My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,283
Tatizo lako una uelewa mdogo mno, huwezi kumfananisha Edward Snowden ,Julian Assange na Eric Kabendera.Nimewasikia CPJ wameiandikia barua serikali ,ni waraka wa kijinga sana kutaka Kabendera aachiwe.
Sijawasikia wakiiandikia British, au Amerika dhidi ya Assange na Snowden kinachoendelea dhidi yao.
CPJ inatumika vibaya sana waziwazi,na walioko nyuma ya CPJ wanajulikana. wanajaribu kulinda maslahi yao kwa kivuli cha haki za waandishi wa habari,kifupi ni mapambano ya vita vya kiuchumi.
Tunataratibu na sheria zetu, pia namna ya kushughulikia makosa ya aina zote kwa mujibu wa sheria za nchi kwa mujibu wa katiba.
Hatuwezi kama nchi kupangiwa namna ya kuandaa mashitaka na kushitaki.
Mahakama zipo na washitakiwa watakua watuhumiwa (innocent) mpaka hapo mahakama itakapomtia hatiani muhusika.
Kabendera kashitakiwa, makosa yake hayana dhamana ndio sheria inavyosema, na hajawekwa kizuizini, kisha fikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka yanayomkabili
Ifike mahala nchi ijisimamie kama taifa huru, wanachotaka kukifanya na wafanye tuwajue dhumuni na rangi yao halisi.
Dunia imejaa double standard sana,umoja wetu na misimamo thabiti ndio itakayo tuvusha,
Lengo lao ni kuona nchi haipigi hatua ya kimaendeleo, wanapenda kuona tukiwategemea wao na kuwapigia magoti, hii ndio furaha yao.
Serikali na sisi wananchi wazalendo tusimame kwa nguvu zote kuhakikisha dola haiingiliwi hovyo na wahuni kwa kigezo cha demokrasia na uhuru wakujieleza ,lazima mipaka iwepo inapoonekana kuna upotoshaji
Edward Snowden siyo mwandishi, ni jasusi wa CIA aliyeikimbia nchi yake na kisha kutoa Siri za nchi.
Julian Assange, ni mmiliki wa mtandao wa wikileaks aliyekuwa akitoa Siri za jeshi la Marekani alizokuwa akipewa na wasaliti.
Sasa Eric Kabendera katoa Siri ipi ya serikali? ni nani asiyejua kuwa Magufuli ni Dikteta hatari Tanzania?
Usilete ushabiki kwa ku expose umbumbumbu.