Serikali mkoani Lindi imekiri kudaiwa TZS Billioni 6.9 za wakulima wa korosho ambao hawajalipwa 2018/2019

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,295
16,997
Serikali mkoani Lindi imekiri kua inadaiwa na wakulima wa korosho kiasi cha Bilioni 6.9 za wakulima wa korosho kwa msimu wa 2018/2019.

Wakulima hao ni wale serikali ilichukua korosho zao na kuahidi kuwalipa ila hadi sasa hawajalipwa.

Serikali inadai sababu kubwa ya kuchelewa kuwipa ni kutokana na uhakiki lakini pia ukosefu wa fedha.

Serikali imewaomba radhi wakulima na imeahidi kuwalipa punde tu pesa zitakapopatikana, imewaomba wawe wavumilivu pesa ikipatikana watalipwa.

=======

Serikali yakiri kudaiwa bil. 6/- malipo korosho

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Godfrey Zambi, wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri (RCC) kilichofanyika mjini hapa.

Zambi alisema hayo kufuatia wajumbe kutaka wapewe maelezo kinachokwamisha wakulima wa korosho mkoani humo kutolipwa fedha zinazotokana na uuzaji korosho kwa msimu wa mwaka 2018/2019.

Akijibu hoja za wajumbe hao, alisema katika madai hayo, wapo wakulima waliokwisha lipwa sehemu ya fedha zao na wengine bado hawajalipwa huku akitaja sababu kubwa kuwa ni utaratibu wa uhakiki.

Aliwaambia wajumbe wa kikao hicho kwamba wakulima wa korosho ambao bado hawajalipwa wanadai Sh. 4,869,550,801 huku waliopunguziwa kulipwa wanadai Sh. 1,224,493,477.

Akitaja viwango kwa kila halmashauri, alisema Liwale ndiyo inayoongoza wakulima wake kudai Sh. 1,771,544,094 ikifuatia Nachingwea, Sh. 1,605,348,226, Ruangwa Sh. 1,398,682,428, Lindi Vijijini Sh. 669, 973,916, Kilwa Sh. 599,544,924 wakati Manispaa ya Lindi, wakidai Sh. 48,453,690.

Alisema ucheleweshwaji huo, umechangiwa na mambo mbalimbali, yakiwamo uhakiki ili kuwafahamu wahusika halisi wanaostahili kulipwa fedha hizo, huku akisisitiza serikali kutambua deni la wakulima hao na litalipwa fedha zitakapopatikana.

“Tunajua wamechelewa kulipwa, lakini tunawaomba wavumilie na pale fedha itakapopatikana watalipwa,” Zambi alisisitiza.

Awali, wakichangia hoja katika kikao hicho, wabunge Hamidu Bobari (Mchinga), Mohamedi Kuchauka (Liwale) na Selemani Said Bungara (Bwege) (Kilwa kusini), walihoji sababu za wakulima wa korosho kuchelewa kulipwa fedha zao zinazotokana na uuzaji wa zao hilo, msimu wa mwaka 2018/2019.

Chanzo: Nipashe
 
1 siti.

Nashkuru wazee wangu walipata ila wengine wanaugulia moyoni.

Wawe na subra tu kiza kikiwa totoro ndo kunakucha.

Mzigo ukiwa mzitoo ndo unafika huo.

Kilima kikiwa kikubwa mno ndo mtwremko wake uko karibu tena mkaliii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali hii hii inayonunua "birds" kwa cash I nashindwa kuwalipa wakulima shs Bil 6.9?. Mkuu wa mkoa anaposema pesa zitakapopatikana anataka kusema kwa sasa Serikali ya awamu ya tano imekaukiwa!!!!
Mwenye fedha utamfahamu kwa matumizi yake na hakopi hovyo hovyo.Hawa wanatamba wanazo ila wanakopa na wanaomba misaada ya viwanja vya michezo na nyumbani za ibada.Maajàbu ya Dunia.
 
Siku PM anatoa taarifa pale ikulu kwamba ameshapata wafanyabiashara wa kununua korosho Jiwe alimkatisha haraka haraka na kumwambia achana nao hao watatuchelewesha, serikali itanunua tena kwa bei nzuri.
Haya sasa, hayo ndiyo matokeo ya kutumia fomula za Kemia kwenye biashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hi.jpg
 
Serikali mkoani Lindi imekiri kua inadaiwa na wakulima wa korosho kiasi cha Bilioni 6.9 za wakulima wa korosho kwa msimu wa 2018/2019.

Wakulima hao ni wale serikali ilichukua korosho zao na kuahidi kuwalipa ila hadi sasa hawajalipwa.

Serikali inadai sababu kubwa ya kuchelewa kuwipa ni kutokana na uhakiki lakini pia ukosefu wa fedha.

Serikali imewaomba radhi wakulima na imeahidi kuwalipa punde tu pesa zitakapopatikana, imewaomba wawe wavumilivu pesa ikipatikana watalipwa.

=======

Serikali yakiri kudaiwa bil. 6/- malipo korosho

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Godfrey Zambi, wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri (RCC) kilichofanyika mjini hapa.

Zambi alisema hayo kufuatia wajumbe kutaka wapewe maelezo kinachokwamisha wakulima wa korosho mkoani humo kutolipwa fedha zinazotokana na uuzaji korosho kwa msimu wa mwaka 2018/2019.

Akijibu hoja za wajumbe hao, alisema katika madai hayo, wapo wakulima waliokwisha lipwa sehemu ya fedha zao na wengine bado hawajalipwa huku akitaja sababu kubwa kuwa ni utaratibu wa uhakiki.

Aliwaambia wajumbe wa kikao hicho kwamba wakulima wa korosho ambao bado hawajalipwa wanadai Sh. 4,869,550,801 huku waliopunguziwa kulipwa wanadai Sh. 1,224,493,477.

Akitaja viwango kwa kila halmashauri, alisema Liwale ndiyo inayoongoza wakulima wake kudai Sh. 1,771,544,094 ikifuatia Nachingwea, Sh. 1,605,348,226, Ruangwa Sh. 1,398,682,428, Lindi Vijijini Sh. 669, 973,916, Kilwa Sh. 599,544,924 wakati Manispaa ya Lindi, wakidai Sh. 48,453,690.

Alisema ucheleweshwaji huo, umechangiwa na mambo mbalimbali, yakiwamo uhakiki ili kuwafahamu wahusika halisi wanaostahili kulipwa fedha hizo, huku akisisitiza serikali kutambua deni la wakulima hao na litalipwa fedha zitakapopatikana.

“Tunajua wamechelewa kulipwa, lakini tunawaomba wavumilie na pale fedha itakapopatikana watalipwa,” Zambi alisisitiza.

Awali, wakichangia hoja katika kikao hicho, wabunge Hamidu Bobari (Mchinga), Mohamedi Kuchauka (Liwale) na Selemani Said Bungara (Bwege) (Kilwa kusini), walihoji sababu za wakulima wa korosho kuchelewa kulipwa fedha zao zinazotokana na uuzaji wa zao hilo, msimu wa mwaka 2018/2019.

Chanzo: Nipashe

Si tuliambiwa wakulima wote walishalipwa?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom