Serikali mkimuachia Erick Kabendera kwa shinikizo la walio nyuma yake, nitaidharau maisha yangu yote. Onyesheni msimamo thabiti

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,233
9,059
Nimewasikia CPJ wameiandikia barua serikali ,ni waraka wa kijinga sana kutaka Kabendera aachiwe.
Sijawasikia wakiiandikia British, au Amerika dhidi ya Assange na Snowden kinachoendelea dhidi yao.

CPJ inatumika vibaya sana waziwazi,na walioko nyuma ya CPJ wanajulikana. wanajaribu kulinda maslahi yao kwa kivuli cha haki za waandishi wa habari,kifupi ni mapambano ya vita vya kiuchumi.

Tuna taratibu na sheria zetu, pia namna ya kushughulikia makosa ya aina zote kwa mujibu wa sheria za nchi kwa mujibu wa katiba.
Hatuwezi kama nchi kupangiwa namna ya kuandaa mashitaka na kushitaki.
Mahakama zipo na washitakiwa watakua watuhumiwa (innocent) mpaka hapo mahakama itakapomtia hatiani muhusika.

Kabendera kashitakiwa, makosa yake hayana dhamana ndio sheria inavyosema, na hajawekwa kizuizini, kisha fikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka yanayomkabili

Ifike mahala nchi ijisimamie kama taifa huru, wanachotaka kukifanya na wafanye tuwajue dhumuni na rangi yao halisi.

Dunia imejaa double standard sana,umoja wetu na misimamo thabiti ndio itakayo tuvusha,
Lengo lao ni kuona nchi haipigi hatua ya kimaendeleo, wanapenda kuona tukiwategemea wao na kuwapigia magoti, hii ndio furaha yao.

Serikali na sisi wananchi wazalendo tusimame kwa nguvu zote kuhakikisha dola yetu haiingiliwi hovyo na wahuni kwa kigezo cha demokrasia na uhuru wakujieleza ,lazima mipaka iwepo inapoonekana kuna upotoshaji
 
Aisee! Unanikumbusha tulipokuwa form IV term ya mwisho jamaa alipokwaruzana na mamlaka za shule na akapangiwa adhabu ya viboko vitano mbele ya shule nzima. Baadhi ya wenzie wakamshauri asikubali aonyeshe msimamo na wengine wakamwambia akubali tu yaishe, yeye akachagua kukataa na kufukuzwa shule!
 
You seeking helps Wewe pole sana ulitakiwa uwepo pale msavu last week cjuw ulichelewa wp hopeless bastards kabisa
IMG_20190812_114539.jpeg
 
Naungana na mtoa hoja,Tanzania ni nchi huru,haipaswi kuingikiliwa na mabeberu kwa maslahi yao,Kabendera akiachiwa wataibuka wakina kabendera mia moja,na watavuruga mipango ya serikali yote kwana watajua kuna walio nyuma yao watawatetea na serikali itaogopa itawaachiwa,ashikiliwe hivohivo na wala asipelekwe mahakamani leo wala kesho,ili wanaotarajia kuwa wakina kabendera wasifanye kama kabendera original
 
Aisee! Unanikumbusha tulipokuwa form IV term ya mwisho jamaa alipokwaruzana na mamlaka za shule na akapangiwa adhabu ya viboko vitano mbele ya shule nzima. Baadhi ya wenzie wakamshauri asikubali aonyeshe msimamo na wengine wakamwambia akubali tu yaishe, yeye akachagua kukataa na kufukuzwa shule!
..
Mwenye uelewa na akuelewe mkuu.
Hili jbu funzo tosha
 
mkuu hebu chukua nafasi ya Kabendera, unakatwa kisa sio raia, unahojiwa kwa siku nne mfululizo kisha unashitakiwa kwa kosa la utatishaji na uhujumu uchumi utasikiaje?

yaani hata wangemuachia kisha kumkamata tena na kumchukua maelezo ya utakatishaji na uhujumu uchumi walishindwa?

hicho tu ndio kinaleta ukakasi, wala sio jingine. sheria tunazo, tuzitumie kama sheria zinavyotutaka na sio kwa utashi wa mtu
 
Naungana na mtoa hoja,Tanzania ni nchi huru,haipaswi kuingikiliwa na mabeberu kwa maslahi yao,Kabendera akiachiwa wataibuka wakina kabendera mia moja,na watavuruga mipango ya serikali yote kwana watajua kuna walio nyuma yao watawatetea na serikali itaogopa itawaachiwa,ashikiliwe hivohivo na wala asipelekwe mahakamani leo wala kesho,ili wanaotarajia kuwa wakina kabendera wasifanye kama kabendera original
Mkubwa habari za mchana?

Ni vyema kama hutaki kuingiliwa usiingiliwe ki vyovyote vile! Huwezi kataa kuingiliwa kuulizwa maswali lakini unaomba kila siku kuingiliwa kupewa msaada! Chagua upande mmoja na udumu nao. Mdomo huo huo unaosema hutaki kuingiliwa kesho asubuhi unatamka Wazungu ni ndugu zetu tunaomba msaada wa dawa na vyandarua. Mdomo huo huo kesho asubuhi unatamka undugu wa Tanzania na Norway ni wa kihistoria na wamekuwa wanatoa nakisi ya bajeti ya nchi toka mwaka 1961!
 
Sasa ni n
Tatizo ni namna haya mashitaka yalivyopatikana!

Mtu kakamatwa kwa tuhuma kuwa si raia!

Alafu unampeleka mahakamani kwa kosa la kutakatisha fedha!

Hii inasababisha "Extenals kuhoji ueledi wetu wa jinsi tunavyo deal na watuhumiwa.

Sasa si ndo kosa limepatikana, walitafuta mengine yakagoma, likapatikana malipo bila kodi na malipo toka nje kwa kificho, saa wafanyeje? Hata wakimuachia leo kesho atakamatwa kwa hayo malipo maana bado ni kosa atajicherewesha tu.
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom