Serikali mkoani Mwanza imepinga Pamba kuuzwa shilingi 1100 kwa Kilo

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
pamba.jpg

Siku moja baada ya Bodi ya pamba Tanzania kufungua msimu wa ununuzi wa zao hilo kwa wakulima wa mikoa 15 ya kanda ya ziwa na magharibi, serikali mkoani Mwanza imepinga bei ya shilingi 1100 iliyotangazwa na bodi hiyo na badala yake imeagiza kampuni zinazonunua zao hilo katika mkoa huo kuwalipa wakulima bei ya shilingi 1300 kwa kila kilo moja ya pamba.

Mjadala mkali umeibuka kati ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya pamba Tanzania Michael Mutunga kuhusu bei elekezi ya shilingi 1100 iliyokuwa imetangazwa na bodi hiyo,ambapo Mongella amesema serikali haiko tayari kujaribiwa na wanunuzi wa zao hilo.

Mwenyekiti wa kikao cha kujadili maendeleo ya sekta ya pamba mkoani Mwanza John Mongella,pia ameagiza wakuu wa wilaya kuwakamata na kuwafungulia mashitaka wanunuzi watakaoenda kununua pamba bila utaratibu wa kupitishwa na halmashauri husika.

Sakata la kampuni ya Alliance iliyoingia mkataba na wakulima wa wilaya ya Magu, ambayo inadaiwa kushindwa kuwasaidia wakulima kwa kuwakopesha mbegu na madawa ya kuulia wadudu wanaoshambulia zao la pamba, limetawala mjadala huo baada ya mkuu wa mkoa kuagiza kampuni hiyo isiruhusiwe kununua pamba wilayani humo kwa kushindwa kutimiza masharti ya mkataba huo


Chanzo: ITV
 
Sasa wanunuzi wasiponunua huyo Mh RC atainunua na akinunua ataichambulia wapi? Je! wakulima watapaje hela ya kujikimu badala ya mauzo ya pamba?
 
Wakulima Waachwe wauze pamba yao kama wanaona ni sawa mambo gani haya ya kupangiana kila kitu
 
Back
Top Bottom