Serikali mko kimya nini hatima ya mrundikano wa wahitimu wa vyuo na wako mtaani?

Mzee wa kusawazisha

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
1,587
1,136
Inasikitisha Sana kuona wimbi kubwa la vijana wanasaidia fundi, wengine mama ntilie wengine madereva boda boda, bajaji hivi ndo zao ndo kusema zimeshafifia?

Mimi mmoja wapo Lakin nipo private institution at least napata cent japo kabla ya hapa nimesota mtaani mwaka 1 karibuni tujadili labda Serikali itaoa mwongozo maana wapo humu
 
Inasikitisha Sana kuona wimbi kubwa la vijana wanasaidia fundi, wengine mama ntilie wengine madereva boda boda, bajaji hivi ndo zao ndo kusema zimeshafifia? Mimi mmoja wapo Lakin nipo private institution at least napata cent japo kabla ya hapa nimesota mtaani mwaka 1 karibuni tujadili labda Serikali itaoa mwongozo maana wapo humu
Nyie sio makada nyie mnalilia nini sasa nendeni Lumumba mkachukue buku7
 
Ulimwengu tuliopo ni wa kibepari, kwenye ujamaa tulishatoka; sasa ni juhudi kwa kila kijana kusoma fani inayomuachia ujuzi ili aweze kujiajiri
 
Serikali haiwezi kuajiri wahitimu wote. Hakuna serikali duniani yenye uwezo huo. Wajibu mkuu wa serikali ni kuandaa sera nzuri, kukuza uchumi na kuandaa mazingira mazuri ili vijana waweze kujiajiri. Mwajiri mkuu duniani kote ni sekta binafsi. Kama ni kuilaumu serikali basi ilaumiwe kwa kushindwa kuandaa mazingira rafiki kwa vijana kuweza kujiajiri/kuajiriwa katika sekta binafsi.
 
Mnatakiwa mjiajiri vijana, ila cha ajabu hakuna mtaji, cha ajabu kingine ni kwamba mkipata mtaji mnashindwa ku manage, mtu anapewa 2m unaanza mawenge hadi inaisha
 
Inasikitisha Sana kuona wimbi kubwa la vijana wanasaidia fundi, wengine mama ntilie wengine madereva boda boda, bajaji hivi ndo zao ndo kusema zimeshafifia?

Mimi mmoja wapo Lakin nipo private institution at least napata cent japo kabla ya hapa nimesota mtaani mwaka 1 karibuni tujadili labda Serikali itaoa mwongozo maana wapo humu
Kazi kubwa ya serikali ni kukusanya kodi. Haiwezi kuajili kila mtu, hali ya ukosefu wa ajira ipo kila sehemu duniani ingawa tofauti ni ukubwa wa tatizo. Hali ya uchumi wa taifa letu kwa sasa ni mbaya, hivyo nafasi za ajira ni chache sana ukilinganisha na uhitaji. Tunahitaji kukubaliana na hali halisi na kupambana kwa namna yoyote bila kutegemea serikali. Kwa hali iliyopo sasa, umri wa kustaafu unaweza kufika bila kupata ajira. KWA SASA KUNA HAJA YA KUFUTA KABISA NENO AJIRA KATIKA AKILI ZETU. Ukibahatika kupata ajira ni vizuri sana ila sio jambo la kutegemea sana.
 
Back
Top Bottom