika hakina guarantee hivyo basi kinaweza kuharibika muda wowote pasipokupewa fidia hivyo basi 80% ya magari yote yanayotumika hapa TZ ni chakavu, hivyo basi ili kuzuia rushwa au kupunguza kila daladala inayofanya kazi mijini lazima kuwe na karatasi itakayoelekeza vitu muhimu ambavyo hiyo gari inahitaji kuwa navyo ili iwe na sifa ya kubeba habiria kwa mfano, honi, hendiketa, taa mbele na nyuma, break, hand break, na weiper, pamoja na vibali vingine ambavyo ni kuashiria kwamba serikali inapata kodi zake halali basi na hivyo vitu kila daladala limalobeba habiria liwe nacho kimebandikwa sehemu kwenye gali ili hata habiria wavifahamu ili kuondoa usumbufu unaosababishwa na polisi wa usalama barabarani pindi mnapokuwa safarini kwani bila kufanya hivyo traffik wataendelea kuwa miungu watu kwani hakuna kipengele kinachomfunga, anaweza kusimamisha gali bila sababu akasema gali bovu na ikawa hivyo na kusiwe na mahali popote unapoweza kwenda kulalamika, haya mambo yamewapa kiburi polisi trafik kiasi kwamba wamekuwa miungu watu na kibaya zaidi hii ni kwa manufaa yao,pi a ni mazingira makubwa sana ya rushwa.
Napenda kuwakilisha.
 
Hayo mabasi ya mwendo kasi pia yanaoptions za watu kusimama...yaan unasimama huku umeshika vile vishikizi...hii kusimama ipo kuanzia marekan ulaya china south africa...sasa leo hapo kwa mfuga mbwa ndo ipigwe marfuku...mbona siamin...

Ona huruma basi kidogo kwa Tanzania ,eti hapo kwa mfuga mbwa hahaha
 
Aaaaah aisee yaaan haya maisha dsm haiwezekan kabsa hiko kitu....! Sana sana raia watazichapa na polisi mchana kweupe...!

Mimi sijui viongozi wetu wanaiga nini cha maana kutoka kwa hayo mataifa yaliyo endelea ,yaani unapiga marufuku watu kusimama wakati magari yenyewe ni machache na pamoja na uchache huo foleni ni kiama ,je ukiongeza magari ili kukizi haja ya level seat ,Dar patapitika ????
 
Mi nashauri kwnza wangefanya utafiti ni kwanini abiria wanasimama, then majibu yake yangewapa muongozo nini cha kufanya badala ya kukurupuuka tu
 
Aina ya daladala zinazotumika kimuundo haziruhusiwi kusimamisha abiria ila muunda ungekuwa wa mabasi makubwa kwa design ya kuweka vishikio juu unaruhusiwa kama wanavyofanya nchi za ulaya.Hapa kwetu inatakiwa mfumo.ubadilike wa uendeshaji wa kuchukua abiria ambapo kwenye mazingira yetu yanaitajika mabasi makubwa au tren zinazoweza.kuchukua watu wengi.kwa wakati mmoja.Tanzania ni nchi ambayo bado iko kwenye mfumo wa mtu binafsi kujinunulia basi analotaka na kulitumbukiza barabarani akishapata vibali bila kuanisha standards za mabasi zinazotakiwa.Nchi nyingi kwa sasa ili kuondoa dhana hiyo uwataka watu binafsi au manisipaa za majiji au mji kuanzisha kampuni ya usafirishaji na watu ama kupeleka mabasi yao kwa standard inayotakiwa au kununua hisa.Kwa staili tuliyonayo lazima usafiri Dar uwe kizungumkuti hata kama tunabarabara za juu kwa juu.Duniani kote hakuna barabara zilizotosha ila ni mfumo uwekwa vizuri.Sina shaka wataalam wataifanyia kazi kwani sasa tuna DART serekali inatakiwa iwaweke watu wabunifu na isiwe vyeo vya kisiasa
 
Back
Top Bottom