thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Nimewasikia CPJ wameiandikia barua serikali ,ni waraka wa kijinga sana kutaka Kabendera aachiwe.
Sijawasikia wakiiandikia British, au Amerika dhidi ya Assange na Snowden kinachoendelea dhidi yao.
CPJ inatumika vibaya sana waziwazi,na walioko nyuma ya CPJ wanajulikana. wanajaribu kulinda maslahi yao kwa kivuli cha haki za waandishi wa habari,kifupi ni mapambano ya vita vya kiuchumi.
Tuna taratibu na sheria zetu, pia namna ya kushughulikia makosa ya aina zote kwa mujibu wa sheria za nchi kwa mujibu wa katiba.
Hatuwezi kama nchi kupangiwa namna ya kuandaa mashitaka na kushitaki.
Mahakama zipo na washitakiwa watakua watuhumiwa (innocent) mpaka hapo mahakama itakapomtia hatiani muhusika.
Kabendera kashitakiwa, makosa yake hayana dhamana ndio sheria inavyosema, na hajawekwa kizuizini, kisha fikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka yanayomkabili
Ifike mahala nchi ijisimamie kama taifa huru, wanachotaka kukifanya na wafanye tuwajue dhumuni na rangi yao halisi.
Dunia imejaa double standard sana,umoja wetu na misimamo thabiti ndio itakayo tuvusha,
Lengo lao ni kuona nchi haipigi hatua ya kimaendeleo, wanapenda kuona tukiwategemea wao na kuwapigia magoti, hii ndio furaha yao.
Serikali na sisi wananchi wazalendo tusimame kwa nguvu zote kuhakikisha dola yetu haiingiliwi hovyo na wahuni kwa kigezo cha demokrasia na uhuru wakujieleza ,lazima mipaka iwepo inapoonekana kuna upotoshaji