Serikali mmechonga vinyago msiviogope. Viongozi wa Kiroho sio jukumu lao

Standards Person

JF-Expert Member
Apr 22, 2021
498
1,000
Kupitia vyanzo mbalimbali vya habari imeripotiwa kwamba jana tarehe 09/052021 Mh. Kasim Majaliwa Waziri Mkuu wa JMT alikua wilayani Lushoto kwenye kusimikwa kwa askofu Msafiri Mbilu wa KKKT usharika wa kaskazini mashariki.

Jambo ambalo amewasisitizia viongozi wa dini nikuqaasa vijana wawe makini na janga la Ukimwi. Hapo amenena vyema sana na abarikiwe kwani anaokoa nguvu kazi na kuokoa vifo.

Jambo jingine amewaomba viongozi wakemee maovu na uvunjifu wa maadili. Nukta hii imenipa msukumo wa kutoa maoni yangu.

Mh. Waziri mkuu anatakiwa afahamu kwamba wapo baadhi ya wavunja maadili wakubwa wamewalea,wakawasifia na wengine wakapongezwa. Sasa mnapowaomba viongozi wa dini wakemee watu wenu mlio waweka hiyo sio sawa. Nitatoa mfano.

. Je anayoyafanya Ndugai na Tulia ndani ya bunge serikali na chama hamuyaoni? Au mnaona nisawa? Watu kujiwekea kinga kwamba hawataguswa kwa kushtakiwa hata wafanye nini wakiwa ndani ya ofisi maana yake ni nini? Hayo sindio maovu ya kukemewa? Kuna maovu gani ndani ya nchi yanayozidi ubabe na ubaguzi ikiwemo kutukanana matusi?

.Aliyoyafanya Makonda kuvamia studio na silaha za kijeshi mlimfanyaje?Tena waliopiga kelele dhidi yake wakatulizwa na tuliona je hayo nayo mnawaachia mashehe na mapadri wakemee?

.Kasesela kule Iringa juzi ametoa lugha chafu hamumgusi mnatupa ujumbe gani wanajamii? Au ndio asubirietu huo mkeka mnaosuka?

.Ole Sabaya anaishi kama mwana mfalme mmeshaambiwa anaweka watu ndani kwa uonevu na RC wake mama Anna Mgwira amesema hadharani je mmemfanyaje Sabaya?

.Walichofanya BASATA chini ya Bashungwa hamjakiona? Leo nikajua mpaka saahizi tungesema Bashungwa ameliwa kichwa badala yake Waziri mkuu anasema Basata watoe taarifa. Mbona mnafanya siasa kila mahali?
Ona sasa walichofanya wadau wa mpira juzi kila mtu analalamika,simba na Tanga wanalalamikiana,TFF wanasikitishwa na kilichotokea,Bodi ya mpira sijui nao wanasikitika,wizara hisika nao hawajielewi,waziri mkuu nae anasikitika.Kwahiyo viongozi wrote wanasikitiaka sijui wapenzi na mashabiki wa mpira nao wafanyaje. Hiyo wizara na viongozi wote wa kisiasa hapo fumua.

.Ubadhirifu alioripoti CAG mmewafanyaje watuhumiwa? Yule mkurugenzi wa bandari mama Kafanya yake je wakurugenzi wengine bado mnawaomba wawajibike wenyewe?

Yule DED wa Bahi bado yupo au mmemuwajibisha? Au hela iliyopotea ni kidogotu haina shida? Au kuna watu na majitu?

.Wananchi wa Tanga wanaripoti kuporwa ardhi, kunyanyaswa na kudhalilishwa na mkurugenzi na watu wa ardhi na Takukuru wanakula nao pamoja ikiwa RC na DC wanajua na wamejifungia wanachunguliatu kwenye madirisha watu wakipita au hamuoni mitandaoni?

Ummy Mwalimu kufanya uonevu wa kusimamisha wakurugenzi wengine kazi akimuacha wakwake Tanga mjini mwenye tuhuma kibao au hamuoni raia wakilalamika na aina za rushwa zinazotumika Tanga? Hamjui kama Tanga mtumishi akiiba na mkurugenzi anapandishwa cheo?

Binafsi ninaona mmechonga vinyago vyenu sasa vinawatisha. Natamani ningekua na rungu kama la Kassim Majaliwa ningewaponya walio umizwa.

Inakuaje umpe askofu kazi ya kukemea watu ambao mmewaweka nyie na nyie ndio mnawapongeza wakifanya uonevu?

Kwanini Makonda alipewa ukuu wa wilaya maratu baada ya kumchapa makofi mzee Sinde Warioba?. Haiwezekani watu muwapongeze kwa ubabe,vitisho na dhulma kisha muwape viongozi wa dini kazi ya kukemea.

Ondoeni vikwazo vyenu mlivyovilea muwaachie viongozi wetu wa dini watujenge kiroho na kutuhubiria pepo na mema yake

Ushauri kwa Mh. Raid
Mama hao wanakuchukulia pia wakidhani kwamba wao ndio Tanzania na Tanzania ni wao. Kwanza vunja baraza la mawaziri yani mama watakuheshimu hao wanasiasa na watafanya kazi kwa kufuata kanuni

Kazi Iendelee

Kwenu wanajukwaa kwa maoni zaidi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom